Kutoa Sadaka Kwa Nia Yake Na Aliyefariki Inakubaliwa?

 

SWALI:

 

Assalam aleykum,

 

Asanteni sana kwa kutupatia nasaha hizi za kila siku Allah (s.w) awazdishieni leo duniani na kesho akhera. Napenda kuuliza hivi je unaweza kutoa sadaka kwa ajili ya aliyefariki na sadaka hiyohiyo kwa ajili yako (yaani sadaka moja ukatoa kwa ajili ya mtu anbaye ni aliyefariki na hiyo hiyo kwa ajili yako?) au inabidi ziwe mbili tofauti?

 

Wabilah tawfiq

 


 

JIBU:

 

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

  

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako zuri kuhusu kutoa sadaka kwa nia yako na aliyefariki.

 

 

Tufahamu kuwa ‘amali zote zinategemea na nia, na pia kuwe na ikhlasi katika jambo hilo. Swali hili ni kama ule mfano wa mtu mmoja kufunga Swawm kwa nia ya kulipa funga ya Ramadhaan na hapo hapo kufunga Swawm ya Sunnah.

 

Kuna ibada ambazo unaweza kufanya hivyo kama kuweka nia ya kuoga kwa ajili ya kuondosha janaba na hapo hapo kwa ajili ya kuoga kwa Swalah ya Ijumaa. Kwa hiyo ukatekeleza nia mbili kwa kitendo kimoja; kuoga mara moja tu.

 

 

 

Ama katika hilo uliloliuliza huwezi kufanya hivyo.

 

Kwa minajili hiyo, inabidi uwe na nia moja ima hiyo sadaka utoe kwa ajili yako au kwa ajili ya aliyefariki aliye jamaa yako. Kwa hiyo, itakuwa ni busara kwako wakati mmoja utoe kwa ajili yako mwenyewe ili upate kwayo thawabu na wakati mwengine utoe kwa nia ya aliyefariki aliye jamaa yako ikiwa ni mama au baba.

 

Bonyeza kiungo kifuatacho upate maelezo zaidi:

 

Kumfanyia Mzazi Aliyefariki Swadaqatun-Jaariyah Inakubalika? Thawabu Anapata Mzazi Au Mtoto?

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share