Mashairi: Umasoni Ni Hatari

                   ‘Abdallah Bin Eifan

                   (Jeddah, Saudi Arabia)

Salamu zangu natuma, zije na nyinyi bukheri,

Tunamuomba uzima, Allaahumma Qahari,

Tumkumbuke daima, Apate kutusitiri,

Umasoni ni hatari, ni chama cha siri sana.

Ni chama cha siri sana, Umasoni ni hatari,

Njama za zamani sana, kimeundwa kihodari,

Na tena werevu sana, wamejiweka tayari,

Umasoni ni hatari, ni chama cha siri sana.

Kuitawala dunia, wapo wakitafakari,

Kila njia hutumia, wamejijenga vizuri,

Na chama kilianzia, Jerusalemu dhahiri,

Umasoni ni hatari, ni chama cha siri sana.

Kazi zao kwa mipango, zinaendeshwa kwa siri,

Upagani na uongo, ndizo wanazohubiri,

Upotofu lao lengo, hakika ni makafiri,

Umasoni ni hatari, ni chama cha siri sana.

Hulenga wenye akili, na khasa maprofesori,

Wakubwa wa serikali, raisi na mawaziri,

Wafalme na wenye mali, wapo kwenye msitari,

Umasoni ni hatari, ni chama cha siri sana.

Na kule Uingereza, ndipo waliposhamiri,

Kituo chao cha kwanza, kilianza mashauri,

Wakaanza kueneza, fikra zao za shari,

Umasoni ni hatari, ni chama cha siri sana.

Thamani ya maadili, wameitia dosari,

Tabia wanabadili, kama nyama kwenye pori,

Wao wanalenga mbali, Dajjaal* wanamsubiri,

Umasoni ni hatari, ni chama cha siri sana.

Alama ya jicho moja, tazama kwenye dollari**

Pia serekali moja, ndivyo wanavyobashiri,

Pia kiongozi mmoja, ndivyo wanavyotabiri,

Umasoni ni hatari, ni chama cha siri sana.

Umasoni, Uzayuni, Uyahudi machachari,

Ni ndugu wa mashetani, wanazo zote habari,

Hueneza upagani, ufisadi na kamari,

Umasoni ni hatari, ni chama cha siri sana.

Wapo wengi wanachama, tena watu mashuhuri,

Inaendelea njama, hufanywa kwa tahadhari,

Na vita vingi tazama, uone yao athari,

Umasoni ni hatari, ni chama cha siri sana.

Na vita vya ukombozi, utawakuta tayari,

Hata kwenye mapinduzi, wao wanatoa amri,

Wao wenye uamuzi, kama dereva wa gari,

Umasoni ni hatari, ni chama cha siri sana.

Kuwatambua vigumu, kawachunguze vizuri,

Mwisho wao jahanamu, wawekwe kwenye tanuri,

Atuepushe Rahimu, hapa nafunga shairi,

Umasoni ni hatari, ni chama cha siri sana.

* Masiyhud-Dajjaal (Bonyeza hapa chini),

Nani Masiyhud-Dajjaal? Ni Mtu Au Jini? Ataingia Kila Kona Ya Dunia?

**Alama ya kuwepo Umasoni ndani ya Marekani inaonekana wazi kwenye sarafu ya dola ambayo inabeba picha ya raisi wa mwanzo wa Kimasoni George Washington, na picha ya alama ya Kimasoni iitwayo "Jicho Moja Linaloona Kila Kitu."

Share