Skip navigation.
Home kabah

Anaweza Kufanyiwa Hajj Ikiwa Hawezi Kwenda Mwenyewe?

SWALI

Mimi ninao uwezo wa kwenda hijja (fedha, afya n.k) lakini ninaishi nchi za nje na sina sheria za kutoka katika hiyo nchi. JE! Ninaweza kumpatia mtu fedha akanihijia?? .

 

 

 



JIBU

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum)  na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Ni matumaini yetu kuwa kila mmoja wetu yu katika siha nzuri, uzima na Imani thabiti. Shukrani kwa kaka yetu ambaye ameuliza swali hili ambalo ni zuri.

Kwa hakika hakuna katazo lolote kuhusu jambo hilo bali Uislamu umehimiza ya kwamba ikiwa mtu alikuwa na uwezo wa kutekeleza amali ya Hijjah lakini hakuweza kwa sababu moja au nyengine aweza kumwakilisha mtu kumfanyia na ni vyema zaidi ampate jamaa yake kwani hilo linakuwa ni deni. Lakini ni vizuri zaidi kwa mtu kufanya mwenyewe amali hiyo ndipo anapopata zile faida nzuri nzuri na kuwa katika hali ambayo inakaribisha kwa Muumba wake.

Tukija katika hali ya mtu mwenyewe ni kuwa hali hii ya kutoruhusiwa haitabaki milele na hivyo angojee mpaka hali kuwa shuwari naye kupata fursa hiyo ya kufanya mwenyewe. Lakini ieleweke kuwa mwanadamu anaweza kufariki wakati wowote hivyo kaka huyo aweke wasiya wake tayari na kumpatia mtu ambaye anamuamini na katika wasiya huo aweke wazi kuwa lau atafariki basi kabla ya mali kurithiwa itolewe hela ya kumwezesha mtu kwenda kumfanyia amali ya Hijjah kwani hilo ni deni. Lau fursa itatokea naye yu hai basi atakwenda mwenyewe.

 

Na Allah Anajua zaidi.