Nani Wana wa Israiyl Na Ipi Nchi Yao
SWALI:
A/Alaykum: Ndugu zangu naomba kuuliza habari Kuhusu Wana-israil. Swali langu ni Kua hii Israil ni ya watu gani. Na
Waasalam Alaykum Warahmatul llway wabarakat.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani
Mwanzo tungependa kutoa taarifa fupi kuhusiana na ibara tatu: Wana wa Israili, Mayahudi na Wazeyuni.
Wana wa Israili ni kabila la jamii iliyozalikana na Nabii Ya‘quub (‘Alayhis Salaam) ambaye jina
Mayahudi ni makafiri kati ya Wana wa Israili. Katika hili Anatuelezea Allaah Aliyetukuka: “Walialaaniwa wale waliokufuru miongoni mwa Wana wa Isarili kwa ulimi wa Daawuud na ‘Iysa bin Maryam. Hayo ni kwa sababu waliasi na wakapindukia mipaka” (5: 78).
Pia, “Tukambarikia yeye (Ibraahiym) na Is-haaq. Na katika kizazi chao walitokea watendao wema na wanaodhulumu nafsi zao waziwazi” (37: 113).
Ama Uzeyuni ni chama cha kisiasa kilichoanzishwa na Dkt. Theodore Herzl mwaka wa 1895 chenye uana memba wa Mayahudi pekee. Malengo
Jambo ambalo tunatakiwa tulifahamu ni kuwa wengi miongoni mwa wanaojiita Mayahudi au Wana wa Israili sasa si Waisraili kidamu. Hawa wengi wao ni wale walioingia katika Uyahudi takriban karne kumi na moja iliyopita, lakini kwa maslahi
Philip Ochieng anatupatia jibu
Kweli, kafara ya Hitler ilikuwa ya siku za usoni. Lakini ilicheza dauru muhimu na kuu kwa mataifa ya Kikristo kugeuza ghafula muelekeo wao kwa Mayahudi. Japo kuwa uzio kwa Mayahudi ulibaki mkali, hisia za hatia zilianza kupenya katika dhamiri za Wazungu. Kwa nini tusiutumie Uzeyuni na tuue ndege wawili kwa jiwe moja? Wasaidie Mayahudi kupata nchi mbali na Bara Ulaya mahabubu, na kwa hivyo punguza hatia na ondoa uzio. Wazeyuni walijitoa kutumiwa na wanyanyasaji wao wa awali na kuwa ala ya kuwaibia na kuwatesa watu wengine kabisa – Waarabu. Kwa muda mrefu tumemeza madai ya ulaghai na udanganyifu wa Uzeyuni kuwa Mayahudi wa Ulaya ni Wasemiti – dhuria wa Judah (Yudah).
Matendo ya Israili yanathibitisha hayo. Mayahudi wote ambao si Wazungu (wale wanaohamia Israili kutoka mataifa ya Kiarabu na Afrika kuanzia 1948, kama Wafalasha kutoka Habeshi) ni raia wa daraja la pili. Ni kwa nini Israili inacheza michuano ya kimataifa ya kandanda katika Bara Ulaya na wala sio Bara la
Uhusiano wa Mayahudi kiutendaji ulikatika kabisa Palestina kwa takribani miaka 1,800 (yaani kuanzia 135 BI mpaka karne ya ishirini). Katika kipindi hiki, hawakuwa na nguvu wala uwezo wa kisiasa au kitamaduni au wa uongozi, bali walikatazwa kabisa na mafundisho ya dini
Kuongezea ni kwamba dai lao la mafungamano na uhusiano na Palestina haliwezi kusimama mbele ya hakika kuwa Banu Israili wengi walikataa kumuunga Nabii Musa (‘Alayhis Salaam) katika safari ya kwenda ardhi tukufu. Hivyo hivyo, wengi wao walikataa kurudi Palestina kutoka Babeli baada ya Mfalme Cyrus alipojitolea na kuahidi kuwalinda. Na katika historia yao yote mpaka leo, idadi ya Mayahudi wanaokaa Palestina hawazidi 40% ya Mayahudi duniani hata katika kipindi chao kizuri na bora zaidi.
Sasa tukija katika sehemu waliyoahidiwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) walipokuwa wako Misri utumwani wakati wa Nabii Musa (‘Alayhis Salaam) ni Palestina wala Israili kwani wakati huo kulikuwa hakuna nchi hiyo katika ulimwengu. Hasa katika miaka hiyo eneo
Amesema al-Kalby: Ardhi tukufu ni
Je, hii aya imewapatia Mayahudi wirathi wa moja kwa moja katika ardhi ya Palestina? Je, huu ni wirathi wa majukumu au wa damu? Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) kuhusu Nabii Ibraahiym (‘Alayhis Salaam) amesema: “Na pindi Mola wako alimpomfanyia Nabii Ibraahiym mtihani kwa Amri nyingi, naye akatimiza. Akamwambia: ‘Hakika Mimi nitakufanya kiongozi wa watu’. Ibraahiym akasema: ‘Je, na katika kizazi changu pia?’ Akasema: ‘Ndio lakini ahadi Yangu haitawafikia madhalimu wa nafsi zao” (2: 124).
Kwa hivyo ahadi ya Allaah haiwachanganyi madhalimu. Ni udhalimu gani ulio mkubwa kuliko kukufuru na kueneza uharibifu katika ardhi ambao unashinda ule wa Bani Israili uliofanywa na unaofanywa. Kuna dhulma gani kuliko ya Maisraili kuwafanyia ndugu zetu wa Palestina. Lakini ni Sunnah ya Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) kuwapatia nguvu madhalimu ili wawatie adabu Waumini ili waweze kurudi katika njia sahihi ya Uislamu. hili ni fundisho kwetu na kurudi kwetu katika utukufu na nguvu ni kushikamana kwetu na Qur-aan na Sunnah.
Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala) Anatueleza kuhusu kuhama kwa Nabii Ibraahiym na Lut (‘Alayhimas Salaam):
“Na tulimuokoa yeye (Nabii Ibraahiym) na Luut tukampeleka kwenye ardhi tuliyoibariki kwa ajili ya ulimwengu wote” (21: 71).
Katika msafara wao huu kutoka Ur, Iraq walipitia kusini mwa Uturuki, kaskazini mwa Syria na baadae Nablus kisha Ramallaah baadae al-Quds, kisha Bi-ir Sab-a na kumalizika kwa safari yao huko Misri. Wakati wa kurudi kutoka Misri walipitia
Ni kweli kabisa kuwa Nabii ‘Iysa (‘Alayhis Salaam) alizaliwa, kuishi na kufanya Da‘wah yake katika nchi ya Palestina. Na yeye alitumwa kuwaongoza Wana wa Israili pamoja na kuwaita katika Uislamu ama ibara ya kondoo waliopotea ni ya Biblia na wala sio katika machimbuko ya sharia yetu. Lakini inatakiwa ifahamike kuwa kuwepo kwake katika nchi hiyo haimaanishi kuwa ni ya kwao, Wana wa Israili. Leo wapo watu wengi kutoka Afrika Mashariki waliohamia nchi za ng’ambo (Marekani na Bara Ulaya) kwa sababu moja au nyengine mpaka wakapata uraia wa nchi hizo. Je, watu hawa hudai kuwa nchi hizo ni za kwao? Jambo hili haliingii katika mizani ya mantiki. Tunafahamu kuwa alipozaliwa Nabii ‘Isa (‘Alayhis Salaam) nchi hiyo ya Kanaani ilikuwa inatawaliwa na Kaesari (Dola ya Kirumi) na wana wa Israili hawakuwa ni wenye kuwa na mamlaka aina yoyote. Tufahamu kuwa wakati huo kulikuwa katika nchi hiyo makabila kadhaa yasiyokuwa ya Kiisraili. Sasa ni hoja gani ambayo tutaweza kutoa kuonyesha kuwa ardhi hiyo ilikuwa
Sasa sisi Waislamu tuko chini ya mashambulizi ya vyombo vya habari ambazo zinapotosha uhakika wa mambo. Ni hakika ya kihistoria kuwa Waisraili walitawala kwa kipindi kifupi
Mayahudi waliuliwa kwa kiasi kikubwa pindi Waislamu walipofukuzwa Andalusia (
Ifahamike kuwa dola ya kwanza ya Waisraili katika ardhi ya Kanaani ni ile iliyoanzishwa wakati wa Nabii Yusha bin Nuun (‘Alayhis Salaam) takriban mwaka wa 1210 KI (Kabla ya kuzaliwa Nabii ‘Isa), nayo haikubali kwa muda mrefu kwani alipofariki Waisraili walizozana
Katika mwaka wa 1004 KI, Nabii Daawuud (‘Alayhis Salaam) alifanywa mfalme wa dola hiyo changa iliyoanzishwa na mfalme Twaaluut. Katika miaka yote hiyo Waisraili hawakuweza kuiteka na kuutawala mji wa al-Quds. Mji huo uliingia katika dola hiyo katika uhai wa Nabii Daawuud (‘Alayhis Salaam) mwaka wa 995 KI. Utawala wake na mtoto wake Nabii Sulaymaan (‘Alayhis Salaam) katika thuluthi mbili (2/3) ya ardhi ya Palestina sasa
Baada ya hapo dola hiyo ya Kiislamu iligawanyika na kuwa dola mbili. Utawala wao ulimalizika kabisa katika ardhi hiyo mpaka mwaka 15 Mei 1948 walipotunukiwa nchi hiyo na Muingereza kinyume na mikataba ya kimataifa na haki za wanati (raia) wake.
Jibu hili ni kwa mujibu wa swali lililoulizwa na ndugu yetu. Ikiwa ndugu atataka ziada kuhusu hata Biblia inasema nini kuhusu ardhi hiyo tutaweza kuchambua
Na tawfiki yote inatoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta‘ala).
Na Allaah Anajua zaidi
[1] Jamii/asili ya Kihindi – Kizungu. Tazama TUKI Kamusi ya Kiingereza – Kiswahili, 110.
[2] Kwa sasa Amerika inaisaidia Israeli kwa dola bilioni tano za Kimarekani kila mwaka
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


