Tawassul Kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Inafaa?
SWALI:
Assalam alaikum,
Hadithi ya wasila ni hii, kwa mujibu wa Sheikh Albany ni sahihi,
19 الترغيب في صلاة الحاجة ودعائها
681(1) (صحيح) عن عثمان بن حنيف رضي الله عنه أن أعمى أتى إلى رسول الله صلى الله عليه وسلم فقال يا رسول الله ادع الله أن يكشف لي عن بصري قال أو أدعك قال يا رسول الله إنه قد شق علي ذهاب بصري .قال فانطلق فتوضأ ثم صل ركعتين ثم قل اللهم إني أسألك وأتوجه إليك بنبيي محمد صلى الله عليه وسلم نبي الرحمة يا محمد إني أتوجه إلى ربي بك أن يكشف لي عن بصري اللهم شفعه في وشفعني في نفسي فرجع وقد كشف الله عن بصره رواه الترمذي وقال حديث حسن صحيح غريب. والنسائي واللفظ له وابن ماجه وابن خزيمة في صحيحه والحاكم وقال صحيح على شرط البخاري ومسلم وليس عند الترمذي ثم صل ركعتين إنما قال فأمره أن يتوضأ فيحسن وضوءه ثم يدعو بهذا الدعاء فذكره بنحوه ورواه في الدعوات.
ikiwa hii ni sahihi Je? Kutawasali kwa kusema kama alivyosema huyu mja alokuwa anaulemavu wa macho, kwamba "ewe Allah ninatawasali kwako kwa nabiy Muhammad Swalla llah alaihi wasallama........."
Wabillah taufiq
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kutawasali kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
Mwanzo ni vyema tujue maana ya neno lenyewe kabla ya kuingia katika maelezo mengine. Al-Wasiylah, inatokana na Tawassul nayo ina maana ya anapofanya mwanadamu amali ya kujileta karibu na Allaah Aliyetukuka. Na al-Wasiylah ni matarajio na kutaka, na pia ina maana nyengine yenye mafungamano na asili, nayo ni cheo na daraja.
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mnaposikia mwadhini semeni
Ama ufahamu wa al-Wasiylah katika Qur-aan Tukufu haitoki nje ya hapo. Amesema Aliyetukuka:
"Hao wanaowaomba, wao wenyewe wanatafuta njia ya kwendea kwa Mola wao Mlezi - hata miongoni mwao walio karibu mno – na wanataraji rehema Zake na wanaikhofu adhabu Yake. Hakika adhabu ya Mola wako Mlezi yafaa kutahadhari nayo" (al-Israa' [17]: 57).
Kuhusu Aayah hii, Imaam Ibn Kathiyr amesema yafuatayo katika Tafsiyr yake:
"Na kauli Yake Aliyetukuka: 'Hao wanaowaomba'. Amepokea al-Bukhaariy kutoka kwa Hadiyth ya Sulaymaan bin Mahraan al-A'mash kutoka kwa Ibraahiym kutoka kwa Abu Ma'mar kutoka kwa 'Abdullaah (Radhiya Allaahu 'anhu) katika kauli Yake: 'Hao wanaowaomba, wao wenyewe wanatafuta njia ya kwendea kwa Mola wao Mlezi'. Baadhi ya majini walikuwa wakiabudiwa, kisha wakasilimu'. Kulingana na riwaya nyingine: 'Baadhi ya wanaadamu walikuwa wakiwaabudu baadhi ya majini, baadaye hao majini wakasilimu, lakini wale wanaadamu walishikilia dini
Hakika nasw za kisheria zinazo tilia mkazo wa Tawassul kutoka katika Qur-aan na Sunnah hazitoki katika vipengele vitatu. Navyo ni
1. Kutawasali kwa Allaah Aliyetukuka kwa kutumia jina miongoni mwa majina Yake yaliyo mazuri au sifa miongoni mwa sifa Zake zilizo juu na tukufu. Mfano ni
2. Mwanaadamu kutawasali kwa 'amali zake njema
3. Kutawasali kwa du'aa ya mtu mwema aliye hai. Kwa mfano, Muislamu anapopatwa na tatizo na akaenda kwa mtu anayeitakidi kuwa ni mcha Mngu amuombee kwa Mola wake Mlezi ili Amfariji katika shida zake. Na kuhusu kipengele hichi zipo dalili nyingi. Miongoni mwazo ni yule Bedui aliyemtaka Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) naye yupo juu ya Minbar amuombe Mola wake ili awapatie mvua (al-Bukhaariy na Muslim). Na katika
Na Allaah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
