Skip navigation.
Home kabah

Kachori Za Duara

 

 

 

 

Vipimo

 

Viazi                                                            1kg

         

Ndimu                                                          2

 

Rai                                                               2 vijiko vya chai

 

Unga wa ngano au wa dengu                        2 vikombe vya chai

 

Bizari ya majano                                          1 Kijiko cha chai

 

Chumvi                                                        Kiasi

 

Pilipili ya unga                                               Kiasi upendavyo

 

Mafuta ya kukaangia

 

 

                                     

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

 

  1. Osha viazi vizuri na viweke katika sufuria

 

 

  1. Tia maji ndani ya sufuria iliyokuwa na viazi na hakikisha maji niyakutosha kuweza kuivisha viazi

 

 

  1. viweke jikoni vichemke na kuiva baada ya hapo viweke viazi pembeni vipoe kwanza

 

 

  1. Kisha menya maganda na uviponde ponde hadi vilainike

 

 

  1. Tia chumvi kiasi, ndimu, rai na pilipili  na vichanganye pamoja vizuri.

 

  1.  Kata madonge madonge na yazungushe zungushe katika mikono ili yawe duara

 

 

  1. Chukua unga na tia bizari ya majano, chumvi kiasi na maji kiasi

 

 

  1. Changanya mchanganyiko huo hadi uchanganyike vizuri uwe mzito mzito

 

 

  1. Weka kikaango jikoni na subiri mafuta yapate moto

 

 

  1. Kisha chukua donge moja moja na lichovyee lote katika unga ulio tengeneza hakikisha donge hilo limeenea unga huo sehemu yote

 

 

  1. Kisha tumbukiza katika kikaango na fanya hivyo kwa madonge mengine yaliyo bakia

 

 

  1. Baada ya kumaliza yote tia katika sahani na tayari kwa kuliwa

 

Assalamu alaikum Ahsante

Assalamu alaikum

Ahsante sana kwa upishi na mafunzo mazuri lakini nilikuwa nauliza suali moja kwani sijafamu jio Rai ni kitu gani? naomba kufahamishwa

Ahsante sana