050-Swahiyh Fiqhis-Sunnah - Mlango Wa Twahara: Kutayamamu (2)

 

NI KIPI KINATOSHELEZA KUTAYAMAMU?

 

Kutayamamu kunakuwa ni badala ya Wudhuu na josho la janaba wakati maji yanapokosekana au kuwa vigumu kuyatumia. An-Nawawiy amesema:

“Haya ndiyo madhehebu yetu. Na hivi ndivyo walivyosema Maulamaa wote katika Maswahaba, Taabi’ina na waliokuja baada yao isipokuwa ‘Umar bin Al-Khattwaab, Abdullaah bin Mas’uud([1]) na Ibraahiym An-Nakhi’y ambaye ni Taabi’i. Hawa wamelizuia, yaani wamezuia kutayamamu kwa ajili ya hadathi kubwa”.

 

Ibn As-Swibaagh na wengine wamesema kuwa inasemekana kuwa ‘Umar na Abdullaah waliachana na msimamo wao.

 

Jamaa zetu hawa na Jamhuri wametoa dalili ya kauli Yake Allaah Mtukufu:

((إذا قمتم إلى الصلاة فاغسلوا وجوهكم))

((Mnaposimama kuswali, basi osheni nyuso zenu)).

 

Hadi Neno Lake:

((وَإِن كُنتُمْ جُنُبًا فَاطَّهَّرُوا))

((Na mkiwa na janaba, basi jitwaharisheni)).

 

Kisha Allaah Mtukufu Akasema:

((فلم تجدوا ماء فتيمموا))

((na hamkupata maji, basi tayamamuni)).

Na hili linarejea kwa wote wawili; mwenye hadathi na mwenye janaba.([2])

 

 

Ninasema:

Kuna dalili nyingine juu ya ushari’ah wa kutayamamu kwa ajili ya hadathi kubwa. Ni Neno Lake Allaah Mtukufu:

((أو جاء أحد منكم من الغائط أو لامستم النساء فلم تجدوا ماء فتيمموا صعيدا طيبا)) 

 ((Au mmoja wenu ametoka chooni, au mmewagusa wanawake na msipate maji, basi ukusudieni mchanga safi)).([3])

 

Makusudio ya kugusana hapa ni tendo la kujamii kwa mujibu wa kauli ya mjumuiko wa Maulamaa akiwemo Ibn ‘Abbaas.([4])

 

Kisha kuna Hadiyth Sahihi zilizopokelewa toka kwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) zinazofahamisha kuwa kutayamamu hutosheleza janaba. Kati ya Hadiyth hizo ni:

 

1- Hadiyth tuliokwisha ielezea ya ‘Imraan bin Haswiyn wakati Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipomwambia mwenye janaba:

((عليك بالصعيد فإنه يكفيك))

((Tumia mchanga, kwani unakutosha)).([5])

 

2- Hadiyth ya ‘Ammaar bin Yaasir, amesema: “Nilipata janaba, kisha nilijigaragaza mchangani, nikamjulisha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya hilo, akaniambia:

((إنما كان يكفيك هكذا:

وضرب يديه على الأرض، ومسح وجهه وكفيه)).

((Hakika ilikuwa inakutosha hivi:

Akapiga mikono yake miwili juu ya ardhi, akosha uso wake na viganja vyake viwili)).([6])

 

 

JE, MAITI HUTAYAMAMISHWA MAJI YAKIKOSEKANA?

 

Maiti hutayamamishwa kama aliyehai maji yakikosekana, kwani kuoshwa kwake ni jambo la lazima. Tumekwishaeleza hapo kabla kuwa mchanga hutwaharishiwa kama maji hakuna.([7])

 

 

 

 

([1]) Imekuja katika Sahihi ya Al-Bukhaariy (345) na Muslim (796) kuwa Ibn Mas’uud amekataza kutayamamu kwa ajili ya janaba na kuwa Abu Muusa alimpinga kwa Aayah.

Ninasema: “Huenda Ibn Mas’uud kulipinga hilo, kumetolewa juu ya yale yaliyo sahihi kwake toka kwa At-Twabariy (9606) wakati alipolifasiri Neno Lake Allaah Mtukufu: ((أو لامستم النساء)) akisema kuwa الملامسة ni chini ya kujamii.

([2]) Al-Majmuu (2/240).

([3]) Surat An-Nisaa: 43

([4]) ((Tafsir At-Twabariy)) (9583) kwa sanadi sahihi kutoka kwake.

([5]) Imekubaliwa na wote. Imeelezewa karibuni.

([6]) Hadiyth Sahihi: Imetolewa na Al-Bukaariy (338) na Muslim (798).

([7]) Angalia “Al-Muhalla” (2/158).

 

Share