Kuwa Na Sijda Kipajini

SWALI:

 

Assallam allaikum

 

Je, ni lazima muislamu kua na sijda na kama hauna je ni vibaya nini maana ya kua na sijda.

 


 

 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu Muislamu kuwa na sijdah.

Ukweli ni kuwa si lazima kwa Muislamu kuwa na sijdah. Sijdah ambayo inapatikana katika paji la uso wa Waislamu ni ishara ya kuwa wao wanamsujudia Allaah Aliyetukuka mbali na kuwa wengine ni nukta muhimu ya kupata sijdah. Hata hivyo, kutokuwa nayo haimanishi kuwa basi wewe si mswalihina wala hutoingia Peponi.

 

Allaah Aliyetukuka Anatuelezea:

Muhammad ni Mtume wa Allaah, na wale aliokuwa nao ni wakali kwa makafiri lakini wenye huruma baina yao. Utawaona wanarukuu, wanasujudu wakitafuta fadhila na radhi za Allaah, katika paji za uso zao wana athari ya sijdah” (al-Fath [48]: 29).

 

Kuwa na sijdah tunafahamishwa hapa ni alama na ishara moja kufanana na wafuasi wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Na kufanana huko kutamfanya mtu awe na ucha Mungu, maadili mema na kutekeleza ‘Ibaadah kwa kiasi kikubwa hivyo huwafanya waingie katika rehema ya Allaah Aliyetukuka na hivyo kuingia Peponi.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share