060 - Kutayamamu (12)
MWENYE KUKOSA VITWAHARISHO VIWILI (MAJI NA MCHANGA)
Kauli sahihi zaidi kati ya kauli mbili za Maulamaa kuhusiana na mtu aliyekosa vitwaharisho viwili (maji na mchanga) ni kuwa ataswali katika hali aliyonayo katika wakati wa Swalah na wala hatoirejesha.
Huu ni mwelekeo wa Ash-Shaafi’iy, Ahmad na Ibn Hazm. Ibn Taymiyyah ameukhitari mwelekeo huu([1]).
Hoja
((فاتقوا الله مااستطعتم))
((Basi mcheni Allaah mwezavyo)).([2])
Na
((لا يكلف الله نفسا إلا وسعها))
((Mwenyezi Mungu Haikalifishi nafsi yoyote ila kwa uwezo wake)).([3])
Na kauli yake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
((إذا أمرتكم بأمر فائتوا منه مااستطعتم))
((Nikiwaamuruni jambo, basi lifanyeni kwa uwezo wenu)).([4])
Wamesema: “Huyu amefanya alichoweza katika Swalah, na jambo la kujitwaharisha ambalo hakuliweza, limemwondokea. Na kwa
Ninasema: “Na huenda mwelekeo huu unatiliwa nguvu na Hadiyth ya Mama wa Waumini ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) aliyesema:
“Mtume wa Mwenyezi Mungu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimtuma Asyad bin Al-Khudhayr – na hali mimi nasikia – kukitafuta kidani nilichokipoteza. Ukafika wakati wa Swalah, nao wakaswali bila ya Wudhuu. Kisha wakamjia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakamweleza
Na ushahidi hapa ni kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwakubalia – wakati walipokosa maji – kuswali bila ya Wudhuu na wala hakuwaamuru kurejesha Swalah. Na endapo
Na kwa upande mwengine, Abuu Haniyfah, Asw-haabur Ra-ay, Maalik na Al-Awzaa’iy, wao wanaona kwamba hatoswali mtu mpaka apate maji ya kutawadhia au mchanga wa kutayamamia, hata
- Login or register to post comments
- Email this page
