Fadhila Za Kusuluhisha Waliogombana (Sehemu ya 2)
Tukiendelea na Fadhila za Kusuluhisha ugomvi, na iwapo baada ya kusoma mada hii tutazithamini fadhila hizi, basi kila mmoja wetu atakimbilia kufanya hima ya kupatanisha ndugu zetu wa Kiislamu waliogombana.
Allaah سبحانه وتعالى Amelichukia jambo hili kwani linavunja asili ya undugu wa Kiislamu
((إِنَّمَا الْمُؤْمِنُونَ إِخْوَةٌ فَأَصْلِحُوا بَيْنَ أَخَوَيْكُمْ))
((Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu))
[Al-Hujuraat: 10]
Na kwa jinsi jambo hili lilivyochukiza hadi kwamba Allaah سبحانه وتعالى Anakaataa kupokea amali za watu wanaogombana mpaka wapatane
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال : قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( تُعرض الأعمال في كل أثنين وخميس فيغفر الله لكل أمريء لايشرك بالله شيئاً، إلا إمرءاً بينه وبين أخيه شحناء فيقول : اتركوا هذين حتى يصطلحا))
رواه مسلم
Imetoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه kwamba kasema Mtume صلى الله عليه وآله وسلم ((Amali njema (vitendo vyema) huoneshwa kila Jumatatu na Alkhamiys, kisha Allaah Humghufuria kila mtu asiyemshiriki kitu Allaah, isipokuwa mtu aliyekuwa baina yake na baina ya ndugu yake uhasama, Husema: Waacheni hawa wawili mpaka wapatane)) [Muslim]
Kwa hiyo ni hatari kubwa kwa waliogombana kuwa wanapoteza umri wao bure kutenda mema na hali kumbe havipokelewi vitendo hivyo hadi wapatane.
Njia za kupatanisha Watu
1)
2) Msikilize kila mmoja malalamiko yake.
3) Ukishajua sababu ya ugomvi, watajie hatari ya kuhasimiana
4) Tafuta wakati na sehemu munaasib kwa wote wawili.
5) Ikibidi kusema uongo, unaweza kusema uongo katika jambo hili kwa kutaka kumridhisha mmojawao ili kuleta suluhisho
((لَيْسَ الْكَذابُ الَّذِي يُصْلِحُ بَيْنَ النَّاسِ فَيَنْمِي خيرا أو يقول خيرا)) رواه البخاري ومسلم
((Si muongo yule anayesuluhisha watu kwa kusema uongo, kwani anaarifu mema au anasema mema [kwa lengo la kusuluhisha])) [Al-Bukhaariy na Muslim]
6) Fanya uadilifu, usipendelee hata
((...فَأَصْلِحُوا بَيْنَهُمَا بِالْعَدْلِ وَأَقْسِطُوا إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُقْسِطِينَ))
((…basi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanaohukumu kwa haki))
[Al-Hujuraat: 9]
7) Wakishapatana InshaAllaah omba du'aa Allaah سبحانه وتعالى Awaendeleze masikilizano na mapenzi baina
************
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


