Mwanamke Kuharamishwa Kuvaa Mavazi Ya Kiume

 

 Mwanamke Kuharamishwa Kuvaa Mavazi Ya Kiume

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

assalam aleykum warrahmatullah wabarakatuh Dada etu … wa … amekwenda mahakamani kuipinga hukmu ilotolewa kwa kuvaa suruali na amehakikisha kuwa makafiri wanaotupiga vita wamehudhuria kwenye kesi kuzidi kuitukanisha dini yetu tukufu. Suala langu aloharamisha mwanamke kuvaa nguo za kiume na mume kuvaa nguo za kike ni binadamu au ni Allah?  sasa … aikana sheria ilowekwa na muumba wetu.

 

 

JIBU:

 

  

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Hakika aloharamisha hilo ni Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth zake nyingi, miongoni mwazo ni:

 

1 .Imepokewa kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaah ‘anhu) kuwa amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) amemlaani mwanamme anayevaa kivazi cha kike na mwanamke anayevaa vazi la kiume” [Abu Daawuwd].

 

 

2. Imepokewa kwa Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kuwa amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) amemlaani mwanamme mwenye kujifananisha na mwanake na mwanamke mwenye kujifananisha na mwanamme” [Al-Bukhaariy, Abuu Daawuwd na At-Tirmidhiy].

 

na analokataza Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) huwa nalo limekatazwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa). Hiyo ni kuwa sisi Waislamu tumeamriwa kufuata hukumu za Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Bonyeza kiungo upate faida ziyada:

 

 

Vazi Lipi Lililo Bora Mbele Ya Allaah?

 

 

Tatizo kubwa ni Waislamu leo kutaka kuwaridhisha makafiri na kutaka kuonyesha kuwa Uislamu unamdhulumu mwanamke kwa njia moja au nyingine, ilhali hilosio sawa.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share