Kulipa Deni La Ramadhaan Na Sita Shawwaal
SWALI
As-salaam alaykum Warahmatullah Wabarakatuh
Naomba fatwa kwa masuala yangu yafuatayo:
Suali: 1
Je inawezekeana kwa mwanamke aliyeingia kwenye siku zake (hedhi) katika mwezi wa ramadhani, baada ya ramadhani kumalizika, kufunga ( kulipa ) ramadhani na wakati huo huo(sambamba) kufunga sitatul shawwal? yaani
a)
b)
suali: 2
Je ikiwa mwanamke alijifungua(kazaa) yaani kapata mtoto kabla ya ramadhani na ramadhani ikamkutia bado hajakooga arubaini(siku 40 baada ya kujifungua) na ikawa siku ya edi-el fitri ndio siku yake ya mwisho, na akamua kuwa siku inayofuata aanza kulipa (yaani mwezi pili mfunguo mosi)ramadhani na wakati huo huo anataka afunge sitatul shawwali, na iwapo kama atafunga ramadhani siku 29 au 30, ataikosa sitatul shawwal je anaweza kuanza sitatul shawwal, badae ndio akanza kufunga ramadhani? na je ni lazima akianza kufunga ramadhani azifuatanishe zote siku 29/30 au anaweza kufunga taratibu taratibu?
Natunguliza shukurani kwa majibu, na nitafurahi
AS-SALAAM ALAYKUM
JIBU:
Wa 'Alaykumus salaam WarahmatuLLahi Wabarakaatuh,
Jibu la Swali la kwanza
Haiwezekani kufunga deni na Sita Shawwaal kwa nia moja. Rai iliyosahihi ni kwamba, kufunga Sita Shawwaal kunawezekana tu baada ya kumaliza deni kwanza la Ramadhaan. Hii ni kutokana na Hadiythi ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم
((من صام رمضان ثم أتبعه بست من شوال))
((Atakayefunga Ramadhaan, kisha akafuatia na Sita za Shawwal…)) [Muslim, Abu Daawuud, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Ahmad, ad-Daarimiy].
Kiunganisho cha neno 'kisha' katika Hadiythi hii kinaonyesha kuwa kufunga huko lazima kutimizwe kwa mpango, yaani kwanza kukamilisha funga Ramadhaan pamoja na deni
Kwa hiyo kutia Nia moja katika funga hii ya Sita Shawwaal haiwezekani, bali ikiwa atafunga mtu deni
Kwa maelezo zaidi ya Swala hili soma katika Fataawa iliyokuwepo katika kiungo hiki kifuatacho:
Fataawa Mbali Mbali Kuhusu Kulipa Deni Na Kufunga Sita Shawwaal
Nia haitajwi Kwa Matamshi:
Nia ya kufanya jambo lolote la ibada huwekwa moyoni na huwa haitajwi nia kwa matamshi
Na kutajwa nia kwa matamshi ni jambo la bid'ah (uzushi) kwani nia mahali pake ni moyoni. Haikuthibitika kutoka kwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم wala Maswahaaba wala Maimaamu wakubwa wote kwamba walikuwa wakitaja nia kwa kusema. Kwa hiyo inatosha kuiweka moyoni.
Jibu la Swali la pili
Ikiwa ni hali kama hiyo uliyoitaja basi atakuwa ana 'udhuru wa kumchelewesha kufunga Sita Shawwaal, kwa hiyo hukumu yake ni vile vile kwamba kwanza amalize deni la Ramadhaan mpaka alimalize, na atakapomaliza deni na ukaingia mwezi wa pili yaani Dhul-Qaada basi afunge Swawm za Sita Shawwaal katika mwezi huo na atapata fadhila zake. Lakini atakayeuwacha mwezi wa Shawwaal kupita bila ya kufunga na bila ya 'udhuru wowote, basi hatopata thawabu za Sita Shawwaal ikiwa atazifunga katika mwezi wa Dhul-Qaadah.
Sheikh Ibn 'Uthaymiyn alipoulizwa kuhusu mas-ala haya , alimalizia kujibu kwa kusema : "Ikiwa mfano mwanamke aliyetoka katika uzazi amelipa deni lake lote katika mwezi wa Shawwaal, kisha ukaingia mwezi wa Dhul-Qaadah na yeye anataka kufunga Sita Shawwaal apate fadhila zake, basi afunge Sita Shawwaal katika mwezi huo wa Dhul-Qaadah ili apate thawabu zake, kwa sababu amezichelewesha (funga za Sita Shawwaal) kutokana na 'udhuru (sababu) muhimu.[Majmu'u ya Fataawa 20/19]
Kuhusu utaratibu wa kufunga, kama tulivyosema hapo juu kwamba ikiwa mtu ana nia ya kufunga na Sita Shawwaal na yeye ana deni la mwezi mzima, basi afunge deni lake katika mwezi wa Shawwaal bila ya kuziwacha siku kupita ili aunganishe na Sita Shawwaal hata kama umeingia mwezi wa pili. Lakini kama mtu hana nia ya kufunga Sita Shawwaal, basi sio lazima kulipa deni
Na Allaah Anajua Zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


