Skip navigation.
Home kabah

Vitimbi Vya Makafiri Kutaka Kuipotoa Qur-aan Tukufu

 

Imeandikwa na: Ummu Iyyaad

 

بسم الله الرحمن الرحيم الحمد لله رب العالمين  والصلاة و السلام على سيدنا محمد وعلى آله وأصحابه أجمعين وبعد

Anasema Allaah سبحانه وتعالى

((مَّا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُواْ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَلاَ الْمُشْرِكِينَ أَن يُنَزَّلَ عَلَيْكُم مِّنْ خَيْرٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَاللّهُ يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَن يَشَاء وَاللّهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ))

((Waliokufuru miongoni mwa watu wa Kitabu na washirikina hawapendi mteremshiwe kheri yoyote kutoka kwa Mola wenu Mlezi))  [Al-Baqarah:105]

Kuchukia kwao makafiri  kwa kuletwa Mtume wa mwisho Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم na kitabu cha mwisho Qur'aan Tukufu kunawapelekea kufanya kila juhudi kwa kutumia kila aina ya mbinu ili wawapotoshe Waislamu katika 'Aqiydah (Iymani) yao iliyo sahihi na waingie katika upotofu. Vitimbi vyao hivi karibuni ni kutunga kitabu wanachokifafananisha na Qur'aan, inayoitwa 'Al-Furqaan Al-Haqq' (The True Furqaan) ambayo imesambazwa na kuuzwa maeneo mengi. Inasemekana imetolewa huko Kuwait.

Tunamshukuru Allaah سبحانه وتعالى  kwa kututanabahisha na pia tunawashukuru ndugu zetu wanaojitahidi kusambaza ujumbe ufuatao hapa chini ambao ulikuwa ukisambazwa kila mara kupitia njia za mtandao na barua pepe  ili  kuwatahadharisha ndugu zetu Waislamu kuhusu upotofu kama huu. 

QURAN MPYA YA KIMAREKANI -  HADAA YA KHATARI KWA WAISLAMU!

Quran mpya inasambazwa Kuwait iitwayo "Al-Furqan", imechapishwa kwa lugha ya Kiarabu na Kiingereza.

Imeelezewa (na maulamaa wa haki) kuwa ni aya za shetani na jarida la kila wiki "Al-Furqan Weekly" limefichua kuwa kuna makampuni mawili ya kimarekani (Omega 2001 na Wine Press) yanahusika na kuchapisha pamoja na kusambazwa kwa "Quran" hiyo ambayo wameiita "The True Furqan", ambayo pia wanaiita ni Quran ya karne ya Ishirini na Moja.

"Quran" hiyo ina zaidi ya kurasa 366 za Kiarabu na Kiingereza .... na inasambazwa kwa watoto wetu Kuwait na katika shule/skuli binafsi za Kiingereza!  Kiji-Quran hicho kina jumla ya Sura 77, ikiwemo Suratul Fat-haa, Al-Jannah (Pepo) na Al-Injiyl, na mwanzo wa kila sura kuna mfumo mpya wa Bismillah Rahmani Rahim unaoingiza itikadi ya imani ya kikristo ya utatu!

Ki-Quran hicho kinapinga imani nyingi za Dini yetu Tukufu ya uislamu, katika mojawapo ya aya hizo za uzushi kinafafanua kwamba kitendo cha kuwa na mke zaidi ya moja ni kuzini, talaka haina ruhusa na pia kimetoa utaratibu mpya wa kugawa mirathi ambao hauendani na ule uliotoka kwa Allah  S.W.T  

Kama hayo bado hayajatosha, ki-Quran hicho kinasema kinagaubaga kuwa Jihad ni Haramu na katika kufurutu ada kinamshambulia kimaneno Allah S.W.T; yote hayo yanafanywa ili kuwanyunyizia sumu watoto wetu kwa nia ya kuudhoofisha uislamu, bei ya kitabu kimoja ni dola 103.00 za kimarekani.

Ujumbe huu ni muhimu usafirishwe na ufikishwe kwa kila Muislamu ili kupeana tahadhari za vitimbi  vya hawa maadui wa uislamu.

Kwa ujumbe huu, natumai kila moja wetu atachukua juhudi ya kuusambaza ili kupeana tahadhari na kujilinda na vitimbi vya wanafiki na makafiri.

 Allah S.W.T Atatulipa kwa jitihada zetu za kuufichua huu udhalimu na pia Atatulipa kama tutazembea bila kuchukua hatua zozote za kutangaza vitimbi vya namna hii.

kwa ushahidi kamili kuhusu hicho kitabu, tafadhalini fungua ukurasa huo hapo chini

http://www.amazon.com/exec/obidos/tg/detail/-/1579211755/

 

Qur'aan Tukufu Itahifadhika milele!

Kwa hakika vitimbi hivi vya kutaka kuipotosha Qur'aan Tukufu lisiwe jambo la kututia khofu sana, bali kila Muislamu anayemuamini Allaah سبحانه وتعالى na maneno Yake, awe ana matumaini makubwa ya kuwa maneno Yake Allaah سبحانه وتعالى ni ya kweli kama Alivyotuambia katika Qur'aan Tukufu:

 

((إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ))

((Hakika Sisi ndio Tulioteremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio Tutaoulinda)) [Al-Hijr:9]

Hapa maneno Aliyoyatumia Allaah سبحانه وتعالى ni maneno ya yenye uhakika na ya yakini nayo ni

إِنَّا 

Nuun' hii ni Nuun ya yakini kwamba Hakika Sisi ndio Tulioteremsha Ukumbusho huu

Na vile vile 'Laam' iliyokuweko katika mwanzo wa neno la

لَحَافِظُونَ

Nayo pia ni 'Laam' ya yakini maana kwamba ni Hakika Sisi ndio Tutakaoihifadhi hii Qur'aan.

Na ndio hivyo ilivyo na itakavyokuwa tokea siku aliyopewa utume Mtume Muhammad  صلى الله عليه وآله وسلم kwa kuteremshiwa aya za mwanzo za Qur'aan mpaka siku ya Qiyaamah. Hatatokea mtu atakayeweza kuibadilisha Qur'aan hii Tukufu wala herufi moja, ni uhakikisho na yakini isiyo na shaka kutoka kwa Mwenyewe Mola wa viumbe vyote.  Na pindi atakapotokea mtu kutaka kuipotosha na kutunga yake basi ni muda mchache tu utapita kisha uongo utadhihirika na ukweli utaendelea kudumu kama Anavyosema Allaah سبحانه وتعالى 

 ((وَقُلْ جَاء الْحَقُّ وَزَهَقَ الْبَاطِلُ إِنَّ الْبَاطِلَ كَانَ زَهُوقًا))  

((Na sema: Kweli imefika, na uongo umetoweka. Hakika uongo lazima utoweke!)) [Al-Israa :81]

Ila tu ni jambo la kutusikitisha, kutuchukiza na kututia uchungu mioyoni mwetu kuona vitimbi vyao hivi ambavyo kila siku vinakuja kwa mitindo na sampuli tofauti. Kusambaza habari hii kwa ndugu zetu Waislamu ndivyo tulivyotuamrishwa na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  katika Hadiyth ifuatayo, kwani kufanya hivyo kunathibitisha dalili ya imani katika nyoyo zetu:

عن أَبي سعيدٍ الخُدْريِّ رضي اللَّه عنه قال : سمِعْتُ رسُولَ اللَّه صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم يقُولُ :   ((مَنْ رَأَى مِنْكُم مُنْكراً فَلْيغيِّرْهُ بِيَدهِ ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطعْ فبِلِسَانِهِ ، فَإِنْ لَمْ يَسْتَطِعْ فَبقَلبهِ وَذَلَكَ أَضْعَفُ الإِيمانِ)) رواه مسلم .

Kutoka kwa Abu Sa'iyd Al-Khudhriy رضي الله عنه  ambaye amesema: Nilimsikia Mtume صلى الله عليه وسلم  akisema:

((Yeyote yule atakayeona kitendo kiovu mwache akiondoe (abadilishe) kwa mkono wake, ikiwa hawezi basi kwa ulimi wake (alikemee au kukataza), na ikiwa hawezi basi kwa moyo wake (achukie) na huo (yaani kuona baya na kunyamaza) ni udhaifu wa Imani)) [Imesimuliwa na Muslim]

Tahryif (Upotofu/Uharibifu)  ya Tawraat na Injiyl

Vitimbi vya kutaka kuvipotosha vitabu vya Allaah سبحانه وتعالى havikuanza hivi karibuni, bali vimeanza zamani sana kwa lengo lao Ahlul-Kitaab (Watu waliopewa vitabu nao ni Mayahudi na Manasara) la kubadilisha maneno ya Allaah سبحانه وتعالى , kuyaondoa yale wasiyoyapenda na kuweka yale waliyoyapenda. Allaah سبحانه وتعالى  Ametuelezea njama hizi zao mara nyingi katika Qur'aan kama ifuatavyo:

((فَبِمَا نَقْضِهِم مِّيثَاقَهُمْ لَعنَّاهُمْ وَجَعَلْنَا قُلُوبَهُمْ قَاسِيَةً يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِ وَنَسُواْ حَظًّا مِّمَّا ذُكِّرُواْ بِهِ وَلاَ تَزَالُ تَطَّلِعُ عَلَىَ خَآئِنَةٍ مِّنْهُمْ إِلاَّ قَلِيلاً مِّنْهُمُ)) 

((Basi kwa sababu ya kuvunja agano lao Tuliwalaani, na Tukazifanya nyoyo zao kuwa ngumu. Wanayabadilisha maneno kutoka pahala pake, na wamesahau sehemu ya yale waliyokumbushwa. Na huachi kuvumbua khiana kutokana nao, isipokuwa wachache miongoni mwao)). [Al-Maidah:13]

Maana kwamba,

 Yanatajwa baadhi ya mabaya ya Mayahudi. Moja katika hayo ni kubadilisha maneno ya kitabu chao Alichowateremshia Mwenyeezi Mungu wakatoa wasiyoyataka wakaweka wanayoyapenda.  Na kazi hii pia Manasara waliifanya na wanaifanya mpaka leo.  Hizi Biblia zao wanazozitabiisha wakazitawanya katika pande zetu hizi na kwingineko.  Ukiiitazama Chapa ya safari hii utaiona tofauti kidogo na ya safari ile.  Na kila inayokuja inakhtilafiana  na iliyotangulia, ima:

(a) yametolewa yaliyokuwamo au

(b) yametiwa yasiyokuwamo au

(c) yanasemwa vingine si kama yalivyosemwa mara ya awali.  Na yote haya yanaonyesha dhahiri shahiri  kuwa hiyo ni mipango yao wenyewe  tu ya kutaka kuvutia kwa pupa upande wa dini yao.   Wanayoyaona yatawavutia watu wanayatia wakasema ni ya Mungu, kumbe yao wenyewe.  Na wanayoyaona yatawakimbiza watu wanayatoa upesi upesi, wakiyazikilia mbali. Dini gani hiyo inayogeuka kila usiku uchao na mchana uiingiyo!   [Tafsiyr ya Sh Abdullah  Swaalih Al Farsiy Allaah سبحانه وتعالى   Amrehemu]

Vile Vile Allaah سبحانه وتعالى Anasema,

((أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُواْ نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يَشْتَرُونَ الضَّلاَلَةَ وَيُرِيدُونَ أَن تَضِلُّواْ السَّبِيلَ ))

(( وَاللّهُ أَعْلَمُ بِأَعْدَائِكُمْ وَكَفَى بِاللّهِ وَلِيًّا وَكَفَى بِاللّهِ نَصِيرًا))

 (( مِّنَ الَّذِينَ هَادُواْ يُحَرِّفُونَ الْكَلِمَ عَن مَّوَاضِعِهِ وَيَقُولُونَ سَمِعْنَا وَعَصَيْنَا وَاسْمَعْ غَيْرَ مُسْمَعٍ وَرَاعِنَا لَيًّا بِأَلْسِنَتِهِمْ وَطَعْنًا فِي الدِّينِ وَلَوْ أَنَّهُمْ قَالُواْ سَمِعْنَا وَأَطَعْنَا وَاسْمَعْ وَانظُرْنَا لَكَانَ خَيْرًا لَّهُمْ وَأَقْوَمَ وَلَكِن لَّعَنَهُمُ اللّهُ بِكُفْرِهِمْ فَلاَ يُؤْمِنُونَ إِلاَّ قَلِيلاً))

((Huwaoni wale waliopewa sehemu ya Kitabu wananunua upotovu na wanakutakeni nanyi mpotee njia?))

((Na Mwenyezi Mungu Anawajua vyema maadui zenu. Na Mwenyezi Mungu Anatosha kuwa ni Mlinzi, na Anatosha kuwa ni Mwenye Kukunusuruni))

 ((Miongoni mwa Mayahudi wamo ambao hubadilisha maneno kuyatoa mahala pake, na husema: Tumesikia na tumeasi, na sikia bila ya kusikilizwa. Na husema: "Raai'naa", kwa kuzipotoa ndimi zao ili kuitukana Dini. Na lau kama wangelisema: Tumesikia na tumetii, na usikie na "Undhurna" (Utuangalie), ingelikuwa ni kheri kwao na sawa zaidi. Lakini Mwenyezi Mungu Amewalaani kwa kufuru yao; basi hawaamini ila wachache tu)) [An-Nisaa 44- 46]

Na Allaah سبحانه وتعالى  Hakuwaacha bila ya Kuwaonya na Kuwaandalia adhabu kali kwa kazi yao hiyo wanayoifanya Anawaambia:

((فَوَيْلٌ لِّلَّذِينَ يَكْتُبُونَ الْكِتَابَ بِأَيْدِيهِمْ ثُمَّ يَقُولُونَ هَذَا مِنْ عِندِ اللّهِ لِيَشْتَرُواْ بِهِ ثَمَناً قَلِيلاً فَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا كَتَبَتْ أَيْدِيهِمْ وَوَيْلٌ لَّهُمْ مِّمَّا يَكْسِبُونَ))

((Basi ole wao wanaoandika kitabu kwa mikono yao, kisha wakasema: Hiki kimetoka kwa Mwenyezi Mungu, ili wachumie kwacho pato dogo. Basi ole wao kwa yale iliyoandika mikono yao, na ole wao kwa yale wanayoyachuma))

[Al Baqarah: 79] 

Hicho kitabu chao kinauzwa kwa bei ya $103.00 ni thamani ndogo kabisa kulingana na adhabu kali watakayoipata ya moto matumboni mwao, ghadhabu kubwa kutoka kwa Mola Mtukufu na adhabu kali ya moto akhera.

((إِنَّ الَّذِينَ يَكْتُمُونَ مَا أَنزَلَ اللّهُ مِنَ الْكِتَابِ وَيَشْتَرُونَ بِهِ ثَمَنًا قَلِيلاً أُولَئِكَ مَا يَأْكُلُونَ فِي بُطُونِهِمْ إِلاَّ النَّارَ وَلاَ يُكَلِّمُهُمُ اللّهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلاَ يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ))

((أُولَئِكَ الَّذِينَ اشْتَرَوُاْ الضَّلاَلَةَ بِالْهُدَى وَالْعَذَابَ بِالْمَغْفِرَةِ فَمَآ أَصْبَرَهُمْ عَلَى النَّارِ))

((ذَلِكَ بِأَنَّ اللّهَ نَزَّلَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ وَإِنَّ الَّذِينَ اخْتَلَفُواْ فِي الْكِتَابِ لَفِي شِقَاقٍ بَعِيدٍ))

 ((Hakika wale wafichao aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu katika Kitabu, wakanunua kwacho thamani ndogo, hao hawali matumboni mwao isipo kuwa moto, wala Mwenyezi Mungu Hatawasemeza Siku ya Kiyama, wala hatawatakasa. Nao watapata adhabu chungu))

((Hao ndio walionunua upotofu badala ya uongofu, na adhabu badala ya maghfira. Ama wavumilivu wa Moto watu hawa!))

((Hayo ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameteremsha Kitabu kwa haki. Na wale waliokhitilafiana katika Kitabu wamo katika upinzani ulio mbali na haki))

 [Al-Baqarah: 174-176]

Wamebadilisha maneno ya Allaah    katika vitabu vyao Tawraat na Injiyl juu ya kwamba walichukua ahadi kutoka kwa Mola wao kuwa watawabainishia watu maamrisho yote yaliyokuwemo humo, 

((إِذْ أَخَذَ اللّهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُواْ الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلاَ تَكْتُمُونَهُ فَنَبَذُوهُ وَرَاء ظُهُورِهِمْ وَاشْتَرَوْاْ بِهِ ثَمَناً قَلِيلاً فَبِئْسَ مَا يَشْتَرُونَ))            

 ((Na pale Mwenyezi Mungu Alipofungamana na waliopewa Kitabu kuwa: Lazima mtawabainishia watu, wala hamtokificha, walikitupa nyuma ya migongo yao, na wakanunua kwacho thamani duni. Basi ni kiovu hicho walichonunua)) [Al 'Imraan: 187]

Na Akawaonya ubaya wote huo wanaoufanya na kuwa wasifiche haki,

((وَآمِنُواْ بِمَا أَنزَلْتُ مُصَدِّقاً لِّمَا مَعَكُمْ وَلاَ تَكُونُواْ أَوَّلَ كَافِرٍ بِهِ وَلاَ تَشْتَرُواْ بِآيَاتِي ثَمَناً قَلِيلاً وَإِيَّايَ فَاتَّقُونِ))

  ((وَلاَ تَلْبِسُواْ الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُواْ الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ))

 ((Na aminini Niliyoyateremsha ambayo yanasadikisha mliyonayo, wala msiwe wa kwanza kuyakataa. Wala msiuze Ishara Zangu kwa thamani ndogo. Na Niogopeni Mimi tu))

((Wala msichanganye  kweli na uongo na mkaificha kweli nanyi mnajua))  [Al-Baqarah: 41- 42]

Lakini wapi!  Kuificha haki na kutaka kuipotoa Qur'aan tukufu kunaendelea tu wala hawatachoka kufanya hivyo.

Hakuna Atakayeweza kuleta Qur'aan

Kwa vyovyote hawatoweza kufanikiwa kuipotoa Qur'aan kwani hata makafiri Quraysh wa Makkah walijaribu kutaka kutunga Qur'aan na Allaah سبحانه وتعالى  Aliwaita na Akawataka washindane Naye kutunga Sura moja tu na hawakuweza. Na sura  ndogo kabisa katika Qur'aan ni zenye aya tatu tu, na hata hivyo wameshindwa.

((وَإِن كُنتُمْ فِي رَيْبٍ مِّمَّا نَزَّلْنَا عَلَى عَبْدِنَا فَأْتُواْ بِسُورَةٍ مِّن مِّثْلِهِ وَادْعُواْ شُهَدَاءكُم مِّن دُونِ اللّهِ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِينَ))

 (( فَإِن لَّمْ تَفْعَلُواْ وَلَن تَفْعَلُواْ فَاتَّقُواْ النَّارَ الَّتِي وَقُودُهَا النَّاسُ وَالْحِجَارَةُ أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ))

 ((Na ikiwa mna shaka kwa hayo Tuliyomteremshia mja Wetu basi leteni sura moja ya mfano wake, na muwaite mashahidi wenu badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa mnasema kweli))

 ((Na mkitofanya - na wala hamtofanya kamwe - basi uogopeni moto ambao kuni zake ni watu na mawe walioandaliwa hao wanaokanusha))  

[Al Baqarah:  23-24]

Waliposema makafiri kuwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kaizua Qur'aan kuwa ni maneno aliyofundishwa na mtu, wengine wakisema ni visa vya watu wa kale, mara wakisema ni maneno ya mchawi, maneno ya mshairi, almuradi walimsingizia kwa kila aina, Allaah سبحانه وتعالى  Alishindana nao walete sura kumi zilizokuwa zimezuliwa lakini ziwe kama Qur'aan, nao hawakuweza,

((أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ قُلْ فَأْتُواْ بِعَشْرِ سُوَرٍ مِّثْلِهِ مُفْتَرَيَاتٍ وَادْعُواْ مَنِ اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللّهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ)) 

 ((Au wanasema: Ameizua? Sema: Basi leteni Sura kumi zilizozuliwa mfano wa hii, na waiteni muwawezao badala ya Mwenyezi Mungu, ikiwa mnasema kweli))  [Huud:13]

Bali hata sura moja ya kuizua hawakuweza!

((أَمْ يَقُولُونَ افْتَرَاهُ قُلْ فَأْتُواْ بِسُورَةٍ مِّثْلِهِ وَادْعُواْ مَنِ اسْتَطَعْتُم مِّن دُونِ اللّهِ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ))

((Je! Ndiyo wanasema ameizua? Sema: Hebu leteni sura moja mfano wake na muwaite (kukusaidieni) muwawezao, isipo kuwa Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnasema kweli))    [Yunus: 38]

Kisha Akazidi Allaah سبحانه وتعالى kushindana nao kuwa hata kama wakikusanyika viumbe vyote kuitunga Qur'aan kama hii, juu ya uhodari wao wowote,  basi hakuna atakayeweza! 

((قُل لَّئِنِ اجْتَمَعَتِ الإِنسُ وَالْجِنُّ عَلَى أَن يَأْتُواْ بِمِثْلِ هَذَا الْقُرْآنِ لاَ يَأْتُونَ بِمِثْلِهِ وَلَوْ كَانَ بَعْضُهُمْ لِبَعْضٍ ظَهِيرًا ))

((Sema: Wangelikusanyika watu na majini ili walete mfano wa hii basi hawaleti mfano wake, hata wakisaidiana wao kwa wao))  [Al Israa: 88]

Maneno ya Allaah سبحانه وتعالى ni maneno ya Allaah سبحانه وتعالى  na maneno ya binaadamu ni maneno ya binaadamu tu, itawezekana vipi kuwa  maneno ya Muumba wa mbingu na ardhi na viumbe vyote duniani yawe sawa na maneno ya viumbe Vyake Alivyoviumba? Haiwaingii akilini jambo hili? Subhana Allaah! Hawaoni kwamba maneno yao ni uongo mtupu usioingia akilini?  Hawasomi maneno ya Allaah سبحانه وتعالى katika Qur'aan Tukufu iliyo ya haki? Qur'aan isiyokwenda pojo? Hawaoni kwamba maneno yao wanayoyatunga hayana uzito wa maana wala hayamnufaishi binaadamu kwani sio wao waliyemuumba binaadamu kujua nini khaswa kinachomfaa na nini kisichomfaa? Hawatafakari? Na bila shaka hayo maneno yao yatakuwa yanakhitilafiana kwani hawana uwezo kama uwezo wa Mola Mtukufu Anayesema:

((أَفَلاَ يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ وَلَوْ كَانَ مِنْ عِندِ غَيْرِ اللّهِ لَوَجَدُواْ فِيهِ اخْتِلاَفًا كَثِيرًا))

((Hebu hawaizingatii hii Qur'an? Na lau kuwa imetoka kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu bila ya shaka wangelikuta ndani yake khitilafu nyingi))  [An-Nisaa:82]

SWALI tunawauliza hao waliotunga hicho kitabu   chao 'Al-Furqaan Al Haqq' (The True Furqan): Kawaida ya vitabu vinavyotoka mbinguni huletwa na Mitume, sasa je, Nani Mtume wao hiki kitabu cha 'Al-Furqaan Al Haqq?

Zama za Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  alitokea mtu aliyedai kuwa yeye ni Mtume ambaye aliitwa Musaylamah, akapachikwa jina la 'Muongo' hivyo akajulikana kuwa ni Musaylamah Al-Kadhaab  'Musaylamah Muongo'. 

Kwa vile baadhi ya Sura za Qur'aan zimeitwa majina ya wanyama kama 'Al Baqarah' (ng'ombe), 'An-Naml' (mdudu sisimizi) Al-'Ankabuut' (buibui) 'Al-Fiyl' (tembo)  na yeye akatunga sura ya wanyama kufananisha nazo na  kusema kuwa ni Qur'aan nayo akaleta maneno haya:

يا ضفدع،  يا ضفدعين

Ewe chura  - Enyi vyura wawili

نِقّي ما تنقّين

Lia (kwa mlio wako) kama unavyolia

نصفك في الماء ونصفك في الطين.

Nusu yako uko katika maji  na nusu yako uko katika udongo

الشاة وألوانها

Kondoo na rangi zake

وأعجبها السود وألبانها

na ajabu yake ni weusi na maziwa yake

والشاة السوداء

Na kondoo mweusi

واللبن الأبيض

na maziwa meupe

إنه لعجب محض

Hakika ni maajabu khalisi

وقد حرِّم المذق

Na kuonja kumeharimishiwa

فما لكم لا تمجعون؟!

Sasa mna  nini hamtemi?

Vile vile akazifananisha Surah ya  Al-'Adiyaat ambayo kama kawaida ya Qur'aan baadhi ya sura zinaishia kwa sauti inayofanana sawa mwisho wa aya,

((وَالْعَادِيَاتِ ضَبْحًا))  (( فَالْمُورِيَاتِ قَدْحًا))  ((فَالْمُغِيرَاتِ صُبْحًا))    ((فَأَثَرْنَ بِهِ نَقْعًا))  ((فَوَسَطْنَ بِهِ جَمْعًا))

1. Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua

2. Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini 

3. Wakishambulia wakati wa asubuhi

4. Huku wakitimua vumbi

5. Na wakijitoma kati ya kundi

[Al-'Adiyaat 1 – 5]

Naye akaleta,

والمبذرات زرعا

Na wenye kupanda mbegu   

والحاصدات حصدا

na wenye kuchuma mazao  

والذاريات قمحا

na upepo wenye kupeperusha  ngano

والطاحنات طحنا

na wenye kusaga unga  

والعاجنات عجنا

Na wenye kukanda unga  

والخابزات خبزا

Na wenye kuoka mikate  

والثاردات ثردا

Na wenye kuchambua  thariyd  (mkate unaochanganywa na mchuzi)

واللاقمات لقما

Na wenye kumeza tonge 

Ni dhahiri kuwa ni maneno ya kipuuzi na upumbavu yasiyoleta maana wala taathira yoyote, na Waislamu moja kwa moja walimjua kuwa ni muongo kwani waliamini maneno ya Mola wao kuwa hakuna Mtume baada ya Mtume Muhammad  صلى الله عليه وآله وسلم wala hakuna kitabu baada ya Qur'aan mpaka siku ya Qiyaamah kama Anavyosema Allaah سبحانه وتعالى

((مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَكِن رَّسُولَ اللَّهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ وَكَانَ اللَّهُ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمًا))

)) Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Mwisho wa Manabii, na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa kila kitu)) [Al-Ahzaab: 40]

Sasa je, atasema nini adui wa Mwenyeezi Mungu huyu aliyetunga hicho kitabu na kusema kuwa ni Qur'aan nyingine?  Kuwa yeye ni Mtume mwingine baada ya Muhammad?  

Na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم hakuthubutu kubadilisha lolote katika Qur'aan. Hata aya alizogombeshwa hakuthubutu kuzificha, na lau angelitaka kuficha aya basi angelificha aya hizi katika Suratul-Ahzaab  na 'Abasa.

((وَتُخْفِي فِي نَفْسِكَ مَا اللَّهُ مُبْدِيهِ وَتَخْشَى النَّاسَ وَاللَّهُ أَحَقُّ أَن تَخْشَاهُ))

((Na ukaficha nafsini mwako Aliyotaka Mwenyezi Mungu Kuyafichua, nawe ukawachelea watu, hali Mwenyezi Mungu Ndiye mwenye haki zaidi kumchelea))  [Al Ahzaab:37]

((عَبَسَ وَتَوَلَّى))  (( أَن جَاءهُ الاََعْمَى))    ((وَمَا يُدْرِيكَ لَعَلَّهُ يَزَّكَّى))  (( أَوْ يَذَّكَّرُ فَتَنفَعَهُ الذِّكْرَى))

 (( أَمَّا مَنِ اسْتَغْنَى))  (( فَأَنتَ لَهُ تَصَدَّى))  (( وَمَا عَلَيْكَ أَلاَّ يَزَّكَّى )) (( وَأَمَّا مَن جَاءكَ يَسْعَى )) 

 (( وَهُوَ يَخْشَى))  (( فَأَنتَ عَنْهُ تَلَهَّى))

 1.Alikunja kipaji na akageuka

2. Kwa sababu alimjia kipofu! 

3. Na nini kitakujuulisha pengine yeye atatakasika? 

4. Au atawaidhika, na mawaidha yamfae? 

5. Ama ajionaye hana haja, 

6. Wewe ndio unamshughulikia? 

7. Na si juu yako kama hakutakasika. 

8. Ama anaye kujia kwa juhudi, 

9. Naye anaogopa, 

10. Ndio wewe unampuuza? 

['Abasa:1-10]

Na pia Allaah سبحانه وتعالى Amesema maneno haya yafuatayo kuhakikisha kuwa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم hakuthubutu kubadilisha maneno ya Qur'aan:

((وَلَوْ تَقَوَّلَ عَلَيْنَا بَعْضَ الاََقَاوِيلِ))  (( لأخَذْنَا مِنْهُ بِالْيَمِينِ))  (( ثُمَّ لَقَطَعْنَا مِنْهُ الْوَتِينَ))   

((Na lau kama angelituzulia baadhi ya maneno tu))

((Bila ya shaka Tungelimshika kwa mkono wa kulia))

((Kisha kwa hakika Tungelimkata mshipa mkubwa wa moyo!))

[Al Haaqqah :44-46]

Hapo ingelikuwa ni mauti yake Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kwani kukatwa mshipa wa mkubwa wa moyo ni mauti tu.  Kisha Anasema Allaah سبحانه وتعالى :

(( فَمَا مِنكُم مِّنْ أَحَدٍ عَنْهُ حَاجِزِينَ))

((Na hapana yeyote katika nyinyi ambaye angeliweza kutuzuia))

[Al Haaqqah: 47]

Haikuwa mabingwa wa lugha na mashairi wa Kiarabu ma-Quraysh ambao nao walishangazwa kupita kiasi na maneno haya kama Waliyd Bin Mughiyrah aliposomewa Qur'aan na Mtume صلى الله عليه وآله وسلم aliwiva uso, na kurudi kwa maQuraysh wenzake na kuwaambia kuwa amesikia maneno ya ajabu yasio na mfano kwa kusema,

والله إن له لحلاوة ،   وإن عليه لطلاوة ،    وإن أسفله لمغدق ،      وإن أعلاه لمثمر ،

 وإنه يعلوا ولا يُعلى عليه

Wallahi hakika hiyo (Qur'aan) ina utamu (wa ajabu)

Na hakika ina upya (uhai) wa ajabu.

(Mizizi) chini  yake  imejaa rutuba na juu (matawi) yake yamejaa mazao/matunda.

Nayo inatawala (iko juu daima) wala haitawaliwi (hakuna kilicho juu yake)

Majini  na  Qur'aan

Hata majini nao walivyoisikia Qur'aan walishangazwa na maneno ya ajabu, wacha binaadamu. Tunawauliza hao wanaotunga kitabu chao walichokiita Qur'aan, je?   Kinasikilizwa na kuaminiwa na majini pia? 

((قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا ))

(( يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ وَلَن نُّشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا ))    

((Sema: Imefunuliwa kwangu ya kuwa kundi moja la majini lilisikiliza, na likasema: Hakika sisi tumeisikia Qur'ani ya ajabu!))

((Inaongoza kwenye uwongofu, kwa hivyo tumeiamini, wala hatutamshirikisha yeyote na Mola wetu Mlezi))  [Al-Jinn: 1-2]

((وَإِذْ صَرَفْنَا إِلَيْكَ نَفَرًا مِّنَ الْجِنِّ يَسْتَمِعُونَ الْقُرْآنَ فَلَمَّا حَضَرُوهُ قَالُوا أَنصِتُوا فَلَمَّا قُضِيَ وَلَّوْا إِلَى قَوْمِهِم مُّنذِرِينَ ))

 (( قَالُوا يَا قَوْمَنَا إِنَّا سَمِعْنَا كِتَابًا أُنزِلَ مِن بَعْدِ مُوسَى مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ وَإِلَى طَرِيقٍ مُّسْتَقِيمٍ))

((Na wakati Tulipowaleta kundi la majini kuja kwako kusikiliza Qur'an. Basi walipoihudhuria walisema: Sikilizeni! Na ilipokwisha somwa, walirudi kwa kaumu yao kwenda kuwaonya))

((Wakasema: Enyi kaumu yetu! Sisi tumesikia Kitabu kilichoteremshwa baada ya Musa, kinachosadikisha yaliyokuwa kabla yake, na kinachoongoza kwenye Haki na kwenye Njia Iliyonyooka)) [Al-Ahqaaf: 29-30]

Athari ya Qur'aan  

Wangapi walioingia Uislamu tokea zama za Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kwa kusikia Aya moja tu? Na hadi leo wangapi wanaosilimu kwa kuathirika na Aya za Qur'aan?  Milioni ya watu wanaingia dini hii tukufu kwa kusikia Aya za Kitabu hiki cha ajabu na kutambua ukweli wa maneno ya Mola wao Muumba wa kila kitu.  

Inaposomwa Qur'aan katika Swalah za Jama'ah, wangapi inawaliza nyuma ya Imaam kwa vilio vya kwikwi na vya huzuni? Nao wamo wanaoifahamu maana yake na wasioifahamu Subhana Allaah!  Kwa nini wanaathirika nayo?  Bila shaka ni kutokana na ufasaha wa lugha ya maneno yanayokolea na kuamsha nyoyo za milioni wa viumbe kwa kusikia maneno ya Mola wao.

Hata majabali yameathirika na Qur'aan hii kama Anavyosema Allaah سبحانه وتعالى ,

((لَوْ أَنزَلْنَا هَذَا الْقُرْآنَ عَلَى جَبَلٍ لَّرَأَيْتَهُ خَاشِعًا مُّتَصَدِّعًا مِّنْ خَشْيَةِ اللَّهِ وَتِلْكَ الأَمْثَالُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ))

((Lau kuwa Tumeiteremsha hii Qur'ani juu ya mlima, basi bila ya shaka ungeliuona ukinyenyekea, ukipasuka kwa khofu ya Mwenyezi Mungu. Na hiyo mifano tunawapigia watu ili wafikiri)) [Al-Hashr: 21]

Na hii ni kwa sababu haya sio maneno ya binaadamu, bila shaka kila Alichokiumba Allaah سبحانه وتعالى  kinachoishi na kisichoishi vyote vitakuwa vinamnyenyekea na kumtukuza  Mola Muumba wa kila kitu kama Anvyosema,

((تُسَبِّحُ لَهُ السَّمَاوَاتُ السَّبْعُ وَالأَرْضُ وَمَن فِيهِنَّ وَإِن مِّن شَيْءٍ إِلاَّ يُسَبِّحُ بِحَمْدَهِ وَلَكِن لاَّ تَفْقَهُونَ تَسْبِيحَهُمْ إِنَّهُ كَانَ حَلِيمًا غَفُورًا))

((Zinamtakasa zote mbingu saba na ardhi na vyote viliomo ndani yake. Na hapana kitu ila kinamtakasa kwa sifa Zake. Lakini nyinyi hamfahamu kutakasa kwake. Hakika Yeye ni Mpole na Mwenye maghfira)) [Al-Israa:44]

Kiarabu Lugha Pekee Ya Qur'aan

Na uzuri wake Qur'aan ni kwa ajili ya lugha ya Kiarabu ambayo Ameichagua Allaah سبحانه وتعالى kuwa ndio lugha ya Qur'aan, lugha ambayo ina ufasaha wa hali ya juu kabisa kuliko lugha zote.

بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ

 ((حم )) (( وَالْكِتَابِ الْمُبِينِ))  (( إِنَّا جَعَلْنَاهُ قُرْآنًا عَرَبِيًّا لَّعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ))

1. H'a Mim 

2. Naapa kwa Kitabu kinachobainisha. 

3. Hakika Sisi tumeifanya Qur'ani kwa Kiarabu ili mfahamu.

[Az-Zukhruf:1-3] 

Na Waislamu tunaamini kuwa Qur'aan haiwezi kuwa Qur'aan ila kwa lugha hii iliyoteremshwa mbinguni. Lugha yoyote nyingine ikitumika ni tarjuma tu na sio maneno ya Mola Muumba.    

Qur'aan kitabu cha pekee kinachohifadhiwa nyoyoni!

Kwa vile Allaah سبحانه وتعالى Ameahidi Kukihifadhi kitabu Chake Kitukufu, ndio ikawezekana kuhifadhika Qur'aan mpaka leo bila ya kubadilishwa kwa kupunguza hata herufi moja au  kuzidishwa, na ndio kitabu cha pekee kinachohifadhiwa katika nyoyo za Waislamu, hakuna kitabu chochote kingine kilichohifadhiwa katika nyoyo. Ama Qur'aan milioni ya Waislamu wanahifadhi kitabu hiki kizima katika nyoyo zao. Kwa hiyo hata kama vikitupwa vitabu vyote baharini au vikiunguzwa moto vyote basi vyote vitapotea  isipokuwa Qur'aan iliyoko katika nyoyo za wengi. Na maajabu ni kwamba anayejua lugha ya kiarabu na asiyejua, wadogo na wakubwa  wote Amewawezesha Allaah سبحانه وتعالى   kuiihifadhi hii Qur'aan Tukufu. Anasema Allaah سبحانه وتعالى  

((بَلْ هُوَ آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ فِي صُدُورِ الَّذِينَ أُوتُوا الْعِلْمَ وَمَا يَجْحَدُ بِآيَاتِنَا إِلاَّ الظَّالِمُونَ))

((Bali hii (Qur'ani) ni Ishara zilizowazi katika vifua vya waliopewa ilimu. Na hawazikatai Ishara Zetu isipo kuwa wenye kudhulumu)) [Al-'Ankabuut:49]

Haya, na tuwaone sasa je? Hicho kitabu chao kitaweza kuhifadhiwa nyoyoni?  Tunawajibu kwa maneno ya Allaah سبحانه وتعالى  

(( هَيْهَاتَ هَيْهَاتَ))

((Hayawi! Hayawi…)) [Al-Muuminuun :36]

Tunamuomba Allaah سبحانه وتعالى  Azidi Kuidhihirisha dini ya Kiislamu na Atuhifadhi na shari za makafiri wanaotaka kutuletea upotofu katika dini yetu na Awafedheheshe duniani na akhera.

Allaahumma Tujaaliye miongoni mwa wa wabebao Kitabu Chako, kwa kuihifadhi Qur'aan katika nyoyo zetu, kuisoma na kufuata maamrisho na makatazo Yake.  

Allaahuumma Tunakuomba Utupanulie vifua vyetu kwa Qur'aan, na Unawirishe (Utie nuru) katika nyoyo zetu kwa Qur'aan, Ututilie uzito katika mizani zetu siku ya Qiyaamah kwa Qur'aan. 

Allaahumma Tufundishe tusiyoyajua ya Qur'aan, na Tukumbushe tunayoyasahau, na Turuzuku tuisome nyakati za usiku na mchana, Na Ijaalie Qur'aan iwe hoja yetu na sio juu yetu Ya Arhamar-Raahimiyn.

Wa Allaahu A'aalm

 

 JIPYA KUHUSIANA NA MAUDHUI:

HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA WAISLAMU DHIDI YA KITABU HICHO

1)     Wameweka katika mtandao Ombi la malalamiko Kupinga kitabu hicho.

Ingia katika kiungo kiufatacho ili utume malalamiko yako kuipinga hicho kitabu:

http://www.petitiononline.com/ahu786/petition.html

2)     Serikali ya India imepiga marufuku kuingiza kitabu hiki  kama ilivyoripotiwa "Serikali ya India imepiga marufuku kabisa kuingiza kitabu hiki kutokana na kitambulisho namba 78/2005-CUSTOMS (NT) tarehe 7 Septemba 1005"

Kwa hiyo matokeo ya kitabu hiki ni sawa tu na kitabu cha Salman Rushdie 'Aya za Shaytwaan'.  Na wasomaji kutoka India wamefurahishwa na hatua hii kuwa imewaepusha na vurugu kwa vile hawatoweza kukisoma kitabu hicho India.