Itikadi Ya Mashia Kuhusu Vitabu
Bila shaka wislamu wote wanaamini kuwa Qur-ani ni kitabu cha mbinguni kilicho teremswa kutoka kwa Allah (a.w)kuja kwa nabii wake Muhammad bin Abdillah,(s.a.w).
Lakini nilipatwa na mshangao mkubwa sana baada ya kusoma kwangu na kuvipitia vitabu vyetu vya kishia ambavyo ndivyo vinavyo tegemewa kama marejeo yanayotegemewa , nilikuta majina ya vitabu vingine ambavyo vinazingatiwa kwa itikadi ya kishia kuwa navyo ni vitabu vitukufu ,na wana zuoni wetu wakubwa wa kishia wanadai kwamba vitabu hivyo pia viliteremshwa kwa mtume (s.a.w)ikiwa ni pamoja na Qur-an, na vitabu hivyo alibaki navyo Amiril-muuminina Ally bin Abi talib.
Wala hakuvibainisha kwa watu yeye Ally wala mtume na huu ni uzushi wa mashia wanaomzushia Ally.
Na vitabu vyenyewe ni hivi:
1-ALJAAMIA: (Mkusanyiko wa elimu)
Imepokewa kutoka kwa Abi buswair kutoka kwa Abii Abdallah alisema: mimi na Muhammad , sisi tuna kitabu kinachoitwa Aljaamia, je, ni jambo gani litakalowafahamisha wao ni nini hiyo Aljaamia? Akasema kumuambia mtume nimejitowa muhanga kwa ajili yako , nifahamishe ni nini hiyo Aljaamia? Akasema ni sahifa kitabu chenye urefu dhiraa sabini kwa dhiraa za mtume (s.a.w) na kitabu hiki ni maneno yatokayo mdomoni mwa mtume (s.a.w)na kuandikwa na Ally bin Abitalib kwa mkono wake, ndani ya kitabu hicho kumebainishwa halali na haramu na kila kitu wanacho kihitajia watu katika maisha yao ya kila siku, hata wadudu walio chini ya ardhi. kwa kuthibisha hayo angalia 1- Alkaaf juzuu ya kwanza uku.239.
2- biharul-an-warar juzuu ya 26 uku.22.
na kuna riwaya nyingi
1. AL-KAAF
2. AL-BIHAAR
3. BASWAIRU-ADDARAJAAT
4. WASAAILU-ASHIAT
Hakika sisi tumefupisha habari hizi kwa kuwaleteeni riwaya moja kwa ajili ya kufupisha.
Mimi mpaka leo sifahamu wala sina uhakika iwapo kitabu hiki (AL-JAMEA) kina ukweli wowote ule ama vipi jambo hilo bado limo nje ya fahamu zangu.na sijui kama ni kweli kwamba kitabu hicho kuna kila kitu ambacho wanakihitaji watu mpaka siku ya Qimaya?ikiwa ni kweli basi ni kwa mimi kimefishwa? Na tukanyimwa sisi tusikipate ni hali ya kuwa kitabu hicho kimebainisha kila jambo la halali na haramu pamoja na hukumu zote mpaka siku ya Qiyama,Je huku sikuficha elimu?hali ya kuwa kuficha elimu ni mambo yaliyo katazwa.Je kufanya hivyo sikatika kuficha elimu?jambo ambalo ni kinyume cha dini?!
2. SAHIFA YA AN-NAMUUSI.
Imepokewa kutoka kwa AL-RIDHAA(a.s) katika hadithi inayosimulia alama za imamu.Alisema-na Sahifa itakayo kuwa kwa imamu atakua na majina ya kishia(wafuasi) wao wote mpaka siku ya kiama.Na sahifa hiyo hiyo itakuwa imeandikwa na majina ya maadui zao wote mpaka siku ya kiyama.
Kwa ufafanuzi zaidi angalia:
1. BIHAAR AL AN-WAAR Juzuu-25 Uk.117
2. BIHAAR AL AN-WAAR Juzuu-26 Uk.117
Na utakuta riwaya nyingi zaidi.
Na mimi nikawa najiuliza uliza , ni kitabu cha aina gani hicho ambacho kinaweza kuandikwa majina ya mashia wote mpaka siku ya kiyama!!!!. Na lau tungeweza kuya sajili majina ya washia wa IRAQ peke yake basi ingetulazimu kuhitaji volume mia moja kwa uchache.na ingekuaje kama tungesajili majina ya mashia wa IRAN na BARAHINDI na mashia wa PAKISTAN, SYRIA na LEBANON na DOLA ZA BARA ARABU na nchi nyinginezo?
Na tungalihitaji vitabu vingapi vya kusajili majina ya mashia wetu katika karne zijazo mpaka siku ya kiyama ? na tungalihitaji vitabu vingapi vya kusajili majina ya mahasimu wao kuanzia kudhihiri hiyo sahifa AN-NUUMAS hadi siku ya kiyama. Lau hata kama bahari ingalikuwa ni wino wa kuandikia majina hayo na nyuma yake kukawa kuna bahari nyingine saba,basi wino wa bahari hizo usingeweza kutosha kuandikia majina hayo.
Na hatakama tungeweza kuzikusanya Computer zote za duniani pamoja na akili zote za ELECTRONICS za kisasa vyote hivyo visingeweza kuhifadhi na kudhibiti majina hayo kutokana na wingi wake. Hata wale wajinga wasiokuwa na elimu,Akili zao haziwezi kukubali riwaya hizi(habari hizi)na mfano wake iweje watu wenye elimu na akili timamu wawe wajinga kiasi hiki?!
Hakika ni muhali mno na jambo lisilowezekana kwa maimamu watukufu kusema mfano wa maneno haya ya kipuuzi na uwenda wazimu,kwani jambo hili halikubaliki kiakili na kimantik. Na lau
3. SAHIFA YA AL-UBAITAN
Imepokewa kutoka kwa Amir-al muuminin(a.s) amesema,Ninaapa kwa jina la Allah, hakika mimi ninazo sahifa nyingi ambazo zimetoka kwa Mtume(s.a.w).na kuna ndani ya sahifa hizo,sahifa inayoitwa(AL-UBAITAN) na sahifa hiyo ina habari mbaya sana zinazo husu waarabu. Na mna habari za makabila sitini ya kiarabu ambayo yameangamizwa wala hayana fungu lolote katika dini(yaani ni makafiri) Angalia BIHAAR AL ANWAR- Juzuu 26 Uk.27.
Hakika riwaya hizi hazikubaliki wala haziingii akilini, iwapo idadi yote hii ya makabila itakuwa haina chembe ya dini mbele ya Allah,kwa maana hiyo ni kwamba hakupatikana hata muislamu mmoja ambaye atakuwa ana dini mbele ya Allah. Halafu kuhusisha haya makabila kiaarabu kwa hukumu hii mbaya hapa inapatikana harufu ya ubaguzi wa kitaifa. Na ufafanuzi zaidi utakuja katika mlango unaokuja
4. SAHIFA YA DHUABA AL-SAAIF.
Imepokewa kutoka kwa Abi Buswaira kutoka kwa Abi Abdillah(a.s),anasema kwamba kulikuwa kwa Dhuaba SAIF RASSULI kuna sahifa ndogo ndani ya sahfa hiyo kuna herufi nyingi na kila herufi moja katika herufi hizo hufunguliwa kwa herufi elfu moja.. na amesema Abu Buswaira , alisema Abu Abdillah na hazikutoka katika herufi hizo elfu moja ila herufi mbili tu,na itabaki hivyo hadi siku ya Qiyama. Angalia BIHARU AL- ANWAR Juzuu .26
Mimi ni kasema na kujiuliza, na hizo herufi nyingine zilizobaki ziko wapi? Na kwa nini zisitolewe iliwafaidi mashia wa Ahlul bait?,kwa herufi hizo? Au zitabaki kuendelea kufichwa mpaka hapo atakapo simama AL QAIMU(mahd).
5.SAHIFA YA ALIA NAYO NI SAHIFA NYINGINE ILIYOPATIKANA KWA DHUABA
AL-SEIFU.
Imepokewa kutoka kwa Abi Abdallah alisema ilipatikana kwa Dhuaba Saifu Rasul,sahifa ambayo imeandikwa ndani yake,BISMILLAHI RAHMAN RAHIM,hakika dhalimu mkubwa mbele ya Allah siku ya kiyama ni yule aliyeuwa asiyemuua, na yule aliyempiga asiye mpiga, na yule aliyetawala asiyestahiki kutawala.basi mtu huyo atakuwa ni kafiri aliye kufuru yale yote aliyoyateremsha Allah kwa Mtume wake Muhammad(s.a.w). na mwenye kuzusha uzushi katika dini na yule aliyempa makazi kila mzushi mtu huyo, Allah hatamkubali siku ya kiyama kumkombolea hata fidia yoyote. Angalia BIHARU AL ANWAAR Juzuu.27 Uk:65-104,na Uk: 275.
6. AL-JAFAR: NA AL- JAFAR NI AINA MBILI :-JAFAR NYEUPE NA JAFAR NYEKUNDU.
Imepokewa kutoka kwa Abi Al-alaa alisema nilisikia Aba Abdillah(a.s) akisema hakika mimi ninayo AL-Jafar Nyeupe, na akasema Abi Al-alaa kumuuliza Abi Abdillah,kwani mna nini ndani ya AL Jafar hiyo? Akasema Abi Abdillah: mna zaburi ya nabii Dauud mna Taurat ya nabii Musa na mna injil ya nabii Issa na Suhfu ya nabii Ibrahim na mna upambanuzi kati ya mambo ya halali na haramu,na akaongeza kusema kwamba vilevile ninayo Al Jafar Nyekundu,na akaniuliza na mna nini ndani ya Jafar Nyekundu akasema na kumjibu kwamba ndani yake mna silaha,na silaha hiyo ni mtu mwenye upanga kwa ajili ya kuuwa,na akasema Abdillah Bin Abii Yaafuur kumwambia Abi Abdilah kumwambia kwa kumuombea dua;Allah akuweke katika afya njema. Je haya watakuwa wanayajua Banuu Al Hssan(kizazi cha Al Hassan) akamjibu ee!! Ndio wallahi wanayajua haya kama wanavyoujua usiku kwamba ni usiku na mchana kwamba ni mchana lakini wao wamepatwa na hasadi na kuitafuta dunia kwa kukanusha na kupinga haki, lau kama wangekua wanaitafuta haki kwa haki hilo lingekuwa bora kwao. Angaliaa USUULU AL KAAF Juzuu 1 Uk:24
Nilimuuliza maulana imamu Al Khaui ambaye sasa ni marehemu,kuhusu Al jafar Nyekundu.ni nani atakaye ifungua?na ni damu ya nani itakayomwagwa?.akanijibu na kusema kwamba atakayeifungua ni huyu bwana wa zama(Mwenyezi Mungu amfanyie haraka faraja yake)na watakao mwaga damu hiyo ni Ahlu Sunnati,kwa maana kwamba watakuja kuuliwa Ahlul Sunnat wote kwa pamoja na huyo bwana wa wakati huo,na ataitawanya damu yao na itakuwa nyingi sana na itakuwa inatiririka na kupita mto Dajital na Furat iliyoko IRAQ.
Na vilevile atakuja kulipizia kisasi kwa masanamu wawili wa kikuraish(anakusudia maswahaba wa Mtume ambao ni makhalifa waongofu naye ni Abubakar na Omar pamoja na Aisha Bint Abibakar na Bi Hafsa Bint Omar ambao ni wake zake Mtume,pamoja na Uthman Bin Affan ambaye ni mkwe wake Mtume pamoja na Bani Umaya na Bani Abbas.na hatimaye atakwenda kuyafukua makaburi yao na kuyawacha wazi.
Nikasema hakika kauli ya Imamu Al-Khaui nichafu na inachukiza mno,kwani Ahlul Bait ni watu watukufu na wenye heshima kwani haiwezekani kwao kwenda kufukua makaburi ya maiti waliokufa kwa karne nyingi zilizopita(kwani watapata faida gani kwa hatua kama hiyo?). hakika maimamu (a.s) walikuwa wakiyakabili maovu kwa kumtendea mema,muovu huyo na kumsamehe na kuyapuuza maovu yake.
Kwahiyo haingii akilini kwa maimamu wenye sifa kama hii kuweza kuyafukua makaburi na kuwatoa hao maiti ili waweze kuwaadhibu na kulipizia kisasi na kuwasimamishia hadi(kuwahukumu)kwani maiti hawasimamishiwi hadi(kuhukumiwa hapa duniani)kwani Ahlul Bait wote wanajulikana kwa sifa za usamehevu na kwamba ni watu wazuri wenye roho nzuri,kwani wao walikuwa ni watu wenye tabia njema walikuwa wavumilivu walibarikiwa tabia nzuri na hiyo ni nguzo madhubuti kabisa.
7. MAS-HAFU WA FATMAT
1.imepokelewa kutoka kwa Ally Bin said kutoka kwa Abi Abdilah,alisema: wallah tunao msahafu wa BIFATMAT ambao una sura zote za kitabu cha Allah na msahafu huo ni maneno aliyoyasema Mtume na Ally akayaandika kwa mkono wake. Tazama, BIHAR AL ANWAAR. Juzuu 26 Uk:41.
2. imepokewa kutoka kwa Muhammad ibn Muslim kutoka kwa mmoja kati ya hao maimamu wawili.Bi Ftma aliacha msahafu siyo Qur-ani kama tuliyokuwa nayo,lakini msahafu huo ni maneno ya Mwenyezi Mungu ambayo aliyomteremshia Bi Fatmat khaswa , na mtu akasema maneno haya na Ally akayaandika kwa mkono wake. Tazame: BIHARU AL ANWAAR;Juzuu 26 Uk:42.
3. imepokewa kutoka kwa Ally Bin Abii Hamza kutoka kwa Abii Abdillah(a.s) alisema kwamba,sisi tunao msahafu wa Fatma,ama wallah ndani ya msahafu huo hamna hata herufi moja ya Qur-ani, lakini msahafu huo ni maneno ya Mtume aliyo yatamka kisha akayandika kwa mkono wake.Angalia AL BIHAAR Juzuu 20 Uk:48.
Kisha nikasema na kujiuliza,ikiwa hiki kitabu ni maneno yanayotoka kwa Mtume na akayaandika Ally ni kwa nini basi akifiche kitabu hicho kwa Ummati wake kwani Mwenyezi Mungu akimuamrisha Mtume wake afikishe kila kitu alichoteremshiwa na Allah kwa Ummati wake kwani amesema Mwenyezi Mungu mtukufu katika surat Al-maadil: Aya;67.
Vipi inawezekana kwa Mtume wa Allah kuweza kuwaficha waislamu wote Qur-an hii.na vipi inawezekana kwa Amir Al muuminina na maimamu wote waliokuja baadae kuificha Qur-an hiyo kwa mashia(wafuasi) wao.hilo ni jambo lisilowezekana hata kidogo.
8. TAURAT NA INJIL NA ZABUR.
Imepokewa kutoka kwa Abi Abdillah(a.s) kwamba yeye alikuwa akisoma INJIL na TAURAT na ZABUR kwa lugha ya kiisoiraniah. Tazama AL HUJAJ MINALKAAP, Juzuu 1
9. AL QUR-AN.
Kuthibiti kwa Qur-an kwamba ni kitabu cha Allah kisicho na shaka ndani yake hakuhitaji nasuu(ushahidi).lakini utaona vitabu wa wanavyuoni wetu na kauli za mujitahidina( wanavyuoni wakubwa)wote vinaelezea kwamba Qur-an hii imebadilishwa na sivyo ilivyo. Na hiyo Qur-an ndicho kitabu peke yake kilicho kumbwa na mabadiliko kati ya vitabu vyote vilivyoteremshwa kutoka nbinguni na Allah.
Na hakika hivyo Al-muhadith Annuury Atwabrisiy alitunga kitabu kikubwa sana katika kuthibitisha kwamba Qur-an imebadilishwa na kitabu hicho kinaitwa Faslu Al Khtiab Fii Ithbat Tahriif ktabu Rabu-Al-Arbaadi. Na alikusanya ndani ya kitabu hicho zaidi ya riwaya Alfu moja zinazozungumzia juu ya kubadilisha Qur-an na vilevile akakusanya kauli za mafukaa wote na maulamaa wa kishia katika kubainisha na kuweka wazi juu ya kubadilishwa Qur-an ambayo ipo kwa waislamu.
Kwani wanazouni wote wa kishia na mafukaha wao wote kuanzia waliotangulia mpaka leo hii wanaamini na kusema kwamba hakika ya Qur-an iliyopo hivi sasa kwa waislamu imebadilishwa Haifa kuwa nayo kwani siyo hawaiamini kamwe. Na huu ni uongo wa dhahiri wakishia.
Amesema Syid Hashimu Al Bahraaniy: mimi ninao ushahidi wa kutosha juu ya kauli ya kwamba kubadilishwa kwa Qur-an, na hayo ni baada ya kufuatilia habari hizi kwa undani kabisa,kwa kiasi ambacho inawezekana kutoa hukumu kwamba msimamo huu na itikadi hii ni katika jambo la dharura na yalazima katika madhehebu ya kishia kuamini hivyo. Na hakika hilo ndilo dhumuni kubwa la kunyanganywa ukhalifa Ahl Bait ; zingatia!!. Angalia :MUQADIMAT AL-BURHAN. Mlango wa tano, Uk: 49.
Na amesema Al Sayyid Niimatu Allah Al-Jazaairy,akiwajibu wale wanaosema kwamba Qur-an haikubadilishwa. Hakika kukubali ,na kuamini kwamba Qur-an,upokewaji wake,watu wake , una daraja ya Tawatur(upokeaji uliosahihi).na ni wahyi uliotoka kwa Allah na kwamba Qur-an yote aliteremka nayo Jibril kwa amri ya Allah kutoka mbinguni,basi jambo hili linapelekea kuweza kuzitupilia mbali habari ambazo zina ukweli na uhakika zaidi.pamoja na kwamba wenzetu Ahlul Sunnat wamekubaliana kwa pamoja juu ya kusihi jambo hili na kuliamini moja kwa moja.Angalia AL-ANWAR ANNUUMANIYA . (Juzuu .2- Uk:357.)
Na kwa habiri hizi amesema Abu Jaafar kama ilivyonukuliwa na Jabir,amesema hakuna mtu yoyote ambae aliyedai kwamba Qur-an ilikusanywa mtu muongo kabisa. Nahakuna yoyote aliyekusanya na kuihifadhi hiyo Qur-an
Bila shaka hii ni uthibitisho wa wazi kabisa unaothibitisha kubadilishwa Qur-an ambayo wanyo waislamu hivi sasa. Na Qur-an ya kweli ni ile ambayo iko kwa Ally na maimamu waliomfuatia baada yake yeye mpaka ikamfikia, ikawa huyo(AL QAAIM).
Na kutokana na hali hiyo ndipo aliposema AL-Imam Al- Khaui katika wasia wake kwetu sisi wakati akiwa anakurubia kufa alisema:Shikamaneni na Qur-an hii (ambayo imebadilishwa)mpaka itakapo dhihiri Qur-an ya Fatmah. Na Qur-an ya Fatmah anayoikusudia huyu Imam, ni ule msahafu ambao alioukusanya Ally
Hakika ni jambo la kushangaza na kuchukiza kwamba vitabu vyote hivyo vimeteremka kutoka kwa Allah halafu vitabu hivyo viwe vimemhusu Amirl muumini na maimamu wake baada yake.na vitabu hivyo vikasalia ni vyenye kufichwa kwa umma,na hasa kwa shia wa Ahlul bait isipokua Qur-an ndogo ambayo watu waliweza kuongeza wanachoongeza na kupunguza wanachopunguza. Haya ni kutokana na maneno ya wazuoni wetu wakishia.
Chakushangaza ni kwamba iwapo vitabu hivi vyote ni kweli vimeteremka kutoka kwa Allah na Amirl muuminina kuwa amekusanya na kuhifadhi Qur-an hii,sasa ina maana gani yeye Amirl muuminin kuwafichia ummah. Na hali yakuwa huo umma unahaja sana na Qur-an hiyo ambayo imekusanya taratibu zote za maisha yao ya kila siku na mambo ya ibada zao iliwaweze kumuabudu Allah,kama inavyotakikana?!.
Na wanazuoni (mafuqahaa) wetu wengi wamelielezea jambo hili na kuliletea kwa kila hali kwa ajili ya kuwaogopea upinzani. Na niwajibu wetu sisi kuuliza,Je inawezekana akawa amirul muuminin ambaye pia ni simba wa Banu Hashim kuwa muoga kiasi cha kushindwa kutetea jambo hili? Je anaweza kuficha habari zake na kuunyima ummah kwa ajili ya kuogopa wapinzani wake. La sivyo ninaapa kwa yule aliyeziinua mbingu pasi na nguzo. Haikuwa kwa Ibn AbiTwalib akimuogopa yoyote isipokuwa Allah peke yake. Na pindi tunapouliza atafanya nini Amirl muuminin na maimamu watakao kuja baada yake kwa Zabur na Taurat na Injil mpaka iwafikie watu wote na halafu waisome vitabu vyote hivyo kwa siri.
Na ikiwakuna nasi(hoja) zilizodai kwamba Amirl muuminin ni yeye peke yake aliyehifadhi Qur-an yote, na akavihifadhi vitabu vyote vya mbinguni na sahifu nyinginezo. Sasa kuna haja gani tena kuwa ni Zaburi, Taurat na Injil? Na hasa tunajua ya kwamba vitabu vyote hivyo vimefutwa kwa kuteremka Qur-an?.
Hakika mimi ninaona kwamba kuna mikono ya watu wanaotumbukiza sumu mbaya katika Riwaya hizi,na wakawasingizia maimamu watukufu uongo huu,( na utakuja uthibitisho wa habari hizi katika mlango maalum)
Sisi sote tunajuwa ya kwamba uislamu hauna kitabu isipokuwa kimoja nacho ni Qur-an tukufu. Ama kuwa na mfano wa vitabu vingi jambo hili ni maalumu kwa mayahudi na manasara kama ilivyokuwa wazi kwenye vitabu vyao,ama kauli inayosema kwamba Amirl muuminin amevihifadhi jamii ya vitabu vyote na kwamba vitabu vyote hivyo vinatoka kwa Allah,na kwamba vitabu vyote hivyo vimekusanya mambo yote ya kishia kauli hiyo ni batil,imeingizwa kwetu na baadhi ya mayahudi ambao walijipenyeza kwenye ushia.
- Login or register to post comments
- Email this page


