Kazi Ya Nesi Kumlisha Mgonjwa Asiye Muislamu Nyama Ya Nguruwe

 

SWALI:

Swali langu nime kuwanauliziya kuusu kama mtu anamulisha mtu ambaye asiye jiweza kama mzee ao mgonjwa nyama ya nguruwe na mtu haigusi na mkono wake isipokuwa unatukisha kama kijiko, niharamu?   Na ayo  niliyo yauliza ninalazimika kuyafanya katika programme ya shule niliyo ichanguwa, ambayo niya u nurse, na mimi napenda sana kusomeya iyo kazi, ila tatizo ni hiyo.

 


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kumlisha huyo unayemtazama chakula cha haraam kama nguruwe au chochote japo kwa kutumia kijiko, hilo halifai kabisa. Hata ukisema unabeba tu chupa ya pombe na kumtengea mnywaji, au sahani ya nguruwe, yote hayo ni haraam kishari’ah na unapaswa ujiepushe nayo kabisa.

Itambulikane kwamba Muislamu anapaswa kujiepusha na kila jambo liloharamishwa na kutokushriki nalo kwa hali ya aina yoyote, kwani kufanya hivyo ni kuchuma dhambi sawa  na mwenye kulitenda jambo lenyewe. 

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate manufaa zaidi:

 

 

Nurse Amekataa Kumhudumia Mgonjwa Asiye Muislam Nguruwe, Kashtakiwa, Je, Atii Taratibu Za Kazi Au Afanyeje?

 

Ninafanya Kazi Ya Kuchinja Nguruwe, Je, Halali?

 

Kufanya Kazi Katika Duka Au Sehemu Inayouzwa Nyama Ya Nguruwe

 

 

Kula Pamoja Na Wasio Waislamu Wanaokula Nguruwe Na Vyakula Vinapakuliwa Kwa Pamoja

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share