Mgonjwa Anaambiwa Ana Mashaytwaan Akivaa Pete Hutulia; Je, Avae Pete Au Itakuwa Ushirikina?

 

Mgonjwa Anaambiwa Ana Mashaytwaan Akivaa

Pete Hutulia; Je, Avae Pete Au Itakuwa  Ushirikina?

 

Alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Assalamu Alaykum:

Kwanza natowa shukurani zangu kwa neema nyingi hizi mnazotupatia hapa Allaah Awajalieni kila la kheri In Shaa Allaah.

 

Suali langu ni hili: Kuna mtu ana matatizo mengi tu yaani maradhi haya na haya yanajitokeza anakwenda hospital anafanyiwa uchunguzi na kupewa madawa na kutowa pesa kwa ajili ya matibabu Sasa huyu mtu ana jini sijui ndo shetwani kichwani mwake anakuwa anapanda kichwani na kusema mshaenda kuzitowa pesa zenu basi huyu ni mkaidi hanijali mimi kwani hatuoni sisi tumetajwa hata kwenye quran ananidharau sasa tatizo kuna pete fulani anataka aivae hiyo akiivaa tu maradhi yote yanapowa. Sasa huyu mama hataki kuivaa kwa sababu anaona akiivaa atakuwa anamuabudu yeye huyu shwaitwan. Sasa naomba mtusaidie kwa majibu yenu akiivaa hii pete kama ni kinga kwake itakuwa inafaa? Na hatokuwa yeye mushrik? Ahsanteni Ndugu yenu katika Imani

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Kama mwanamke mwenyewe ambaye ni mgonjwa alivyofahamu ushirikina wa kuivaa hiyo pete ndivyo hivyo. Kwa kufanya hivyo mgonjwa atakuwa amemtii jinni au shaytwaani na Muislamu anafaa amtii Allaah Aliyetukuka tu.

 

Dawa ya mgonjwa huyu ni kusomewa Ruqyah ya Qur-aan na Shaykh mjuzi kwa hilo ambaye pia ni mchaji  wa Allaah. Kwa kufanya hivyo huyo jini kama yuko kweli atatolewa na mgonjwa kutulia.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share