Zichume Sifa Kumi Njema - Sifa Ya Tatu - Wanaume Watiifu Na Wanawake Watiifu
Anasema Allaah سبحانه وتعالى :
((إِنَّ الْمُسْلِمِينَ وَالْمُسْلِمَاتِ وَالْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ وَالْقَانِتِينَ وَالْقَانِتَاتِ))
((Bila shaka Waislamu wanaume na Waislamu wanawake na Waumini wanaume na Waumini wanawake na wanaume wanaotii na wanawake wanaotii …)) [Al-Ahzaab:35]
Baada ya Uislam na Iymaan, kuna daraja la juu lengine la kufikiwa nalo ni kutii.
Maana ya Qunuut (kutii) kwa ujumla katika lugha ya Qur-aan na katika tafsiyr ya Aayah zinazotaja neno
((أَمَّنْ هُوَ قَانِتٌ آنَاء اللَّيْلِ سَاجِدًا وَقَائِمًا يَحْذَرُ الْآخِرَةَ وَيَرْجُو رَحْمَةَ رَبِّهِ))
((Je! Afanyae ibada nyakati za usiku kwa kusujudu na kusimama akitahadhari na Akhera, na akitaraji Rehma za Mola wake Mlezi)) [Az-Zumar:9]
((يَا مَرْيَمُ اقْنُتِي لِرَبِّكِ وَاسْجُدِي وَارْكَعِي مَعَ الرَّاكِعِينَ))
((Ewe Maryam! Mnyenyekee Mola Mlezi wako na usujudu na uiname pamoja na wainamao)) [Al'Imraan:43]
Miongoni mwa wanawake walio bora kabisa
عن أبي موسى الأشعري قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم ((كَمُلَ مِنَ الرِّجَالِ كَثِيرٌ وَلَمْ يَكْمُلْ مِنَ النِّسَاءِ إِلا مَرْيَمُ بِنْتُ عِمْرَانَ وَآسِيَةُ امْرَأَةُ فِرْعَوْنَ")) وقد أخرجه الجماعة إلا أبا داود ولفظ البخاري: ((كَمُلَ مِنَ الرِّجَالِ كَثِيرٌ وَلَمْ يَكْمُلْ مِنَ النِّسَاءِ إِلا آسِيَةُ امْرَأَةُ فِرْعَوْنَ، وَمَرْيَمُ بِنْتُ عِمْرَانَ ، وَإنَّ فَضْلَ عَائِشَةَ عَلَى النِّسَاءِ كَفَضْلِ الثَّرِيدِ عَلَى سَائِرِ الطَّعَامِ)).
Kutoka kwa Abu Musa Al-Ash'ariyy ambaye amesema: Mtume صلى الله عليه وآله وسلم amesema ((Wanaume wamepata ukamilifu, na hawakukamilika wanawake ila Maryam bint 'Imraan na Aasiyah mke wa Fir'awn)) [Imesimuliwa na wote isipokuwa Abu Daawuud na katika usemi wa Al-Bukhaariy,
((Wanaume wengi wamefikia daraja ya ukamilifu lakini hakuna mwanamke aliyefikia daraja hiyo isipokuwa Aasiyah mke wa Fir'awn, na Maryam bint 'Imraan. Na ubora wa 'Aishah (mke wake) kwa wanawake wengine ni
Anasema Allaah سبحانه وتعالى :
((وَمَرْيَمَ ابْنَتَ عِمْرَانَ الَّتِي أَحْصَنَتْ فَرْجَهَا فَنَفَخْنَا فِيهِ مِن رُّوحِنَا وَصَدَّقَتْ بِكَلِمَاتِ رَبِّهَا وَكُتُبِهِ وَكَانَتْ مِنَ الْقَانِتِينَ))
((Na Mariam binti wa 'Imraan, aliyelinda ubikira wake, na Tukampulizia humo kutoka roho Yetu, na akayasadiki maneno ya Mola wake Mlezi na Vitabu Vyake, na alikuwa miongoni mwa watiifu)) [At-Tahriym:12]
Kisa Cha kuzaliwa Maryam na kulelewa kwake:
Hannah bint Faaquudh alikuwa mke wa Bwana 'Imraan. Imesemekena kwamba alikuwa hakujaaliwa kupata watoto na kwamba siku moja aliona ndege akimlisha kinda chake. Alipoona hivyo akatamani
((إِذْ قَالَتِ امْرَأَةُ عِمْرَانَ رَبِّ إِنِّي نَذَرْتُ لَكَ مَا فِي بَطْنِي مُحَرَّرًا فَتَقَبَّلْ مِنِّي إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ))
((Aliposema mke wa 'Imraan: Mola wangu Mlezi! Nimekuwekea nadhiri kilichomo tumboni mwangu kuwa wakfu; basi nikubalie. Hakika Wewe ndiye Mwenye kusikia na Mwenye kujua)) [Al-'Imraan:35]
Maana kwamba Wewe Unasikia Du'aa yangu na Unatambua niya yangu. Hakujua kama atajaaliwa mtoto wa kiume au wa kike. Alipojifungua mtoto wa kike aliona kwamba mwanamke sio
((فَلَمَّا وَضَعَتْهَا قَالَتْ رَبِّ إِنِّي وَضَعْتُهَا أُنثَى وَاللّهُ أَعْلَمُ بِمَا وَضَعَتْ وَلَيْسَ الذَّكَرُ كَالأُنثَى وَإِنِّي سَمَّيْتُهَا مَرْيَمَ وِإِنِّي أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ))
((Basi alipomzaa alisema: Mola wangu Mlezi! Nimemzaa mwanamke - na Allah Anajua
Maryam maana yake ni 'Mtumishi wa Allah'.
Aayah hiyo inathibitisha kuruhusiwa kumpa jina mtoto siku ile ile anayozaliwa (
((وُلِدَ لِي اللَّيْلَةَ وَلَد سَمَّيْتُهُ بِاسْمِ أبِي إبْرَاهِيمَ))
((Usiku huu mtoto (wa kiume) amezaliwa kwangu na nimemwita jina la baba yangu Ibraahiym)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Kama Aayah ilivyomalizikia kwamba Bibi Hannah alimuomba Allaah سبحانه وتعالى Amkinge na shaytwaan. Allaah سبحانه وتعالى Akamtakabalia Du'aa yake na dalili ni Hadiyth ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kutoka kwa Abu Hurayrah رضي الله عنه
((مَا مِن مَوْلُودٍ يُولَدُ إلا مَسَّه الشَّيْطَانُ حِينَ يُولَدُ، فَيَسْتَهِلّ صَارخًا مِنْ مَسِّهِ إيَّاهُ، إلا مَرْيَم َوابْنَهَا)) ثم يقول أبو هريرة: اقرأوا إن شئتم: (( وَإِنِّي أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ))
((Hakuna kizazi chochote kinachozaliwa ila shaytwaan anakigusa kinapozaliwa, na mtoto huanza kulia kwa sababu ya kuguswa huko, isipokuwa Maryam na mtoto wake [yaani 'Iysa عليه السلام]
Abu Hurayrah kisha akasema someni mkipenda: ((Nami namkinga Kwako, yeye na uzao wake, Uwalinde na shaytwaan aliyelaaniwa)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Akapelekwa Maryam tokea utoto wake msikitini na akakulia huko na akamtoa
Waliokuwa na jukumu la kuihudumia Baytul-Maqdis waligombania kumlea Maryam baada ya kufariki baba yake. Walisema kwamba kwa-vile ni mtoto wa Bwana 'Imraan ambaye alikuwa ni Imaam wao basi ni jukumu lao kumlea. Zakariyah عليه السلام naye akadai kumlea Maryam akasema: "Nipeni mimi kwani ndugu wa mama yake ni mke wangu". Wakasema: "Nyoyo zetu hazitopenda umlee wewe kwa sababu ni mtoto wa Imaam wetu". Ikabidi wafanye kura ya kutupa kalamu zao walizokuwa wakiandikia Taurati katika mto wa Jordan. Yule ambaye kalamu yake itaelea katika mto ndiye atakayemlea Maryam. Walipozitupa kalamu zao, zote zilizama isipokuwa ya Zakariyyah عليه السلام ambaye pia naye alikuwa ni bwana wao, Mwanachuoni wao na pia ni Mtume wao.
Allaah سبحانه وتعالى Anampa kisa hiki Mtume صلى الله عليه وآله وسلم katika wahyi (ufunuo) kisha Anawatanabahisha makafiri kwamba hizi ni habari za ghaibu ambazo hakuzijua Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kabla, na kwa maana kwamba haya maelezo ya Qur-aan si maneno ya Mtume
((ذَلِكَ مِنْ أَنبَاء الْغَيْبِ نُوحِيهِ إِلَيكَ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يُلْقُون أَقْلاَمَهُمْ أَيُّهُمْ يَكْفُلُ مَرْيَمَ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يَخْتَصِمُونَ))
((Hizi ni khabari za ghaibu tunazokufunulia; nawe hukuwa nao walipokuwa wakitupa kalamu zao nani wao atamlea Maryam, na hukuwa nao walipokuwa wakishindana)) [Al-'Imraan:44]
Tukirudia kisa alipozaliwa Maryam, Allaah سبحانه وتعالى Alikubali nadhiri ya mama yake Akamjaaliya kuwa na tabia njema na kupata elimu ya dini yake kutoka kwa Nabii Zakariyyah عليه السلام hata akawa mcha Mungu
((فَتَقَبَّلَهَا رَبُّهَا بِقَبُولٍ حَسَنٍ وَأَنبَتَهَا نَبَاتًا حَسَنًا وَكَفَّلَهَا زَكَرِيَّا كُلَّمَا دَخَلَ عَلَيْهَا زَكَرِيَّا الْمِحْرَابَ وَجَدَ عِندَهَا رِزْقاً قَالَ يَا مَرْيَمُ أَنَّى لَكِ هَذَا قَالَتْ هُوَ مِنْ عِندِ اللّهِ إنَّ اللّهَ يَرْزُقُ مَن يَشَاء بِغَيْرِ حِسَاب))
((Tena Mola wake Mlezi akampokea kwa mapokeo mema na akamkuza makuzo mema, na akamfanya Zakariyyah awe mlezi wake. Kila mara Zakariyyah alipoingia chumbani kwake alimkuta na vyakula. Basi alimwambia: Ewe Maryam! Unavipata wapi hivi? Naye akasema: Hivi vinatoka kwa Allah; na Allah Humruzuku Amtakaye bila ya hisabu)) [Al-'Imraan:37]
[Kisa kama kilivyonukuliwa katika tafsiyr ya Ibn Kathiyr]
************
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


