Steki Nyama Kondoo Ya Sosi Tamu/Kali Ya Nanaa, Ukwaju Na Jamu Ya Marmalade (Machungwa)

Steki Nyama Kondoo Ya Sosi Tamu/Kali  Ya Nanaa, Ukwaju Na Jamu Ya Marmalade (Machungwa)

      

 

Vipimo 

Steki ya nyama ya kondoo (Lamb steak) -  3- 4  LB 

Vitunguu vya majani (spring onions) - 5 miche  

Kitunguu saumu (thomu/galic) - 7 chembe 

Pilipili mbichi -  5-6 

*Sosi ya nanaa ya tayari - 2 vijiko vya supu 

Jam ya marmalade (machungwa) - 2 vijiko vya supu  

Ukwaju ulokamuliwa - 1  kikombe cha chai 

Jiyra/cummin/bizari ya pilau - 1 kijiko cha chai  

Chumvi - kiasi  

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika  

  1. Safisha nyama iache ichuje maji weka kando. 
  2. Weka katika mashine ya kusagia, vitunguu vya majani, pilipili mbichi, kitunguu thomu, chumvi na nusu ya ukwaju, kisha saga hadi ilainike . 
  3. Mimina katika kibakuli, kisha changanya na sosi ya nanaa, jam ya marmalade, ukwaju ulobakia na jiyra/cummin/bizari ya pilau ya unga.  
  4. Weka kando sosi kiasi ya ¼ kikombe. Changanya ilobakia katika nyama vizuri, kisha iache ikolee kwa muda wa kiasi masaa 3 nje au zaidi ya masaa katika friji. 
  5. Weka katika treya ya oveni kisha uoke (bake) kwa moto wa 430° - 450°  kwa muda wa saa 1 takriban hadi nyama iwive. (muda na moto inategemea na aina ya nyama).   
  6. Epua kisha  pakaza sosi ilobakia kisha rudisha katika oveni moto wa kuchomea (grill) na iache ichomeke kwa muda wa dakika 2 tu takriban huku unaigeuza. 
  7. Epua ikiwa  tayari kuliwa na mkate au wali. 

Kidokezo:   

Ikiwa hupati sosi ya nanaa ya tayari dukani, unaweza kutumia majani ya nanaa kiasi ya misongo 3 (bunches). Saga pamoja na viungo katika mashine ya kusagia na     uongeze ukwaju kidogo.

 

 

 

  

 

 

Share