Tumkumbuke Allaah Sana Na Tuombe Maghfirah Baada Ya Kutenda Mema Katika Siku Kumi Bora Kabisa Za Allaah
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
((وَاذْكُرُواْ اللّهَ فِي أَيَّامٍ مَّعْدُودَاتٍ))
((Na mtajeni Allah katika zile siku zinazohisabiwa)) [Al-Baqarah:203]
Ibn 'Abbaas (Radhiya Allahu 'anhumaa) kasema: "Siku zinazohisabiwa ni siku za Tashriyq" (11, 12, 13 Dhul-Hijjah) [Al-Qurtubiy: 3.3]
Kwa maana ni siku ya pili, ya tatu na ya nne baada ya siku ya 'Iyd. Hivyo ndivyo Anavyotuamrisha Mola wetu Mtukufu kuwa tumkumbuke baada ya kusherehekea sikukuu yetu ya 'Iydul-Adhwhaa ('Iyd ya kuchinja). Na hivi ndivyo ilivyo desturi ya ibada zetu kuwa zinamalizika kwa kuambatana na mema na sio maasi.
Mahujaji wanapotekeleza ibada
عن عائشة رضي الله عنها_ عن النبي صلى الله عليه وسلم قال :((ما من يوم أكثر من أن يعتق الله فيه عبدأ من النار من يوم عرفة، وإنه ليدنو ثم يباهي بهم الملائكة فيقول: ما أراد هؤلاء؟)) مسلم
عن أبي هريرة رضي الله عنه ((إن الله تعالى يباهي بأهل عرفات ملائكة السماء ، يقول : انظروا إلى عبادي ، أتوني شعثا غبرا من كل فج عميق ، أشهدكم أني قد غفرت لهم)) المصدر: حلية الأولياء خلاصة الدرجة: صحيح الشيخ األباني
Kutoka kwa Mama wa Waumini 'Aishah (Radhiya Allaahu 'anhaa) kwamba Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kasema: ((Hakuna siku ambayo Allaah Huwaacha waja huru zaidi kutokana na moto
Na usimulizi kutoka kwa Abu Huraryah (Radhiya Allaahu 'anhu) ((Allaah Huwafakharisha watu (waliosimama) 'Arafah kwa Malaika wa mbinguni na Husema: Watazameni waja Wangu waliokuja wamejaa nywele, wana mavumbi, wamekuja kutoka kila pande (za dunia) Nakushuhudieni kuwa Nimewaghufuria)) [Hilyat al-Awliyaa – Shaykh Al-Albaaniy kaipa daraja ya swahiyh]
Lakini juu ya kwamba wameghufuriwa, Mola Mtukufu Anawaamrisha Mahujaji wamkumbuke
(( ...فَإِذَا أَفَضْتُم مِّنْ عَرَفَاتٍ فَاذْكُرُواْ اللّهَ عِندَ الْمَشْعَرِ الْحَرَامِ وَاذْكُرُوهُ كَمَا هَدَاكُمْ وَإِن كُنتُم مِّن قَبْلِهِ لَمِنَ الضَّآلِّينَ)) (( ثُمَّ أَفِيضُواْ مِنْ حَيْثُ أَفَاضَ النَّاسُ وَاسْتَغْفِرُواْ اللّهَ إِنَّ اللّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ)) (( فَإِذَا قَضَيْتُم مَّنَاسِكَكُمْ فَاذْكُرُواْ اللّهَ كَذِكْرِكُمْ آبَاءكُمْ أَوْ أَشَدَّ ذِكْرًا ...))
((Na mtakapomiminika kutoka 'Arafaاh mtajeni Allaah penye Mash'aril Haraam. (Muzdalifah) Na mkumbukeni
((Kisha miminikeni kutoka pale wanapomiminika watu, na muombeni Allah msamaha: hakika Allaah ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu))
((Na mkishatimiza ibada zenu basi mtajeni Allaah
Amri hii ya kuomba maghfira na kumkumbuka
((وَالَّذِينَ يُؤْتُونَ مَا آتَوا وَّقُلُوبُهُمْ وَجِلَةٌ أَنَّهُمْ إِلَى رَبِّهِمْ رَاجِعُونَ))
(Na wale ambao wanatoa walichopewa, na hali nyoyo zao zinagopa kwa kuwa watarejea kwa Mola wao Mlezi)) [Al-Muuminuun:60]
Mama wa Waumini 'Aaishah (Radhiya Allaahu 'anhaa), alimuuliza Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ilipoteremshwa Aayah hii: "Ewe Mjume wa Allaah, je, hawa ni wale wale ambao wanaiba, wanazini na kulewa huku wakimkhofu Allaah?" Akajibu Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa ((Sio ewe bint Abubakar, Bintis-Swiddiyq! Hao ni wanaoswali, wanafunga, wanatoa sadaka na huku wanamkhofu Allaah 'Azza wa Jalla (Mola Mtukufu)). [Ahmad]
Tukiangaza katika Siyrah ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), tokea kuanza da'awah yake ya Utume, tabu aliyopata, maudhi mbali mbali ya Makafiri wa Ki-Quraysh, watu wake kumtenga, kufukuzwa na kupigwa mawe na watu wa Twaaif, maafa mbali mbali yaliyomjaza huzuni kubwa, juhudi nzito za kupigana vita na Makafiri, na mengi mengineyo, hadi mwisho wa Fat-hu Makkah (Ufunguzi wa (kuitwaa) Makkah), makundi kwa makundi ya watu waliingia katika dini ya Kiislam. Mafanikio hayo yamechukua muda wa miaka 23 tokea alipopewa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Utume hadi kukaribia kufariki kwake. Tujiulize, je, baada ya kufaulu huko, ni jambo gani Mola wake Alimfunza afanye? Jibu ni uteremsho wa Surah tukufu ifuatayo:
﴿ بِسْمِ اللّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ﴾
((إِذَا جَاء نَصْرُ اللَّهِ وَالْفَتْحُ)) ((وَرَأَيْتَ النَّاسَ يَدْخُلُونَ فِي دِينِ اللَّهِ أَفْوَاجًا)) ((فَسَبِّحْ بِحَمْدِ رَبِّكَ وَاسْتَغْفِرْهُ إِنَّهُ كَانَ تَوَّابًا))
KWA JINA LA ALLAAH MWINGI WA REHMA MWENYE KUREHEMU
((Itakapo kuja nusura ya Allaah na ushindi)) ((Na ukaona watu wanaingia katika Dini ya Allaah kwa makundi)) ((Zitakase sifa za Mola wako Mlezi, na umwombe msamaha; hakika Yeye Ndiye Anayepokea toba)) [An-Naswr: 1-3]
Ni Surah ya mwisho iliyoteremshwa kikamilifu [kauli ya ibn 'Abbaas katika Swahiyh Muslim]
Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) mwenyewe na hata Maswahaba walitambua kuwa hii ni alama ya kukaribia mauti yake.
Mfano mwengine mzuri tunao wa kipenzi cha Allaah na rafiki Yake (Khaliylul-Allah) Nabii 'Ibraahiym (alayhis-salaam) alipomaliza kujenga Ka'abah yeye na mwanawe Ismaa'iyl. Ka'abah hiyo inayozungukwa na mamilioni ya Waislamu kama ni ibada tukufu tokea siku hizo hadi siku ya Qiyaamah. Lakini hawakutegemea kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atawapokelea amali hiyo moja kwa moja, bali kwanza wamemuomba Mola Awatakabalie kisha Awaghufurie:
((وَإِذْ يَرْفَعُ إِبْرَاهِيمُ الْقَوَاعِدَ مِنَ الْبَيْتِ وَإِسْمَاعِيلُ رَبَّنَا تَقَبَّلْ مِنَّا إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ))
(( رَبَّنَا وَاجْعَلْنَا مُسْلِمَيْنِ لَكَ وَمِن ذُرِّيَّتِنَا أُمَّةً مُّسْلِمَةً لَّكَ وَأَرِنَا مَنَاسِكَنَا وَتُبْ عَلَيْنَآ إِنَّكَ أَنتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ))
((Na kumbukeni Ibraahiym na Ismaa'iyl walipoinyanyua misingi ya ile Nyumba wakaomba: Ewe Mola Mlezi wetu! Tutakabalie! Hakika Wewe Ndiye Msikizi Mjuzi)) ((Ewe Mola Mlezi wetu! Tujaalie tuwe ni wenye kusilimu Kwako, na pia miongoni mwa vizazi vyetu wawe Ummah uliosilimu Kwako. Na Utuonyeshe njia za ibada yetu na Utusamehe. Bila shaka Wewe Ndiye Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu)) [Al-Baqarah: 127-128]
Vile vile Kipenzi chetu Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ametufundisha kuwa kila tunapomaliza ibada ya fardhi ya Swalah zetu tano, tuombe maghfira mara tatu kwa kusema:
أَسْـتَغْفِرُ الله
AtastaghfiruLLah
“Naomba msamaha Allah” (mara tatu)
Ikiwa hali ni kama hizo tulizozitaja zote, basi na sisi tutakapomaliza kutenda mema katika siku Kumi Bora Kabisa za Allah, za Dhul-Hijjah, inatupasa tuombe maghfira na tumkumbuke
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atuwezeshe kukamilisha hizi siku kumi kwa kuzidisha juhudi kufanya mema mengi tukiwa na matumaini na pia khofu ya kukubaliwa amali zetu. Aamiyn.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha
