Wamemwozesha Ndugu Yao Bila Radhi Za Wazazi Kwa Sababu Wanachagua Kabila Na Kijana Aliyeposa Ni Mwenye Dini, Wamefanya Makosa?

SWALI:

 

A'ALEYKUM WA RAHAMATULLAH.

 

MTOTO WA KAKA WA MUME WANGU, BAADA YA KUWAPA FURSA  WAZEE WAKE KUMTAFUTIA MKE, MARA 3, ZOTE HAKIFANIKIWA. MTOTO ANA TABIA NZURI NA KUTOKA KWENYE AILA NZURI NA WENYE KUSHIKA DINI YETU SAWA SAWA, BAADA YA KUSUBIRI SANA, KAPATA MCHUMBA AMBAYE PIA NI MWENYE TABIA NZURI NA WAZEE WAZURI NA WENYE KUFATA DINI YETU VIZURI, TATIZO NI KUWA WAZEE WA MTOTO WA KIUME HAWAKUWAFIQ NDOA HII KHUSUSAN UPANDE WA MAMA YAKE, SABABU NI UKABAILA. LAKINI MTOTO WA KIUME NDIYO KESHAMPENDA NA HAKUBALIANI NA WAZEE WAKE. MIMI, MUME WANGU AMBAYE NI AMI YA MTOTO WA KIUME PAMOJA NA WATOTO WETU, TUMEAMUA KUWA PAMOJA NAYE KUMWOZESHA. JE TUMEFANYA MAKOSA KIDINI NA MBELE YA MOLA WETU SUBHAHANAHU WA TAALA? NA IKIWA TUMEKOSEA, TUFANYE, TUSALI AU TUOMBE DUA GANI KWA ALLAH ILI TUWEZE KUSAMEHEWA? AHSANTE SANA NA MOLA AWABARIK KWA UZIMA NA SIHA (AMEN)


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu kumwozesha mtoto wa kiume bila radhi za wazee.

Suala la posa ni suala muhimu sana katika jamii yetu kwa kiasi ambacho wazee wanatoa maneno yaliyo kinyume na maadili ya Kiislamu ya kumtishia au kumtolea mtoto radhi kwa kufanya jambo la sawa.

 

Pili mtoto wa kiume hahitaji idhni ya baba au walii kwake kuoa, na kwa kuwa kuoa ni ‘Ibaadah tena kubwa kwa vijana na wasichana kuolewa. Yeyote mwenye kumsaidia mvulana kuoa ili asiingie katika uzinzi atapata thawabu.

Hakika nyinyi hamjafanya makosa kumsaidia ila tatizo linaweza kuja kwa kijana kupigwa vita na wazazi wake. Hivyo, ikiwa harusi haijafanyika fanyeni juhudi kuwaunganisha baina mtoto na wazazi wake ili kusiwe na bughudha.

Ikiwa nyinyi mumejaribu bila mafanikio jaribuni kutumia Mashaykh na wazee wengine wenye busara na uelewa wa kuweza kuzungumza na wazazi wa mtoto huyo.

 

Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Awalainishe mioyo ya wazazi ili kusiwe na bughudha wala utesi katika familia.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share