Skip navigation.
Home kabah

Je, Maswahaba Walipunguza Qur-aan? Tuhuma Za Mashia (Rafidhah) Zajibiwa

 

Imekusanywa Na Juma Ikusi

 

 

JE SWAHABA WAMEPUNGUZA QUR-AN AU KUZIDISHA?

 

Kila sifa njema zinamstahiki ALLAH mola wa vilivyomo mbinguni na ardhini, na vilivyomo kati ya mbingu na ardhi. Hana msaidizi katika Utawala wake, na wala hana mshirika katika ibada yake, kisha Rehma na amani zimwendee bwana wetu na kiongozi wetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), na swahaba wake na watu wa nyumbani kwake wote lidumu hilo mpaka siku ya mwisho.

 

Ndugu msomaji wa makala haya , tangu zama za nyumba  kumekuwa na maneno yakisemwa kuhusu QUR-AN. Kuwa kuna baadhi ya swahaba wa  Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) wamepunguza baadhi za aya, bali kuna sura pia ambayo imeondoshwa, kwa kuwa ilikuwa ikibainisha maswala ya ukhalifa baada ya kufa kwa  Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam), ama kuna aya ambazo zilibainisha unafiki, ukafiri wao ndio maana swahaba wakaziondosha katika QUR-AN.

 

Haya si madai ya kupanga tu na kuwasingizia watu bila ya sababu, bali ni kauli ambazo zimo katika vitabu vyao vya kutegemewa, japo wao husema vitabu hivyo, ama mapokezi ya riwaya hizo si sahihi, lakini hakuna yoyote katika wataalamu wao aliyethubutu kuyapinga hayo na kuyakosoa kwa IKH-LAS ya dhati, na kama yatakosololewa Bai ni kwa njia ya TAQIYA. Lakini taarikh yanaonyesha kuwa wataalamu wa mwanzo wa hawakulisema hili ila wale waliokuja  katika karne za karibuni, na ni hawa wafuatao.

1.     Ally Bin Ibrahim Al Qummy alifariki mwaka wa 307 H.

2.     Muhammad Bin yakub Alkulayniy aliyefariki mwaka wa 621 H.

3.     Alfaidhy Alkaashaniy aliyefariki mwaka 1091 H.

4.     Ahmad Bin Mansuur Attwabrusiyy aliyefariki mwaka wa 62 H.

5.     Muhammad Baaqir Al Majilisiy aliyefariki mwaka wa 1111 H.

6.     Muhammad Bin Muhamad Ann U’maaniy (Al mufiid) aliyefariki mwaka wa 413 H.

7.     Abul Hasan Al Amiliy aliyefariki mwaka wa 1143 H.

8.     Ni'matu llahi Bin Abdillah Aljazaairiy aliyefariki mwa wa 1112.

9.     Sultan Muhammad Alkhuraasaniy.

10.   Al Hujja Assayyid Adnan Albahrany aliyefariki mwaka wa 1347 H.

Na wengineo sikuwataja hapa zaidi ya kumi kwani ni wengi ila waliotajwa ni wa kutegemewa katika madhehebu yao.

 

Kadhalika kuna ulamaa wao ambao wamesema kuwa mapokezi ya kuthibitisha kuwa Qur-an imebadilishwa ni mapokezi ambayo ni MUTAWAATIR maana ya mutawaatir, mapokezi yaliyopokewa na watu wengi, kutoka kwa watu wengi mfano wao, na inakuwa si rahisi kwao wao kupokea riwaya za uongo) na miongoni waliosema hayo ni:

 

1.     Abul Hasan Al aamily amesema, (JUA KUWA NI HAKI ISIYO NA SHAKA KUTOKANA NA HABARI AMBAZO NI MUTAWAATIR NA ZINGINEZO, KWAMBA HII QUR-AN AMBAYO IKO MIKONONI) MWETU HIVI SASA IMEPATWA NA MABADILIKO BAADA YA MTUME KUFA, NA WAMEONDOSHA WAKUSANAJI (SWAHABA)MANENO NA AYA NYINGI.)

Rejea utangulizi wa kitabu cha tafsir Miraatul an waar wa mishqaatul asraar UK 36.

 

2.     AL Alama alhujja Aassayyid Adnan al bahraaniy amesema; (HABARI AMBAZO SI ZA KUHESABIKA KUHUSU KUBADILISHWA QUR-AN NI NYINGI KIASI ZIMEPETUKA MPAKA WA TAWAATIR) Rejea kitabu Asshumuusu Adduriyya uk 126 chapa ya Bahrain.

 

3.     Sheikh Al Mufid amesema; HAKIKA HABARI ZILIZOPOKELEWA KUTOKA KWA MAIMAMU WA NYUMBA YA MTUME NI NYINGI KUHUSU KUBADILISHWA KWA QUR-AN NA MENGINEYO YALIYOFANYWA NA MADHALIMU KATIKA KUPUNGUZA NA KUONDOSHA AYA). Rejea kitabu Awa ailil maqaalaat uk 91, Hao na wengineo sikuwataja ila itakapobidi. Ni kwa nini wao waitakidi kuwa Qur-an imepunguzwa ama kuzidishwa? Je yoyote anayeamini hivyo hukumu yake ni nini katika madhehebu ya Ahlul Sunna wal jamaa? Je ni kweli madai yao yana uhakika ama ushahidi wa kisheria? Na anayesema kuwa haijapiunguzwa na wala haina kasoro ambayo wao wanaitakidi je wao wanamchukuliaje ama wanamhukumuje?

 

Wao wanaitakidi mabadiliko katika Qur-an kwa sababu zifuatazo:

1.     Hapakutajwa Uimamu katika Qura-an na swala hilo kwao ni nguzo katika nguzo za dini yao kwa kuwa linaambatana na mas ala ya Kiimani kama kumuamini ALLAH na MTUME wake, amesema Muhammad Husein Aali kaashiful ghitwaa -mmoja waa ulamaa wa KISHIA –katika Kitabu Aslu Shhiiat wa Usuuliha uk 58 chaapa ya Beirut.( HAKIKA UIMAMU NI CHEO CHA ALLAH KAMA VILE UNABII, IKIWA ALLAH ANAMCHAGUA AMTAKAYE KATIKA UTUME NA UNABII, NA KUMPA NGUVU YA HILO KATIKA MIUJIZA, AMBAYO NI KAMA USHAHIDI UTOKAO KWA ALLAH, KADHALIKA HUMCHAGUA AMTAKAYE KATIKA UIMAMU NA HUMUAMRISHA MTUME WAKE KWA DALILI YA AYA KUMTEUA IMAM KWA AJILI YA WATU BAADA YAKE.) hivyo kwa itikadi yao kuna maneno yamepunguzwa kwa kuwa swala la uimam halipo.

 

2.     Kupingana kwa Vitabu vya itikadi na Qur-an kuhusu Ubora na Daraja la Maswahaba Qur-an inawataja Swahaba kwa wema na ubora Mwingi, na wao hilo hawalitaki, hivyo ni lazima waikosoe Qur-an iliyotaja Sifa hizo ili malengo yao yaitimie, na sifa hizo zimo katika sura zifuatazo; Attauba aya; 100,Al an Faal aya; 73, Al Hadiid ay; 10, Al A’raf aya; 157, Al fa th aya; 10,18,29 na nyinginezo. Hivyo Allah amewasifu kwa kuwa wamesuhubiana na  Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) muda wote. Amesema ALLAH katika Qur-an: (WALIOTANGULIA MWANZO KATIKA MUHAJIIRINA NA ANSWAAR NA AMBAO WALIOWAFUATA WAO KWA WEMA RADHI ZA ALLAH ZIWE JUU YAO NA WAO WAMERIDHIA KWA ALLAH NA AMEWAANDALIA PEPO ZIPITAZO MITO CHINI YAKE WAKAE HUMO MILELE HUKO NDIO KUFAULI KUKUBWA) Attauba aya; 100.

 

3.     Kuttajwa majina ya maimamu wao na fadhila zao na miujiza yao, na fadhila za Ziara katika makaburi yao katika Qur-an (kuna watu wanafunga safari kwenda Kuffa-Iraq kwa ajili ya ziara ya makaburi). Hilo limewalazimu wao kuitakidi kuwa Swahaba wameondosha maneno hayo katika Qur-an. Tutataja vile ambavyo zimeandikwa sifa na miujiza yao katika vitabu vyao kwa sasa chukua vichwa vya Maelezo:

 

A.     Maimamu ni wenye Elimu kuliko manabii

B.     Wao ni bora kuliko manabii na viumbe wote

C.    Maombi ya manabii yanakubaliwa na ALLAH kwa kupitia kwa maimamu

D.    Maimamu wana uwezo wa kufufua wafu na kuponya wenye vipofu na mbaranga

E.     Maimamu wana elimu ya yaliyokuwa na yatahayokuwa na hakuna kinachofichika kwao.

 

UFAFANUZI

Sisi Ahlu Sunna wa jamaa tunaitakidi kuwa Qur-an kitabu cha Allah kimehifadhika na wala hakijabadilishwa kwa namna yeyote iwayo si kwa kuongezwa wala kupunguzwa, bali kimehifadhika kwa ulinzi wa ALLAH mwenyewe na amesema: {HAKIKA SISI NDIO TUMEISHUSHA QUR-AN NA SISI NDIO TUTAIHIFADHI} Al hijr aya;9, na wala  hakuna katika vitabu vya Ahlul Sunna vyenye kutegemewa kutoa hata RIWAYA MOJA SAHIHI ambayo inatofautiana na Maelezo haya. Hakika wametaja ulamaa wa Ahlu Sunna katika tafsir zao kuhusiana na aya hii kuwa; Qur-an imehifadhika kutokana na mabadiliko ya ziada na upungufu, rejea tafsir ya Imam Alqurtubiy, Imam Ibn Kathiir, Sheikh Shinqitwiy, na wengineo katika mufasiriina wa Ahlul sunna.

 

Na ulamaa wetu wamesema wazi kuwa yoyote atayeitakidi kuwa Qur-an imezidishwa ama kupunguzwa ATAKUWA AMETOKA KATIKA DINI YA UISLAMU. Na itikadi hii kwetu sisi ni jambo la wazo ambalo hakuna haja ya kuleta dalili kwa kuwa Ulamaa wetu hawakupingana juu ya hili.

Amesema Al Qaadhy Iyaadhy (Iyaadh bin Musa) HAKIKA WAMEKUBALIANA ULAMAA KWAMBA QUR-AN ISOMWAYO KATIKA PEMBE ZA DUNIA ILIYAN DIKWA KATIKA MSAHAFU KWA MIKONO YA WAISLAMU KUANZIA SURA YA AY FAATIHA MPAKA SURA YA AN-NAAS, HAKIKA HAYO NI MANENO YA ALLAH NA UFUNUO WAKE ULIOTETEMSHWA KWA MTUME WAKE MUHAMMAD (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) NA YOTE YALIYOMO NDANI YA KITABU HICHO NI HAKI, NA YOYOTE MWENYE KUPUNGUZA HERUFI MOJA KWA MAKUSUDI AU AKABADILISHA KWA KUWEKA HERUFI NYENGINE MAHALI PAKE, AMA AKAZIDISHA HERUFI AMBAYO HAIKUWAPO KATIKA MSAHAFU AMBAO WAISLAMU WAMEKUBALIANA JUU YA USAHIHI WAKE, KWA MAKUSUDI HAYO, HAKIKA YEYE AMEKUFURU).

Rejea kitabu Asshifaa uk 1103.

 

Amesema Sheikh Abdallah bin Ahmad Bin Muhammad bin Quddama (Muwaffaqud diin) ni katika ulamaa wakubwa wa Ahlu Sunna alifariki mwaka wa 620 H; {HAKUNA KHILAFU BAINA YA WAISLAMU KUWA MWENYE KUKANUSHA SEHEMU KATIKA QUR-AN AU SURA AU AYA AU TAMKO AU HERUFI MOJA AMBAYO UMMA UMEKUBALIANA USAHIHI WAKE, ATAKUWA AMEKUFURU).

Rejea kitabu lumghatul ightiqaad uk;19.

 

Kadhalika  amesema Qadhi Abu Ya’laa (Muhammad Bin Al Husain Bin Muhammad) HAKIKA QURAN IMEKUSANYWA MBELE YA SWAHABA WOTE NA HAKUNA ALIYEPINGA WALA KUKANUSHA KATIKA WAO NA WALA HAKUNA YOYOTE ALIYESEMA KUWA KUNA MABADILIKO KATIKA QUR-AN, NA ALU LINGEKUWAPO HILO LAZIMA BAADHI YA SWAHABA WANGELISEMA HILO KUWA KUNA KASORO, KWA KUWA MFANO WA JAMBO KAMA HILI HAIWEZEKANI LIKAFICHWA KA KAWAIDA. NA PIA LAU INGEKUWA IMEBADILISHWA INGEMPASA ALL BIN ABI TALIB KULIBAINISHA HILO NA KUSAHIHISHA KOSA HILO KWA WAISLAMU. IKIWA YEYE ALIKUWA AKIISOMA QUR-AN HIYO NA KUITUMIA. NI DALILI KUWA HAIKUBADILISHWA).

Rejea kitabu almu’tamad fii usuuli ddin uk; 258.

 

Ushahidi wa kubainisha hilo kuwa Qur-an ni SAHIHI uko Mwingi sana katika vitabu vya Tafsir, Uluumul Qur-an, Aqida n.k. na vingine tumevitaja.

 

 

JE SWAHABA WAMEPUNGUZA QUR-AN AU KUZIDISHA?

Ikiwa Swahaba walituhumiwa kwa tendo la kubadili Qur-an, kwa kuwa walifuta  na kuondosha yale ambayo ilikuwa sifa za IMAM ALLY BIN ABI TALIB kuwapo katika Qur-an, Kwanini Ally hakudhihirisha Qur-an ya sawa na ya kweli baada ya kupewa ukhalifa???

Jibu lake tutalipata katika kauli za ulamaa wa KISHIA kama ifuatavyo;

Tafsiri ya majibu hayo:

1.     Amesema Ni’matullah Aljazairiy; Pindi Amiril-muuminiina ALLY alipokalia kiti cha ukhalifa haikuwezekana kwake yeye kuidhihirisha hiyo Qur-an na kuficha  yaliyomo ndani yake kwa kuwa  itambidi kuweka wazi UOVU waliomtangulia(Swahaba).

Rejea kitabu An-waar nu’maniya 2-360

 

2.     Amesema Al Alaama Almuhaqiqu Almirzaa Habibu Alhaashimiy Alkhuiy; (Hakika yeye Ally amani iwe juu yake hakuweza kudhihirisha Qur-an ambayo iko kwake kwa kuwepo TAQIYA ambayo inazuia hilo kwa sababu itamlazimu kuonyesha fedheha ya waliomtangulia… na ili itimie hoja siku ya kiama dhidi ya waliobadilisha Qur-an, na kwa hali hii ili idhihirike UOVU wa kitendo chao hicho mbele ya Umma wote utakaofufuliwa, na swahaba wanastahiki hiyo fedheha kubwa na adhabu iumizayo na kwa kuongezewa mateso kwa kupetuka kwao mipaka ya jambo la UJUMBE na kwa kupunguzwa kwao hilo mpaka wakamnyanganya Ally Ukhalifa.

Rejea Albaraaghatu fiy Sharhi Nahjul balagha juz 2 uk 220 chapa ya Dar al Wafaaiy-Beirut.

 

Ndugu mwislamu hawa ni katika Ulamaa wa kishia wenye kutegemewa katika Madhehebu yao na wanasema hivyo kuhusu swahaba wa   Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Kwa hawa Shia wa kitanzania wanapinga hizi kauli, na muda huo huo bado wanawakumbatia hawa Ulamaa na vitabu vyao pia, bila ya shaka hii ndiyo ile TAQIYA.

 

Tuwaulize tena swali jengine. Iko wapi Qur-an sahihi kwa itikadi ya Shia??

 

Ili jibu lisiwe na upendeleo wala kusingiziwa, na jibu hili pia lijibiwe na Ulamaa wao mwenyewe,

         

Tafsir ya majibu yao:

1.     Amesema Nimatu llah Aljazaariy; Imepokewa katika mapokezi kwamba wao Amani iwe juu yao wamewaamrisha wafuasi wao kuisoma Qur-an hii iliyopo katika swala na sehemu zingine na kuifanyia kazi hukumu zake, mpaka hapo atakapodhihiri mtawala wetu bwana wa nyakati (AL MAHDI) kisha itanyanyuliwa hii Qur-an kutoka mikononi mwa watu kwenda mbinguni na itatolewa Qur-an ambayo ameihariri Amir wa waumini Ally ataisoma bwana wa nyakati na kuifanyia kazi(kuihukumu kwayo).

Rejea kitabu An wam Nu’maaniya juz 2 uk 360.

 

2.     Amesema Muhammad bin Nuuman laqab yake aitwa Almufid (mtoa faida)hakika mapokezi yamesihi kutoka kwa maimamu wetu amani iwe juu yao. Kwamba wao hakika Wanaona kuwa ni bora kuisoma Qur-an hii na wala tusipetuke kwa kusema kuwa imezidishwa wala kupunguzwa mpaka hapo atakapodhihiri MSIMAMIAJI () Imam Mahdi)atawasomea watu yale yaliyoshushwa na ALLAH MTUKUFU na kukusanywa na Amiirul muuminiina (Ally).

Rejea kitabu Almasaailu cha msomaji mwenyewe uk 78-81 pia angalia Araa haulal Qur-an cha Ayatollah Ally Alfaaniy Al Afhaaniy uk 135.

 

3.     Amesema Abul Hasan hakika Quran iliyohifadhika kutokana na yale yaliyotajwa huko nyuma yenye kuafikiana na yale yaliyoteremshwa na Allah, ni ile aliyoikusanya Ally na akaihifadhi mpaka ikamfikia mwanawe Hassan Kadhalika mpaka ikamfikia ALMAHDI amani iwe kwake, na ndio ILE iliyopo kwake hivi sasa.

 Rejea Muqadima wa pili wa tafsir kitabu Mir aatul an-waar wa mishqaatul asraar, uk 36 kilichotungwa na Albah raaniy.

 

 

Kwa mujibu wa Maelezo ya hawa Ulamaa ni kwamba hii Qur-an inasomwa na wao si kwamba ni sahihi kwa itikadi yao bali wanaitumia kwa muda mpaka hapo atakapokuja Imam Mahdi toka pangoni huko alipo. Hivyo swala la kuficha ukweli kwa kupitia njia ya TAQIYA halitoisha kwao kwa kuwa ni ibada kwao.

 

Hivyo kuna kauli za baadhi ya maulamaa wao kuhusiana na la swala la kupunguzwa kwa Qur-an, wakidai kuwa Qur-an iliyopo mikononi mwa waislamu leo ndio ile ile na ni sahihi, Na haya ni madai na maneno tumezoea kuyasikia na hayana ukweli wowote kwa sababu kwa itikadi yao akisema kinyume na ukweli (TAQIYA)anakuwa  katika ibada kubwa.

 

Ndio maana wao kusema Qur-an ni sahihi kama ilivyoteremshwa tangu awali ni taqiya na kusema kuwa Qur-an si sahihi na imepunguzwa ama kuongezwa huo ndio UKWELI ambao hauna   shaka kwao. Angalia  katika kitabu Usuulul Kaafy cha Alhulainy juz 2-uk 222. Amenukuu hadithi itokayo kwa Imam wake isemayo; HANA IMANI YULE AMBAYE HANA TAQIYA. Kwa mujibu hadithi hii YAO ni bora kusema uongo huo ili iman yako iwe kamili, ikiwa hutokuwa ni miongoni mwa  wanaosema huo uongo basi wewe huna imani.

 

Hivyo kuna ziada ya nguzo za imani KWAO WAO zaidi ya zile sita ambazo twazijua sisi Ahlu Sunna waljamaa. Pia katika ukurasa wa 220 kitabu hicho hicho amesema IMEPOKEWA TOKA ABI ABDILLAH AMESEMA: EWE SULEIMAN, HAKIKA NINYI MPO KATIKA DINI AMBAYO MWENYE KUIFICHA ANATUKUZWA NA ALLAH NA MWENYE KUIDHIRIHISHA HUDHALILISHWA NA ALLAH.

 

Kwa itikadi hii ukitaka hii ukitaka ubora na daraja kubwa uwe ni mtu wa kufanya Taqiya saana, la sivyo ukiwa kama sisi Ahlul Suna Waljamaa, utabaki kuwa ni dhalili. Kwa maana nyingine ukiwa Laghai wewe ni bora mbele ya ALLAH. Hakuna maamrisho yeyote toka kwa ALLAH wala Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)  wala hao maimamu 12 kuhusiana na mafundisho haya ya Taqiya bali utakuta Hadithi kama hizi katika kitabu chao SAHIHI wanavyodai wao, kikiwa na riwaya ambazo hazisalimiki na udhaifu hata kidogo.

 

Amesema Alkulainiy katika kitabu chake Alkaafy, Juz 1 uk 384; (HATOMDAI MTU YOYOTE KUWA YEYE AMEIKUSANYA QUR-AN YOTE KAMA ILIVYOTEREMSHWA, ILA ATAKUWA NI MUONGO NA HAKUNA ALIYEKUSANYA NA KUIHIFADHI KAMA ILIVYOTEREMSHWA NA ALLAH ISPOKUWA NI ALLY BIN ABI TALIB.)

 

Kwa maana hiyo pia kama walivyosema  Ulamaa wao Quran hii wanaisoma kwa muda mpaka aje( MAHDI NA QUR-AN)sahihi. Na ile iliyokusanywa na Zaid ma swahaba wengine ni uongo tu, Ingekuwa bora kama wasingeisoma hii mpaka yao ije toka huko Pangoni. Kumbe akifa mtu katika zama hizi naye anasoma  Qur-an ambayo si sahihi au tapataje thawabu?

 

NDUGU MUISLAMU HAKIKA ULAMAA WAO AMBAO WAMEWATUHUMU SWAHABA KUWA WAMEPOTOSHA QUR-AN KAULI ZAO NDIO MAREJEO YAO MAKUBWA KATIKA MADHEHEBU YAO NA KAMA SI VITABU VYAO ASINGEITWA ALKHUIY( katika Ulamaa wa Kishia)KUWA NDIO MAREJEO YA UMMA WA KISHIA”.

 

Ikiwa hizi ndio kauli za viongozi wao kwanini tukizitaja wanasema si sahihi? Kauli hizo zimekosewa? Wakitoa ushahidi wa rejea zao ndio hizo hizo.

 

 

JE SWAHABA WAMEPUNGUZA QUR-AN AU KUZIDISHA?

Ndugu yangu katika DINI; katika hapo nyuma tulibainisha na kuweka wazi baadhi ya majibu ya Ulamaa wa Kishia kuhusiana na Qur-an, na jinsi ambavyo wao wanaitakidi kama viongozi wa kutegemewa katika madhehebu yao.

 

Utakuta baadhi ya Kauli za Ulamaa wao kusema kuwa Qur-an haijapiunguzwa wala kuzidishwa baadhi yake, lisikushangaze hilo kwani ni kawaida yao kusema maneno kinyume na ilivyo haki na kuupachika msimamo huo jina la TAQIYA.

 

Kabla ya kuorodhesha baadhi za Aya ambazo kuwa ima zimepunguzwa ama kuondoshwa kabisa, isome kauli ya Imam Al Kulayniy ya kumsingizia Ja’far Swadiq:

 

Tafsir: Hakika Qur-an ambayo imeshushwa na ufunuo kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)  ni aya elfu saba(7000)na aya ambazo tunazozisoma ni elfu sita na mia mbili na sitini na tatu tu, na zilizobakia zimehifadhiwa kwa Ahlul bait. Rejea kitabu Al Imam Ja’far Swadiq cha Muhammad Abu Zahra uk 323.

 

Na amepokea Al Kulaniy pia toka kwa Hisham Bin Salim toka kwa baba Abdallah, amani iwe kwake amesema; Hakika Qur-an ambayo amekuja nayo Jibril kwa  Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam)  ni Aya elfu kumi na saba. Rejea kitabu Al Kafy cha Al Kulayniy juz 1 uk 110.

 

Kutokana na kauli hizi na zilizopita ni wazi kabisa kuwa Quran kwao si sahihi katika maneno yake basi yamebadilishwa na SWAHABA. Ni vigumu sana kujua ukweli wao kutokana na itikadi yao ya TAQIYA.

 

Ndugu yangu katika dini, hizi ni baadhi za aya miongoni mwa aya zaidi ya mia mbili ambazo SHIA wanadai zimepunguzwa, ukiachia mbali sura ambayo huitwa SURATIL WILAYAT, ambayo pia wanasema imeondoshwa yote na haipo katika Quran ya sasa. Pia zingatia katika aya maandishi yaliyokuzwa ndiyo yanayodaiwa kuondoshwa katika Qur-an. Pia zimetajwa sura zake katika Quran yetu tuisomayo ili iwe rahisi kwa msomaji kurejea.

 

Kuna baadhi za riwaya ambazo zimo katika vitabu vya Ahlu Sunna, zikielekeza baadhi ya hukumu na mas ala ya Qur-an, na wala si kwamba zinathibitisha kuondoshwa ama kupunguzwa Qur-an kama wanavyodai Shia mfano ni kama:

Kuondoshwa hukumu Fulani katika Qur-an ambayo ilikuwapo mwanzo, kwa hekima ya ALLAH juu ya waja wake, na ndio maana amesema ALLAH: (HATUFUTI AYA YOYOTE WALA HATUISAHAU BALI TUNALETA ILIYO BORA KULIKO HIYO AU MFANO WAKE) Al baqarat 106. Na mfano wa Aya umegawika katika sehemu tatu;

 

1.     Kufuta kisomo chake na hukumu yake.

2.     Kufuta hukumu pekee bila ya kisomo chake.

3.     Kufuta kisomo na kubakisha hukumu, kwa Maelezo zaidi, rejea Kitabu Al itqaan Fiy Uluumil Qur-an cha Imam Assuyutwiy, mlango wa Naasikh na Man Suukh.

 

Mmoja wa Ulamaa wa Kishia Al khuiy anawatuhumu Ahlu Sunna kwa kusema; Hakika kauli ya kusema kuna baadhi za aya zimefutwa kisomo chake, hiyo ndiyo kusema kuwa Qur-an imepotoshwa na hayo ndiyo madhehebu ya Ahlu Sunna. Rejea kitabu Albayan cha tafsir ya Quran yao uk; 205. Hapa tunamzindua kila SHIA na SUNNI ambaye amehadaika na kauli za Al Khuiy na wengineo katika ulamaa wao kuwa;

 

Kwamba kufutwa kwa kisomo ambacho mfutaji wake ni ALLAH hili ni jambo ambalo limethibiti katika Qur-an na Hadithi za MTUME, na limethibiti kwa Maulamaa wa Ahlu Sunna, pia kuna baadhi ya wakubwa wa Maulamaa wa kishia wamelikiri hili, japo hatujui ni kukiri KITAQIYA ama KIKWELI na miongoni mwao ni;

 

Ndugu msomaji hao ni baadhi tu ya ulamaa wa kishia ambao wanakubali kuwa ALLAH aweza kuondosha hukumu atakavyo na ni kwa ajili ya maslaha ya waja wake ili awafanyie wepesi katika dini. Mfano katika hilo ni;

Kuondoshwa hukumu ya kusimamia usiku wote ila kidogo, kama ilivyo katika Surat Almuzammil aya ya 2: (EWE ULIYEJIFINIKA NGUO SIMAMA USIKU KATIKA IBADAA ILA KIDOGO) aya hii imefutwa hukumu yake ambayo ilikuwa ni kusimamia usiku wote kwa ajili ya ibada, kwa huruma ya ALLAH  kwa mtume wake wa waumini kwa ujumla akaifuta hukumu na kubakisha kisomo chake, na hapo ALLAH akathibitisha hukumu nyepesi kuliko ya awali na kumliwaza mtume kuwa, ( Kwa hakika mola wako anajua kuwa wewe unasimama (kumuabudu ALLAH)karibu na thuluthi mbili za usiku, na nusu yake na thuluthi yake na baadhi ya watu walio pamoja nawe…) Kwa hiyo Aya ipo tunaisoma japo hukumu yake imefutwa. Rejea Surat Al Muzammil.

 

Hitimisho la ujumbe huu ni kusema kuwa: Shia kuitakidi kuwa Qur-an imepunguzwa ni madai yasiyo na ushahidi wa KISHERIA na hayakubali kiakili, na ushahidi wa hayo tulikwisha utoa awali kupitia kauli ya mwenye Qur-an; (HAKIKA SISI TUMEITEREMSHA QUR-AN NA SISI NDIO TUTAIHIFADHI) kwa hiyo SWAHABA hana jukumu hilo, na pia kuwatuhumu wao kuwa wamefanya khiyana hiyo ni uonevu usio na sababu ila CHUKI. Bali wao ndio waliopata tabu mno kuhusiana na hii Qur-an. Bali inafaa kwa wale wanaowatuhumu Swahaba hawa wasubiri tu Qur-an yao itatoka Pangoni muda wake ukifika. Mwanzo wa makala tulibainisha Kauli za Ulamaa wa Ahlu Sunna Wal Jamaa kuwa; mwenye kuitakidi kuwa Qur-an ina kasoro atakuwa ametoka nje ya MILA (dini) hivyo tunatoa TAHADHARI kuhusiana na itikadi hii ni potofu MNO. La kushangaza ni kuwa wanaotoa tuhuma hizi ndio wanaokumbatiwa pamoja na vitabu vyao, na ukitolea ushahidi kupitia hivyo unaambiwa kuwa hapo wamekosea ama kitabu hicho hakikubaliki kwao.

 

 

Rudi Juu