Kitangulizi Cha Chapa Ya Pili
Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa jinsi kitabu hiki kilivyopokelewa kwa furaha na kukongowewa na kila aliekisoma. Kwa sababu wengi katika ndugu zetu hawakupatabahati ya kukionatumeona ni lazima tukipigishe chapa ya mara ya pili.
Ama watu fulani ambao ndio maamiri na viongozi wa ngoma hii, hao sikutaraji kuwa watafurahi – licha kuniunga mkono. Bali lililokuwa likitarajiwa kwao na kila awajuae, ni jawabu. Lakini hilo hawakulifanya; na badili yake wamenipiga vita, na wakipata nafasi kunitukana katika madarasa yao.
Ingawa kitabu hakikujibiwa, lakini nilipata kumsikia mmoja katika wao akitowa huja mbili ambazo tutazitaja hapa chini amoja na jawabu zake: -
1. Kwa nini mimi nikakanya maasia ya matari, namengineo nisiyakanye?
Jawabu:
a) Kwa sababu maasia mengine yakanywa na wengi, lakini haya hakuna ayakanyae.
b) Hakuna maasia aovu kuliko yafanywayo ni ibada; wala sijui maasia yaliyofanywa ni ibada isipokuwa ngoma hii.
2. Kiwa itendo cha yule kijakazi aliyempigia Mtume (s.a.w.) tari kilikuwa ni kitendo cha Shetani, basi kwa nini Mtume (s.a.w.) akakubali kufanywa kitendo hicho mbele yake?
Jawabu:
Hivi ni kusema kuwa hasadiki Hadithi hii au hamsadiki mwenye Hadithi hiyo (yaani Mtume – s.a.w.). Haifai kwa Muislamu kumuuliza Mtume (s.a.w.) “Kwa nini?” Inawezekana hapo alipotokea sayyidna ‘Umar ndipo uliposhuka wahyi wa kukatazwa ngoma hiyo, na Mtume (s.a.w.) akaikataza kwa kuinasibisha na Shetani.
Katika chapa hii ya pili hatukuongeza kitu isipokuwa kuisemea nukta moja iliomo katika Hadithi ya wale vijakazi waliompigia matari Mwana ‘aishah (r.a.) siku ya Idd, iliyotajwa mwisho wa mlango wa “Hali ya kuwa Shubha”, (uk. 12) nayo ni hii: -
Haithi inaeleza kuwa S. Abubakr (r.a.) alikwenda katika hema la Mtume (s.a.w.) hapa Minaa, akawakuta vijakazi (au banati) wanampigia Mwana ‘Aishah vitari. S. Abubakr akawakaripia na kuwakataza; na Mtume (s.a.w.) akamwambia, “Waache, Abubakr, leo ni Idd”.
Linalofaa kuzingatiwa katika Hadithi hii ni hili: kwa nini S. Abubakr (r.a.) aliwakaripia na kuwakataza hao banati wasipige matari yao? Ana “uthority”gani Abubakr ya kukataza jambo ambalo hakumsikia Mtume (s.a.w.) akilikataza? Lisilokuwa na shaka hapa ni kuwa S. Abubakr alimsikia Mtume (s.a.w.) akikataza matari, ndipo naye alipokataza. Na maneno ya Mtume (s.a.w.), “Waache Abubakr, leo ni Idd” yanaonesha wazi kuwa lau kama haikuwa idd Mtume (s.a.w.) asingewapa ruhusa kupiga matari.
Wassalam alaykum
SHARIFF ABDULLA SALIM AL-HUSEINY
- Login or register to post comments
- Email this page


