08-Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah: Sura Ya 6: 'Aqiydah, Manhaj Na Upinzani

 


Sura Ya 6: ‘Aqiydah, Manhaj Na Upinzani

 

Alhidaaya.com

 

 

 

‘Aqiydah Na Manhaj Yake

 

Ibn Taymiyyah alikana utumiaji wa akili kwa ufahamu wa Asmaa Wa Swifaat (Majina Matukufu na Sifa za Allaah) kwani hiyo haikuwa ni mwenendo bora ulioafanywa na Salaf. Alitoa hoja kwamba Swahaba na vizazi vya mwanzo havikukimbilia hifadhi ya maelezo ya kifilosofia katika ufahamu wa Majina Matukufu na Sifa zake. Aliendelea kutoa hoja kwamba iwapo Salaf wangeliona manufaa yoyote katika kupata hifadhi katika kalaam (hoja za maneno matupu ya kiakili na falsafa) wangelifanya hivyo na wangelihimiza. Hivyo, Ibn Taymiyyah alituhumiwa na wapinzani wake kwamba ni mtu aliyekuwa na elimu ya Dini isiyostaarabika kutokana na msimamo wake katika Majina na Sifa za Allaah.

 

Ukweli ni kwamba, ndani ya kitabu chake ‘Aqiydatul Waasitwiyyah, Ibn Taymiyyah amekana msimamo wa Mushabbihah (wale wanaofananisha uumbaji wa Allaah: wenye elimu ya Dini isiyostaarabika) na wale wanaokaidi, kukana, na kukimbilia hifadhi ya tafsiri za kilahaja na kimaana kwenye Majina na Sifa tukufu. Ametoa hoja kwamba mtindo wa Salaf ni kuchukua njia ya kati na kati baina ya mipaka iliyochupa mpaka katika elimu ya Dini isiyostaarabika na ile ya kukana. Akaendelea kueleza kwamba Salaf wamekubali kwamba Majina yote na Sifa za Allaah bila ya tashbiyh (kuanzisha ufananisho), takyiyf (kuchunguza ni kwa namna “gani” zimegandana na utukufu), ta’twiyl (kukana/kukaidi maana za juu), na bila ya ta-awiyl (kuipa maana ndogo, kugeuza maana halisi).

 

Mara nyingi husimuliwa tokeo maarufu la Maalik Ibn Anas ambaye alimjibu mtu moja kwa moja na kwa maneno machache kabisa ambaye aliuliza: Ni namna gani Allaah alivyo/kuwepo (istiwa) juu ya ‘Arshi? Alijibu kwamba “uibukaji/uwepo” (istiwa) unajulikana, “kivipi” hakutambulikani, “kuwa na imani juu ya hilo” ni lazima, na “kufanya uchunguzi na kuulizia kuhusiana na masuala hayo” ni uzushi wenye kulaumiwa (bid’ah). Hivyo Imaam Malik anakubali maana bora lakini bila ya kulinganisha, wenye kuanzisha unamna gani, na bila ya kutafuta hifadhi ya maana za kitashbihi.

 

Shaykh al-Islaam Ahmad Ibn ‘Abdil-Haliym Ibn Taymiyyah anatambulikana kama ni mmoja katika Mujaddid (waliouhuisha/walioboresha Dini upya baada ya kuingia uharibifu) muhimu sana katika Uislamu. Iwapo jitihada za Mujaddid zinazalisha matunda ndani ya enzi zake na kizazi chake, jitihada za Shaykh al-Islaam Ibn Taymiyyah zimeanza kutoa matunda ndani ya enzi zake na zinaendelea kufanya hivyo hadi hii leo na hadi Qiyaamah, Wanachuoni walioathirika na watafutaji wa elimu na makundi ya Kiislamu yenye kutokana na Ahlus-Sunnah wal-Jamaa’ah. Wanachuoni wangali wanarejea vitabu vyake katika kuwakana maadui wa Uislamu miongoni mwa Mayahudi na Wakiristo na Madhehebu yanayodai kuwa yanatokana na Uislamu kama vile Maraafidhah (Shia), Khawaarij, Mu’utazilah Huluuliyyah na Jahamiyyah, na madhehebu ya uzushi kama vile Ash’ari’ah (Masufi) na Murji-iah.

 

 

Mafanikio yake ndani ya Nyanja za Fiqh, Hadiyth, tafsiyr na suluuk (njia za kujikurubisha karibu kwa Allaah) zinajulikana vyema kwetu hadi kutohitajia kutoa mifano yoyote hapa. Vitabu vyake na maandiko yake yanashuhudia ushahidi katika hilo na wala hahitajii yeyote miongoni mwetu kumsifia, isipokuwa elimu na Fiqh yake ni yenye kubaki na inashuhudia kwamba hakuna anayeiikana isipokuwa kwa yule aliyekuwa mjinga na mkaidi na hasidi mwenye chuki.

 

 

Viapo vya Maimamu wa enzi zake na enzi zilizofuata zinaonesha dhahiri kwa mtu mwenye akili iliyo wazi uongo wa madai uliobuniwa na maadui wa Uislamu na maadui wa Sunnah dhidi ya Imaam huyu muhimu, na kuweka wazi elimu yake, ufahamu wake na umakini wa hoja. Hivyo, tunaelewa sababu kwanini watu wa kufr na uzushi wanampiga vita dhidi yake, ni kwa sababu kwamba aliivuruga misingi yao na

 

قَدْ مَكَرَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ فَأَتَى اللَّـهُ بُنْيَانَهُم مِّنَ الْقَوَاعِدِ فَخَرَّ عَلَيْهِمُ السَّقْفُ مِن فَوْقِهِمْ وَأَتَاهُمُ الْعَذَابُ مِنْ حَيْثُ لَا يَشْعُرُونَ﴿٢٦﴾

Walikwishafanya makri wale wa kabla yao, basi Allaah Aliyasukua majengo yao kwenye misingi, sakafu zikawaporomokea juu yao, na ikawajia adhabu kutoka pande wasizozitambua.   (An-Nahl 16:26)

 

 

Shaykh al-Islaam anaelezea ‘Aqiydah yake ya kisalafi[1]  ndani ya fataawa:

“Vizazi vya mwanzo vya Ummah huu na Maimamu wao wote kwa pamoja wanakubaliana kwamba hakuna chochote chenye kufanana na Allaah, si katika asili Yake wala sifa Zake au matendo Yake. Mmoja katika Maimaam alisema: Yeyote anayemlinganisha Allaah na uumbaji Wake ni kaafir, na yeyote anayekana kwa kile Allaah Alichojisifia Mwenyewe ni kaafir; hakuna chochote ambacho Allaah Amejifananisha Mwenyewe au Rasuli wake alichomlinganisha na Yeye.”[2]

 

 

Yeye (Rahimahu Allaah) pia amesema:

 

“Tamko ambalo ni madhubuti kuhusiana na masuala yote haya ni kwamba Allaah Afananishwe kama vile Alivyojifananisha Mwenyewe au kama alivyofananishwa na Rasuli Wake, na kama vizazi vya mwanzo vilivyomfananisha, na sisi hatuhitajiki kuvuka mpaka kwa yale yaliyosemwa na Qur-aan na Hadiyth.”

 

Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema: “Allaah asifananishwe isipokuwa kwa namna Aliyojifananisha Mwenyewe au kama alivyomfananisha Rasuli wake, na mtu asichupe mpaka dhidi ya Qur-aan na Hadiyth.”

 

Mwenendo wa Salaf ulikuwa ni kumfananisha Allaah kama vile Alivyojifananisha Mwenyewe na kama Alivyomfananisha Rasuli Wake, bila ya kuharibu au kukana, na bila ya kuuliza ni namna gani au ulinganisho Wake na viumbe Vyake. Tunafahamu kwamba yale ambayo Allaah Amejifananisha nayo Mwenyewe ni kweli, na wala hakuna maajabu au kitu chenye kubabaisha katika hilo, isipokuwa maana zake zieleweke kwa yule Mmoja Aliyesema hayo yaeleweke hivyo, haswa pale aliyesema hayo ni mwenye elimu zaidi kwa yale anayosema kuliko watu wengine wote na mwenye kufahamika na mwenye kuweza kueleza kile anachokitaka kueleza, na mwenye ufasaha katika kueleza, kutafsiri na kuongoza.

 

Kwa kuongezea na yote haya, hakuna chochote kinachofanana na Allaah, aidha kwa hali ya utukufu Wake au majina Yake na sifa au matendo. Tunaamini kisawasawa kwamba Yeye ana hali ya kweli na kwamba Ana matendo ya kweli, na sifa za kweli. Hakuna chochote chenye kufanana na Yeye, hali Yake, sifa au matendo. Iwapo kuna chochote kinachomaanisha upungufu au kwamba Yeye ana mwanzo, Yupo mbali kabisa na hilo kwa ukweli haswa, na Yeye afikiriwe kuwa ni mkamilifu katika namna ambayo hakuna ukamilifu juu yake. Yeye hana mwanzo na hakuna uwezekano wa kwamba Yeye ameumbwa, kwa sababu hakuna wakati ambao yeye hakuwepo. Kwa kitu chochote kuweza kuumbwa kinamaanisha kwamba kulikuwa na wakati ambao hakukuwepo, na kwamba uumbaji huo unahitaji muumbaji, lakini Yeye Ameendelea kuwepo tokea enzi zote.

 

 

Muono wa Salaf ni ule wa usasa, sio kwa kukana sifa tukufu wala kumlinganisha Allaah na viumbe Vyake. Hawazilinganishi sifa za Allaah katika sifa za viumbe Vyake, kama ambavyo hawailinganishi hali Yake na hali ya viumbe Vyake. Hawakaidi kwamba yale ambayo Amejisifia Mwenyewe au yale ambayo Rasuli Wake Amemsifia, inayopelekea kukana majina Yake matukufu na sifa zinazovuta hisia, na kuyatoa maneno kutoka sehemu (yake) sahihi (rudia An-Nisaa 4:46) na kuyakimbia majina na alama za Allaah (Fusswilat 41: 40).

 

 

 

Wote wanaokana sifa za Allaah na wale wanaomlinganisha Yeye kwa viumbe Vyake ni wenye hatia ya makosa yote. Wale wanaokaidi Sifa zake na kushindwa kuelewa majina yake na sifa za Allaah isipokuwa kwa namna ambayo inanufaisha viumbe hai, kwa hiyo wanakana dhana hizi na hivyo kuunganisha makosa yote; awali ya yote wamemlinganisha Yeye na viumbe Vyake, kisha wakakana sifa Zake kutokana na hilo. Kwamba ulinganisho wa majina hayo na sifa ni kwa kuweza kueleweka kutokana na majina na sifa za viumbe Vyake, kisha wakakana sifa ambazo Anastahiki kuwa nazo ambazo ni zake Allaah, Mwenye kushukuriwa na kusifwa.[3]

 

Jibu kwa Wale Wanaodai Kwamba Alikuwa ni Mwenye Elimu Ya Diyn Isiyostaarabika

 

Ibn Hajar al-Haythamiy (ni mmoja wa Fuqahaa mkubwa wa ki Shaafi’iy, aliyekufa mwaka 974 H na ni mtu ambaye ni mwengine kinyume na Ibn Hajar al-’Asqalaaniy, mwandishi wa Fat-h al-Baariy aliyefariki mwaka 852 H) amewatolea hoja Mashaykh wawili wa Uislamu, Ibn Taymiyyah na mwanafunzi wake Ibn al-Qayyim, kwa mapana sana na kuwatuhumu kwamba ni wenye kumuelezea Allaah katika maelezo ya kimaumbo, wakimlinganisha yeye na viumbe Vyake, na imani nyengine zisizo na mashiko. Lakini alijibiwa na wengi, ambao walieleza uongo wa yale aliyoyaeleza na kufafanua kwamba Maimaam hao wawili walikuwa safi na mbali na imani yoyote inayokwenda kinyume na Qur-aan na Sunnah. Mmoja wa Wanachuoni waliyemjibu vizuri alikuwa ni:

 

 

-Al-Mulla ‘Aliy Qaariy (Rahimahu Allaah), ambaye amesema, baada ya kunukuu tuhuma za Ibn Hajar al-Haythamiy dhidi yao na hoja zake dhidi ya Aqiydah zao:

 

 

Ninasema: Allaah Awalinde wao – yaani Ibn al-Qayyim na Shaykh wake Ibn Taymiyyah – kutokana na tuhuma kubwa kabisa. Yule ambaye anasoma Sharh Manaazil as-Saa’iriyn cha Nadiym al-Baariy al-Shaykh al-Ansaariy, ambaye ni Shaykh wa Uislamu kwa mujibu wa Masufi, ataona kwa uwazi kwamba walikuwa ni miongoni mwa Ahlus Sunnah wal Jamaa’ah na kwa hakika ni miongoni mwa awliyaa (marafiki wa karibu wa Allaah) wa Ummah huu. Miongoni mwa aliyosema ndani ya kitabu kilichotajwa ni yafuatayo:

 

 

“Maneno haya ya Shaykh al-Islaam yanadhihirisha nafasi yake kama ni Mwanachuoni mkubwa wa Ahlus-Sunnah, na nafasi yake miongoni mwa Wanachuoni, na inaonesha kwamba yeye ni msafi kwa wale maadui wake wa ki-Jahami wanayomtuhumu nao, kwamba amemlinganisha Allaah na viumbe Vyake, kama vile Raafidhah wanavyowatuhumu wao kuwa ni ma Naasibi, na Naasibi wanawatuhumu wao kuwa ni Raafidhah, na Mu’tazilah wanawatuhumu wao kuwa ni wenye elimu ya Diyn isiyostaarabika. Huo ndio urithi wa maadui wa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambao wanamtuhumu yeye na wafuasi wake kwa kubuni dini mpya. Na huu ni urithi ambao Wanachuoni wa Hadiyth na Sunnah kutoka kwa Nabiy wao na kwamba watu wa uongo wanawapa wao anwani za kijinai.

 

Allaah Amrehemu ash-Shaafi’iy, Ambaye Amesema Pale Alipotuhumiwa Kuwa Ni Raafidhi:

 

Iwapo kuwa ni Raafidhi inamaanisha kuwa na mapenzi na familia ya Muhammad, basi waache makabila mawili (ya binaadamu na majini) kushuhudia kwamba mimi ni Raafidhi.

 

 

Allaah Amrehemu Shaykh wetu Abul-‘Abbaas Ibn Taymiyyah pale aliposema:

Iwapo kuwa ni Naasibi inamaanisha kuwa na mapenzi na familia ya Muhammad, basi waache makabila mawili (ya binaadamu na majini) kushuhudia kwamba mimi ni Naasibi.

 

 

Allaah Amrehemu Wa Tatu – Ibn al-Qayyim – Pale Aliposema:

 

Iwapo kuwa ni mwenye elimu ya Diyn isiyostaarabika inamaanisha kuwa na msimamo thabiti wa sifa tukufu na kuzinasibisha hizo kuwa juu ya maana ya muongo, Basi shukrani zote ni za Allaah, mimi ni mwenye elimu ya Diyn isiyostaarabika, walete mashahidi wako.”[4]

 

 

-Wanachuoni Wa Kamati Ya Juu Ya Fatwa Waliulizwa:

Watu wanasema kwamba Ibn Taymiyyah alikuwa si mmoja katika Ahlus Sunnah wal Jama’ah, na kwamba alipotea na kuwapotosha wengine, na kwamba hili ni kwa maoni ya Ibn Hajar na wengineo. Je, kwa hayo wanayoeleza ni kweli au la?

 

 

Wakajibu:

 

 

Shaykh Ahmad Ibn ‘Abdil-Haliym Ibn Taymiyyah ni mmoja wa Imaam wa Ahlus Sunnah wal Jama’ah, ambaye aliwaita watu katika ukweli na katika njia sahihi. Allaah aliisimamisha Sunnah kwa kumtumia yeye na kuwavunja nguvu wafuasi wa uzushi na uzushi na ukafiri. Yule ambaye anamtambua kama ni mwengine zaidi ya hivyo ni yule ambaye ni mzushi na amepotea na anawapotosha wengine. Wamesikia mambo ya uongo kuhusiana naye, na wanafikiria kwamba ukweli ulikuwa ni uongo na uongo ulikuwa ni ukweli. Hayo yanatambuliwa na yule ambaye Allaah Anamuongoza na yule anayesoma kitabu chake na vitabu vya wapinzani wake, na kulinganisha wasifu wake na wao. Hii ni bora na ushahidi thabiti baina ya pande hizo mbili.[5]

 

Hivyo, iwapo tunatambua hapa kwamba yale yaliyoelezwa na watu kwamba alikuwa ni mwenye elimu ya Diyn isiyostaarabika na alikufuru Aqiydah sahihi na kumlinganisha Allaah, Allaah Atukuzwe, na sifa za viumbe Vyake, ni uongo uzushi ulio wazi na uongo ulio dhahiri dhidi ya Shaykh al-Islaam na mtindo wake na Aqiydah. Yeyote anayesoma aina ya vitabu vyake vikubwa ama vidogo atalitambua hilo.

 

 

 

 

[1] Vizazi vitatu ambavyo vimesifiwa na Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) “Viumbe bora ni katika vizazi vyangu (au karne zangu), kisha wanaowafuata wao, kisha wale wanaokuja baada yao. Kisha watakuja watu ambao hawatojali iwapo matamshi yao yanakuja baada ya kiapo au kinyume chake (yaani, hawatochukulia umuhimu wa masuala kiuzito wake).” (Imepokewa na al-Bukhaariy, Muslim na at-Tirmidhiy).

[2] Fataawa ya Shaykh al-Islaam (2/126).

[3] Fataawa Shaykh al-Islaam (5/26-27) 

[4] Mirqaah al-Mafaatiyh, al-Mulla ‘Aliy Qaari (8/146, 147). Maneno yaliyo baina ya alama za nukuu “” zilinukuliwa na al-Mulla ‘Aliy Qaari kutoka kwa Imaam Ibn al-Qayyim, kutoka katika kitabu chake cha Madaarij al-Saalikiyn bayna Manaazil Iyyaaka Na’budu wa Iyyaaka Nasta’iyn (2/87, 88).

[5] Shaykh ‘Abdul-‘Aziyz Ibn Baaz, Shaykh ‘Abdur-Razzaaq ‘Afiyfiy, Shaykh ‘Abdullaah Ibn Ghadyaan, Shaykh ‘Abdullaah Ibn Qa’uud. Fataawa al-Lajnah al-Daa’imah (2/451, 254).

Share