'Aqiydah Iwe Mwanzo

Shaykh Swaalih Al-Fawzaan (Hafidhwahu Allaah)

 

 

 

Jambo la kwanza, kubwa, na la msingi katika kulingania watu kumtii Allaah, na kwa nini ‘Aqiydah iwe mwanzo.

 

‘Aqiydah ni lazima ije mwanzo kwa sababu, kinachozusha mgawanyiko na maangamizi katika ulimwengu wa Kiislamu ni kukosekana ‘Aqiydah iliyo sahihi.

 

 

Kwa Nini ‘Aqiydah Liwe Ni Jambo La Mwanzo?

 

Hakika ‘Aqiydah lazima ije mwanzo kwa sababu ni msingi wa Da’wah ya Mitume wote kama Allaah Alivotuma ujumbe Wake kupitia kwa Mitume Wake. Kama Anavyosema Allaah kwa kupitia kwa ulimi wa kila Mtume Aliyemtuma kwa watu wake:

“Enyi watu! Muabuduni Allaah, hamna mungu isipokuwa Yeye” (Surat Huud 11: 84)

 

‘Aqiydah lazima ije mwanzo kwa ajili ya kuepukana na kizuizi cha kubakia motoni (Jahannam) milele na kujiepusha na adhabu hiyo. Hamujasikia maneno ya Allaah Aliyetukuka:

“Hakika Allaah hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa Amtakaye. Na anayemshirikisha Allaah basi hakika amezua dhambi kubwa”

(Suratun Nisaa 4: 48)

 

Kumshirikisha Allaah ni dhambi kubwa ambayo inampelekea mja kutoka kwenye Tawhiyd (kumpwekesha Allaah), na Tawhiyd ni msingi wa usahihi wa ‘Aqiydah.

 

‘Aqiydah ni lazima iwe mwanzo vilevile kwa ajili kumshirikisha (Shirk) Allaah ni dhambi kubwa ambayo ni dalili ya madhara juu yetu kama Allaah Alivyosema:

“Kwani hakika ushirikina bila ya shaka ni dhulma iliyo kubwa” (Suratul Luqmaan 31:13)

‘Aqiydah ni lazima ije mwanzo kwa sababu, kinachozusha mgawanyiko na maangamizi katika ulimwengu wa Kiislamu ni kukosekana ‘Aqiydah iliyo sahihi na watu kufuata ‘Aqiydah zisizo sahihi.

 

Ndio maana ‘Aqiydah nyingi za Waislamu zimejaa ufisadi kwa mambo ambayo ni shirk kubwa kwa mfano utakuta watu wanatufu (wanazunguka) kwenye makaburi na kuwaomba maiti waliomo ndani ya makaburi hayo wawasaidie haja zao na kudhani kufanya hivyo watapata mahitaji yao na kukidhiwa shida zao.

Na kwa hali hiyo, watu kama hawa wamerudi nyuma kiwakati, wanajirudisha katika wakati wa Jaahilliyah (zama za ujinga kabla ya Uislamu). Na wanajifanya kama hawajasikia maneno ya Allaah Aliyetukuka:
‘‘Mkiwaomba hawasikii maombi yenu; na hata wakisikia hawakujibuni. Na Siku ya Qiyaamah watakataa ushirikina wenu. Na hapana atakayekupa khabari vilivyo kama Yeye Mwenye khabari”

(Suurat Faatwir 35: 14)

 

Na sisi tunawakataza kufuata uzushi wa Masufi ambao wameweza kuueneza kwa watu wa kawaida wasio na elimu na hadi taqriban nchi mbalimbali zimekuwa zikiongozwa na kutawaliwa na uzushi wa hawa Masufi na bid’ah zao kama vile Mawlid. Na hata uzushi wa aina mbalimbali kama kuwaiga Makafiri katika sherehe zao na sikukuu zao, achilia mbali uzushi mbalimbali wanaoufanya katika Dini ambao umegawa nchi zao na kuziweka mbali na Qur-aan na Sunnah.

 

Kwa haya machache ndugu yangu mpendwa, tumejaribu kuwaonyesha ukweli ya kwamba ‘Aqiydah ni jambo la muhimu na la mwanzo katika maisha yako na daima ‘Aqiydah inapaswa iwe mwanzo.

 

 

 

Share