Matari
Matari yana hali tatu:
1. KUTUMIWA KAMA IBADA.
TARI ni namna ya NGOMA zilizoanza kabla ya Uislamu* kama tulivyosema katika kitangulizi. Na bila shaka yoyote hao waliozua ngoma hii na walioipokea baada yao, walikuwa wakiifanyani kama ngoma nyenginezo. Kwa sababu hii mwenye kufanya TARI ni IBADA huwa ameanya mchezo na pumbao kuwa ni IBADA. Na kwa sababu hii ndipo wafasiri wetu wakubwa Swawy na Jamal, katika kufasiri aya ya 70 ya Suratul An’aam iliyosema, “Waachilieni mbali wale wanaofanya dini yao niPUMBAO na MCHEZO …”, waliposema, “Anaingia katika aya hii kila mwenye kufanya dini ya Islam ni PUMBAO (au upuuzi) namchezo kama Khawariji na baadhi ya wale wanaodai kunasibikana na watu wema, waliofanya ndia ya kwenda kwa Mwenyezi Mungu (yaani ibada) ni NGOMA na UMARI, a wakazua mambo ambayo si halali katika Dini ya Mwenyezi Mungu”.
Hivi ndivyo walivyosema wanavyuoni wa Kiislamu juu ya TARI lililofanywa ni ibada; wala hakuna mwanachuoni yoyote aliyesema kuwa inafaa kufanya TARI au ngoma ya namna yoyote kuwa ni ibada.
Na huja kubwa kuliko hizo ni kuwa Mtume (s.a.w.) alisema katika Hadith sahihi ya yule kijakazi aliyempigia tari wakati aliporudi kutoka jihadi (ambayo tutaitaja kwa ukamilifu huko mbele) kuwa “hicho ni kitendo cha shetani”, na hapaa asubutue kusema kuwa kitendo kilichonasibishwa na shetani kinafaa kuitwa “ibada”.
2. KUTUMIWA KAMA NGOMA TU.
Matari iwapo hayakukusudiwa ibada bali yamekusudiwa sherehe au pumbao n.k. yatakuwa na hali tatu:
A. HALI YA KUWA HALALI.
B. HALI YA KUWA HARAMU.
C. HALI YA KUWA SHUBHA (yaani kuwa iko shaka baina ya kufaa na kutofaa)
A. HALI YA KUWA HALALI.
Hali hii ni iwapo yanapigwa kwa ajili ya kutangazia harusi. Zimekuja Hadithi nyingi kuamrisha ndowa zitangazwe kwa matari. Na ingawa Hadithi zote hizo hazina nguvu lakini zinakubaliwa kwa sababu ya wingi wake kama alivyobaini mwenye Subulus Salam. Lakini sio ndani ya msikiti: ama ile Hadithi iliyopokewa na Tirmidhy iliyosema, “Itangazeni ndoa hii na muifanye katika Msikiti, na muipigie matari” tutakuja isemea katika mlango utakaofuata.
B. HALI YA KUWA HARAMU.
Hali hii ni iwapo matari hayo yamepigwa ndani ya msikiti kwa sababu yoyote, hata kama ni kwa ajili ya arusi, kwa huja zinazofuata:
(a) Katika sheria popote linapokatazwa jambo dogo, huwa kubwa kuliko hilo linakatzwa zaidi. Kwa mfano: Katika Qur’an tumekatazwa kuwaudhi wazee wawili hata kwa tamko la “uffin” (lenye maana ya kuwachoka wazee), au kuwakaripia. Haikutaja kuwatukana au kuwapiga. Lakini kwa kukatazwa hayo madogo, imefahamika kuwa haya makubwa ambayo yanaudhi zaidi, yanakatazwa zaidi kwa nassi ya Qur’an au kwa “qiyasul aulawy”.
Basi vile vile Qur’an ilipowakemea na kuwaukana wale waliokuwa wakipiga makofi na miuzi ndani ya msikiti (aya ya 35 ya Suratil Anfaal) imefahamika vile vile kupiga matari vigoma na firimbi yanatukanwa na kukemewa zaidi kwa nassi au kwa “qiyasul aulawy”: kwani ghasia za ngoma hizo ni kubwa zaidi kuliko ghasia za makofi na miuzi.
(b) Wanavyuoni wote wanaofaa kutegemewa na waliotaja mas-la ya kupiga matari katika msikiti, wamekataza hilo kama utakavyoona, wala hapana waliokubalisha isipokuwa hao wenyewe walioanza kutia matari katika misikiti, ambayo vitendo vyao au maneno yao si huja katika dini, khasa iwapo yanakhalifu nassi ya Qur’an na waliowafuata wao.
(c) Kupiga matari katika misikiti ni kuyafanya ni katika ibada ya Kiislam, na kuifananisha misikiti ya Kiislam na misikiti ya Kibaniani.
(d) Haikupokewa Hadith sahihi wala dhaifu kusema kuwa hili limepata kufanyika wakati wa Mtume (s.a.w.) au zamani za Masahaba au Tabi’ina.
MATATIZO YALIOKO
Sasa tutaingilia zile huja wanazozitegmea hao wanaohalalisha kupiga matari katika msikiti, na tuvunje moja moja.
(HUJA YA KWANZA): Hadith iliyopokewa na Tirmidhy iliyosema, “Itangazeni hii ndowa; muifanye katika msikiti; na muipigie matari …”, wanasema kuwa Hadith hii inatowa ruhusa kupiga matari katika misikiti.
Jawabu: Kila mwenye kusoma hadith hii anafahamikiwa wazi wazi kuwa matamko haya: “Muifanye katika msikiti”, yanakhusu ndowa tu, hayakhusu matari. Dhahiri ya hadith ni kuamrisha watu kutangaza ndowa kwa ndia mbili: kuifanya misikitini na kuipigia matari. Kukusanya mambo mawili haya kuwa yote yafanywe katika msikiti ni mbaranganyo usiokubaliana na Hadith hii. Makusudio ya Hadith hii yako wazi, ni kuitangaza ndowa kwa kuifanya misikitini ili wajue waliohudhuria ndani ya msikiti; na ipigiwe matari ili kutangazia wengineo ambao hawakuhudhuria hapo msikitini. Basi iwapo mambo mawili haya yatakusanywa katika msikiti litakuwa limepatikana tangazo la namna moja tu.
Kwa sababu hii amesema mwenye I’anatut Talibiin (Sherehe ya Fat-ul Mu’in) katika juzuu ya tatu “Sio makusudio kuwa (hayo matari) yapigwe ndani ya msikiti, bali hayo ni ya kufanywa nje, amri ya kufanya msikitini inakhusiana na kufunga ndoa tu (Haikhusiani na kupiga matari)”.
Na amesema Dahlawy mwenye Lama’at sherehe ya Mishkaat katika uk. 164 katika kufasiri Hadithi hii: “… lakini matari yatapigwa nje (sio ndani msikiti)”. Na amesema Sheikh Muhammad al-Hifny, katika Sirajul Munir sherehe ya Jamius Saghiir, uk. 235, juzzu ya 1 ya kitabu hicho kufasiri Hadithi hii, “Ikiwa ndowa imefanywa Msikitini, matari yatapigwa nje”.
Wala hapana hata mwanachuoni mmoja aliye bora kuliko hawa aliyesema kinyume cha walioyasema mabwana hawa. Na juu ya hayo haikupokewa Hadithi – hata dhaifu kuwa ilitukia kupigwa matari msikitini wakati wa Mtume (s.a.w.) au katika zama za Salaf (watangu wema) kaa tulivyoma mbele.
Na hapa lipo jambo moja la kufaa kuzingatiwa, Tarikh inaonyesha kuwa matari wakati huo yalikuwa ni ngoma za wanawake. Kwa hivyo utaona Hadithi zote za matari zinasema vijakazi … wanawake, banati, kama tutakavyozibaini huko mbele. Na si kweli kabisa kama Mtume (s.a.w.) ataamrisha wanawake wakapige matari msikitini mbele za watu waume!
(HUJA YA PILI): Hadithi iliyopokewa kwa Abu Dawud iliyosema “MWANAMKE mmoja alimwambia Mtume (s.a.w.): Ewe Mtume wa Allah nimeweka nadhiri kuwa utakaporudi salama katika Jihadi yako hii nikupigie tari “alaa ra’sik” (tutasema maana ya matamko haya). Mtume akamwambia: Kama umeweka nadhiri ondosha nadhiri yako; kama si hivyo usifanye…”
Wanasema hapa kwamba maana ya “alaa ra’sik” ni JUU YA KICHWA CHAKO. Wanasema tena: Kichwa cha Mtume (s.a.w.) ni bora kuliko msikiti. Basi ilipofa kupiga tari juu ya kichwa cha Mtume (s.a.w.), inafaa zaidi kupiga tari katika msikiti.
Katika kujibu huja hii, yako mambo 3 ya kuzingatiwa:
(a) Maana ya “alaa ra’sik”.
(b) Kukisia kichwa ca Mtume na msikiti.
(c) Ukamilifu wa Hadithi hii.
Tamko “alaa ra’sik” ambalo Kiswahili chake ni “juu ya kichwa chako” (kama walivyosema jamaa), hapa halina maana hayo. Waarabu husema “alaa ra’sik” kwa kusudia “mbee yako” (sio juu ya kichwa chako), kama vile tunavyosema kwa Kiswahili “usoni mwako” kwa kukusudia mbele yako. Amesema mwenye Mishkaat katika uk. 290 kama hivi: “Juu ya kichwa chako maana yake ni MBELE YAKO”. Na hivi ndivyo ilivyo katika Hadithi iliyokamilika tutakayoitaja karibuni.
Kwa tafsiri hii ya sawa, hapana tena njia ya kukisia “kichwa cha Mtume” na “msikiti”. Lakini hata tukichukulia maana hayo waliyoyachukulia wao, yaani tukasema kuwa makusudio ni KICHWA cha Mtume., pia tutaona kuwa kukisia heshima ya msikiti na heshima ya kichwa cha Mtume ni kiyasi kisichokubaliana na akili walasheria. Hatuwezi kusema kuwa maadamu inafaa kutia mafuta juu ya kichwa cha Mtume, vile vile inafaa kutia mafuta katika msikiti; au iwapo mtu akikaa msikitini anapata thawabu, basi akikaa juu ya kichwa cha Mtume atapata thawabu nyingi zaidi! Hakuna kukisia hukumu baina ya mtu na kitu katika sharia.
Hadithi tuliyotanglia kuiaja, na ambayo ghalibu ndiyo itolewao, na watetezi wa matari, ni kipande tu cha Hadithi iliyokamilika. Ukamilifu wake ni kama ifuatavyo:
Alitoka Mtume (s.a.w.) katika baadhi ya Jihadi zake aliporudi, akajiwa na kijakazi cheusi, kikamwambia: “Niliweka nadhiri kuwa Allah akikurudisha salama, nitapiga tari na kuimba MBELE Yako”. Mtume akamwambia: “Ikiwa umeweka nadhiri basi piga, na ikiwa si hivyo basi usifanye”. Akasema: “Nimeweka nadhiri”. Akawa anapiga tari na huku akiimba: “Tala al badru ‘alaynaa … kisha akainga Abubakr, nae anaendelea kupiga, kisha akaingia Ali nae anaendelea kupiga, kisha akaingia Uthman nae anaendelea kupiga; kisha akaingia Umar; hapo yule kijakazi akalibwaga lile tari chini ya matako na kulikalia. Mtume (s.a.w.) akasema: “Shetani anakukimbia Umar. Mimi nilikuwa nimekaa, nae anapiga; akaingia Abubakr, nae anapiga; kisha akaingia Aly, nae anapiga; kisha akaingia Uthman, nae anapiga. Ulipoingia wewe Umar, amelitupa tari na kulikalia!”
Hadithi hii ianweka wazi zaidi maaa ya Hadith iliyotangulia. Na linalofaa sana kuzingatiwa hapa ni maneno ya Mtume (s.a.w.) aliyomwambia Umar: “Shetani anakukimbia Umar…” Inafahamika katika maneno hayo kuwa kitendo alichofanya kijakazi yule kilikuwa ni katika uchochezi au pepesa za Shetani. Basi kitendo kilicho nasibishwa na shetani kitafaa vipi kufanywa ndani ya msikiti?
(HUJA YA TATU): Ni Hadith iliyopokewa na Bukhari na Muslim kwa Mw. Aishah (r.a.) akisema: “Nilimuona Mtume (s.a.w.) amesimama mlangoni pa chumba changu na Mahabashi wanacheza kwa sime zao ndani ya msikiti…”
Hadith hii iko wazi kuwa hao Mahabashi walikuwa wakicheza tu, haikusema kuwa walipiga tari au ngoma ya namna yoyote.
Na mchezo waliokuwa wakicheza ni mchezo wa kujizoweza kutumia silaha katika Jihadi. Michezo ya namna hii inatiliwa nuvu na kuhimizwa katika Dini ya Islam hata imefanywa ni nama ya Ibada. Amesema mwenye sherehe ya Mishkaat katika ukurasa wa 272 wa Juzuu ya kwanza ya kitabu hicho, katika kufasiri Hadith hii: “Hilo la kucheza ndani ya msikiti) liliruhusiwa kwa sababu mchezo wao ulikuwa ni wa silaha za vita kupigana na maadui wa Mwenyezi Mungu, kama vile kutupa mishale. Kwa hivyo umekuwa (mchezo huo) ni katika hukumu ya Ibada (ya kufaa kufanywa msikitini)”. Na wapi mchezo huu wa kishujaa na mchezo wa kwenda mrama na kutupa shingo!
Sijui kama hao wenye kutetea kupiga matari msikitini wanazo huja zaidi kuliko tatu tulizokwisha zisema. Kama ziko nyengie, tungependa zitolewe tuzione.
Na kabla ya kufunga mlango huu napenda kuwambia Masharifu wenzangu kuwa iwapo sisi tutaendelea kupiga ngoma zetu katika msikiti tutapata wapi huja ya kuwazuilia watu kupiga ngoma zao?
C. HALI YA KUWA SHUBHA.
Hali hii ni iwapo matari hayakukusudiwa Ibada, wala hayakukusudiwa kupigwa ndani ya msikiti wala kutangaza arusi. Katika hali hii wanavyuoni wanakhitalifiana:
(a) Wako waliokataza.
(b) Wako walioruhusu.
Wenye kukataza wmetegemea:
(a) Maneno aliyosema Mtume (sa.w.) katika Hadith ya yule kijakazi aliyempigia tari, akakinasibishakitendo cake na Shetani.
(b) Kufunga mlango wa kujizoeza kushughulika na upuuziamao ni moja katika sababu ya Waiamu kuvunjikiwa.
Wenye kutoa ruhusa wametegemea:
(a) Hadith ya wale banati na vijakazi waliompoke Mtume (s.a.w.) kwa matari wakati alipowasili Madinah.
(b) Hadith ya vijakazi (au banati) waliompigia mwana ‘Aishah matari, na Mtume (s.a.w.) akawapa ruhusa kwa sababu aliyoitowa mwenyewe Mtume (s.a.w.) kumwambia Sayyidna Abubakar (r.a.), “Waache Abubakar, hizi ni siku za Idd”.
- Login or register to post comments
- Email this page


