Skip navigation.
Home kabah

Firimbi

    Mas-ala ya Firimbi katika kuifanya ni IBADA au kuipiga ndani ya MSIKITI hayana khitilafu na mas-ala ya matari kama inavyodhihiria katika maneno ya Swawy na Jamal katika kufasiri aya ya 35 ya Suratul Anfaal tulizotangulia kuzitaja. Bila shaka penye kukatazwa miunzi, na firimbi pia inakatazwa kama tulivyobaini mbele.

    Kwa kuwa hapana hadithi iliyokuja kuhusu firimbi katika arusi au bila ya arusi wanavyuoni wamekhitalifiana baina ya kuwa hiyo firimbi inaruhusiwa au la. Ukitazama vitabu, utaona kuwa hata wale waliokubalisha matari bila ya arusi, kama mwenye Minhaj na wengineo wanakataza firimbi kwa jumla wenye kukataza ni wengi sana kuliko wenye kukubalisha

    Imam Nawawy aliposahihisha katika Minhaj kuwa firimbi ni haramu amesema mwenye Mughny katika ukurasa 407 wa juzuu ya 4 katika kutilia nguvu, “Hivi, (alivyosema Nawawy) ndivyo alivosahabisha Baghawy na ndiyo yanavyofahamisha maneno ya wanavyuoni wengi wakubwa wakubwa, ama huko kutilia nguvu kauli ya kwanza (isemayo kuwa ni halali), Rafi’iy amemfuta Ghazaly, na amefuata Bulqayny na wengineo kauli ya kwanza kwa kukosekana dalili ya kufaa kuzingatiwa yakuharamisha. Na amehadithia ibn Abdissalaam khitilafu za wanavyuoni juu ya sama’i ifanywayo kwa ala za pumbao na kwa matari na firimbi. Na akasema Assubky: sama’i - kwa namna hii ijulikanao ni uovu na upotevu; na ni katika vitendo vya wajinga na mashetani. Na mwenye kudai kuwa ni ibada, basi amesema uongo na amemzulia Mtume (s.a.w.). Na asemae kuwa (hiyo sama’i) inazidisha nguvu (katika ibada), basi huyo ni mjinga au ni shetani (anataka kupoteza watu). Na mwenye kumnasibisha Mtume (hiyo sama’i) anafaa kupewa adhabu kali, na anaingia katika kundi la wenye kumzulia Mtume (s.a.w.); na mwenye kumzulia Mtume kwa makusudi, naandalie makazi yake katika moto. Wala hii siyo njia ya Mawaly na Mwenyezi Mungu na walioko katika tapo lake wala sio kumfuata Mtume Wake, bali ni njia ya watu wa pumbao na michezo na mambo yasiyofaa. Na haya ni ya kukanywa kwa mkono na kwa ulimi na kwa moyo (Kila mtu ayakataze kwa anavyoweza). Na aliyehalalisha Sama’i katika wanavyuoni basi ni HAIKUTANGAMANA TARI NA FIRIMBI, wala wake na waume, wala asiyefaa kuangaliwa”. Na akayasema maneno haya pia – neno kwa neno - mwenye Tuhfah uk. 220 wa Juzuu ya 10