Duaa Ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم Baada Ya Kutoka Twaaif Matamshi Na Maana Yake
Du'aa hii 'adhiym ni Du'aa ya kipenzi chetu Mtume صلى الله عليه وآله وسلم Alipotoka Twaaif baada ya kufukuzwa na kupigwa mawe na watu Wa Twaaif. Na kabla ya hapo Mtume صلى الله عليه وآله وسلم Alikuwa Makkah na kabla ya kwenda Twaaif alipatwa na msiba wa kufiwa na watu wawili waliokuwa muhimu
Kifo cha 'Ammi yake Abu Talib ambaye ingawa hakuingia uislamu lakini alikuwa akimhifadhi kutokana na maudhi ya maquraysh wa Makkah. Kisha kikafuata kifo cha mke wake mpenzi Bibi Khadija رضي الله عنها ambaye alikuwa akimliwaza
Du'aa hii inatupa mafundisho makubwa kuwa tunapofikwa na maudhi ya kutokana na watu jambo muhimu ni kumkabili Mola Mtukufu na kumshtakia Yeye Pekee na muhimu zaidi ni kutaka Radhi Zake Mola.
Baada ya kuomba Du'aa hii akaendelea kurudi Makkah na alipofika Qarn Al-Manaazil Allaah سبحانه وتعالى Alimtumia Jibriyl عليه السلام pamoja na malaika wa majabali na kumuuliza kama atapenda waifukie Makkah na waangamizwe watu baina ya 'Akhshabayn' (majabali mawili) lakini Mtume صلى الله عليه وآله وسلم kwa upole na khuluq (tabia) yake njema alikataa na kujibu maneno haya yenye kutia moyo kabisa na kutuzidishia imani na mapenzi ya Mtume wetu صلى الله عليه وآله وسلم .
Alisema:
((بل أستأني بهم . لعل الله أن يخرج من أصلابهم من يعبده لا يشرك به شيئا))
((Nitasubiri nao (nitastahmili nao) Pengine Allaah Atatoa katika migongo
(Al-Bukhaariy na Muslim)
DU'AA
اَلَّلهُمَّ إِنِّي أَشْكُو إِلَيْكَ ضَعْفَ قُُوَّتِي, وَقِلَّةَ حِيْلَتِي, وَهَوَانِي عَلَى النَّاسِ, يَا أَرْحَمَ الرَّاحِمِين, أَنْتَ رَبُّ الْمُسْتَضْعَفِينَ وَاَنْتَ رَبّي إِلَى مَنْ تَكِلْنِي؟ إِلَى بَعِيدٍ يَتَجَهَّمُنِي أَمٍ إِلَى عَدُوٍ مَلَّكْتَهُ أَمْرِي؟ إِنْ لَمْ يَكُنْ بِكَ غَضَبٌ عَلَىَّ فَلاَ أُبَاِلي، وَلَكِنَّ عَافِيَتَكَ أَوْسَعُ لِي مِنْ ذُنُوبِي, أَسْأَلُكَ بِنُورِ وَجْهِكَ الَّذِي أَشْرَقَتْ لَهُ الظُّلُمَاتُ، وَصَلَحَ عَلَيْهِ أَمْرُ الدُّنْيَا وَالأَخِرَةِ مِنْ أَنْ يُنْزِلَ عَلَيَّ غَضَبُكَ أَوْ يَحِلُّ عَلَىَّ سَخَطُُكَ وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِكَ
Allaahumma Inniy Ashkuu Ilayka Dha'fa
Ya Allaah , Kwako peke Yako nalalamika udhai'fu wa nguvu zangu, na uchache wa uwezo wangu na unyonge wangu (wa kukabili adha) za watu. Wewe Ndiye Mwenye wingi wa Rehma na wingi wa Huruma na Upole.
Wewe ni Mola wa wasiojiweza na wadhaifu. Nawe ni Mola Wangu. Unanitupa kwenye mikono ya nani (atakayenisaidia)? Kwenye mikono ya jamaa yangu aliye mbali na asiye na huruma na mimi? Ambaye ananihamakia kwa chuki na kunidharau? Au kwenye adui aliyepewa utawala juu ya mambo yangu? Lakini kama ghadhabu Yako haitoanguka kwangu au haitonifikia basi hakuna kitu nitakachojali. Na hakika msamaha Wako ni mkubwa kuliko dhambi zangu.
Nakuomba kutokana na Nuru ya Wajihi wako, ambayo inaangazia mbingu na inaondoa kiza na kutawala mambo yote ya dunia na akhera ili hasira Yako isinifikie au ghadhabu Yako isiniangukie. Na hakuna mamlaka wala nguvu na uwezo ila Wako peke yako.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


