Tahadhari Dhidi Ya Kuenea Dini Ya Maraafidhah (Mashia) Ndani Ya Ardhi Za Waislamu

 

Shaykh Rabiy’ Bin Haadiy Bin ‘Umayr Al-Madkhaliy

Imetafsiriwa Na: Naaswir Haamid

 

 

Shukrani zote zinamstahikia Allaah, Swalah na Salaam ziwe juu ya Mjumbe wa Allaah, Maswahaaba zake na wote waliofuata njia yake.

 

Hakika kwamba kile kinacholeta huzuni ni uharibifu wa pote la Rawaafidh ambao umepewa uwezo na nafasi nyingi za kuenea katika maeneo ya ardhi za Waislamu. Imekuja kwa hakika kuwa ni uenezi mkubwa na wale waliokuwepo nyuma ya mahubiri yake ni Watawala wa ardhi za Kipershia wa Ki-Iran, Ayaat wa Iraan na Mullah ambao ni maadui wa Uislamu, Ukweli, Tawhiyd na watu wake. Wanajipamba kwa mambo ya anasa na yenye thamani katika kueneza madhehebu haya ambayo yanaenda sambamba na juhudi nzito na malengo ya kutisha katika kuziteka ardhi zote za Waislamu.

 

Wanafanya haya kwa kutumia njia zao za uharibifu za Kiitikadi ambazo zimeegemezwa katika:

 

– Kufanya takfiyr (kumkufurisha Muislamu) kwa Maswahaba wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

- Kuikana Sunnah ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa sababu imefikishwa kupitia ukweli na ukweli wa Maswahaba wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

– Kuyaharibu maandiko ya Qur-aan na kutumia maandishi yanayohusisha Ukafiri na Wanafiki kwa Maswahaba wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

– Mbali zaidi ni kutumia maandishi ambayo yanataja tishio la Moto kwa Maswahaba wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), haswa kwa Abu Bakr na ‘Umar (Radhiya Allaahu ‘anhuma)

 

– Kutumia Aayah za kuwatukuza na kuwaahidi kutoka kwa Allaah kwao wenyewe na kwa Watu wa nyumba ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Hata hivyo, Allaah Ameshauacha huru ukoo wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kutokana na pote lenye msimamo muovu wa Rawaafidh na kanuni zao za kutoamini ambazo zimeegemezwa juu ya upotofu.

 

Kutokana na upotofu wao ambao unatumia Aayah za Tawhiyd za Allaah ambazo zinaonesha kumuabudia Yeye pekee – kama yale matamko ya Allaah:

 

Na Allaah Amesemea: “Msifanye waungu wawili; hakika Yeye ni Mola Mmoja tu: Basi Niogopeni Mimi tu.” [An-Nahl: 51].

 

Ni kwa namna gani wameharibu maandiko ya Qur-aan? Yeyote anayetaka kujua ukweli wa dini yao basi asome vyanzo vyao vikuu kama vile ‘al-Kaafi’ cha al-Kullayni, Tafsiyr al-Qummi na Tafsiyr al-‘Ayaashi, ambavyo vimekwenda mbali zaidi ya Mayahudi na Wakristo katika mnasaba wa uharibifu!

 

Kwa yale ambayo yanaujaza moyo kwa huzuni ni kwamba kufuru hii, uharibifu huu mbaya wa pote hili umeanza kuenezwa katika ardhi za Waislamu. Kwa hakika, tumesoma na kusikia kwamba idadi ya watu inaingia katika dini ya Raafidhah (Mashia). Idadi kubwa kati yao inasoma ndani ya miji ya Kiraafidhah inayoitwa Qum, ingawa kuna upinzani juu ya hili kutoka serikalini na kutoka kwa baadhi ya wanazuoni, hata hivyo pinzani zao ni dhaifu. Ni wapi mahitaji yao kuhusiana na Uislamu na Tawhiyd?!

 

Na ni wapi umuhimu wa Qur-aan na Sunnah? Uwapi umuhimu wa Maswahaba wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)?! Enyi Waislamu – serikali na watu – kwa hakika ukaaji wenu kimya kuhusiana na uenezi wa harakati hizi na pote hili – na ninaapa kwa Allaah – yana athari mbaya mno katika mahusiano ya Diyn yenu, dunia yenu, siasa zenu na Aakhirah yenu pale mtakapokutana na Mola wenu, kwa sababu mumekaa kimya kuhusiana na uovu mbaya mno na hatari mbaya sana juu ya Diyn yenu na masuala yenu ya Diyn.

 

Ninamuomba Allaah Aziamshe hisia za Waislamu na akili zao ili kupambana na hatari hii iangamizayo. Njia moja muhimu kwa yale wanayopambana nayo ni kukaa mbali na tovuti zao, ambazo zinahamasisha na kueneza uovu na ukafiri mkuu.

 

Ubainifu wa baadhi ya Kanuni za Maraafidhah (Shia):

 

1. Kwa mujibu wa kanuni zao ni kuwakufurisha Maswahaba na kuwavamia. Hii ni aina ya uharibifu wa Uislamu, ambao haujapata kuonekana isipokuwa ni kuleta uharibifu. Hii ndio sababu ya kujaribu kufikisha takfiyr hii katika namna bora wanayoiweza.

 

2. Kwa mujibu wa kanuni zao ni kwamba Imaam anatokana na misingi mikuu yao ya dini, ambao ni kuchupa mipaka kwao. Misingi ya Diyn imeelezwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Uimamu huo haupo.

 

3. Kwa mujibu wao, kuwafahamu Maimamu kumi na mbili ni kutokana na misingi mikuu ya dini na yeyote asiyekubali Maimamu kumi na mbili basi wanamhesabu kuwa ni Kafiri.

 

4. Maimamu kwa uoni wao, hawakosei (wamehifadhiwa kutokana na dhambi) na wanahifadhiwa kutokana na makosa na kusahau. Wanawatukuza na kuwafadhilisha kuliko Wajumbe na Mitume ('Alayhis Salaam Ajma’iyn).

 

5. Wanaamini kwamba Maimamu wao wanaona Yasiyoonekana (wanajua ghayb) na kwamba wanamiliki na kuratibu kila chembe ndogo atomu ndani ya ulimwengu. Hili ni kutokana na matendo yao makuu ya kutoamini, kwani wamewafanya Maimamu wao washiriki wa Allaah kuhusiana na ‘ilmu ya ghayb na kuratibu ulimwengu.

 

6. Wanadai kwa uongo kwamba Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) – alimtawaza ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) kuwa ni Khaliyfah. Wanadai kwamba Maswahaba walitumia nguvu na uharamia kukwapua Ukhaliyfah dhidi yake. Dai hili ni dai kubwa la uongo na ni msingi wa upotofu wao na uhaini wao dhidi ya Maswahaba, kuwakufurisha na kuwalaani.

 

7. Kutokana na upotofu na ngano (hadithi) zao ni kwamba Mahdi (wanayedai ni yule kutoka katika ukoo wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam)) ndiye wanayemsubiri na kwamba amekuwemo ndani ya pango kwa zaidi ya miaka 1200 ambaye wanadai kuwa ni Imaam wa kumi na mbili. Ukweli ni kwamba, Imaam huyu hayupo kabisa, Mahdi huyu wala hajaumbwa. Mahdi ambaye Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amemtaja ni wa kweli, hata hivyo, sie Mahdi ambaye wanadai Maraafidhah (Mashia). Kutokana na ngano zao ni kwamba Muwsaa bin Ja’far (amefariki mwaka 184H) ambaye Maraafidhah wanadai kuwa ni mmoja wa Maimamu – amesema kwa mtu katika kipindi chake: ‘Iwapo utaishi basi utakutana naye.’ Tokea hapo, miaka 1249 imepita na bado hawajakutana naye. Huu ni ushahidi kwamba huu ulikuwa ni uongo na tuhuma dhidi ya Muwsaa.

 

8. Kutokana na misingi yao ni kuwa na Iymaan (imani) kwamba mtu anarejeshwa tena maishani baada ya kufa na kwamba, kwa mujibu wa dini yao, yeyote asiyeamini hili ni Kafiri. Al-Aluwsiy amesema ndani ya ‘Mukhtaswar at-Tuhfah al-Ithnaa ‘Aashariyyah.’ [uk. 200-201]:

 

‘Madhehebu ya Ahlus-Sunnah ni kwamba aliyefariki harejei maisha ya duniani kabla ya Siku ya Hukumu. Madhehebu ya Imaamiyyah (Ithnaa ‘Ashariyyah) na baadhi ya madhehebu mengine ya Maraafidhah (Kishia) wote yanasema kwamba baadhi ya waliofariki watarejea.

 

Wanadai kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na yule aliyemrithi (wakimaanisha kuwa ni ‘Aliy), watukufu wakuu (Hasan na Husayn), pamoja na maadui zao – wakimaanisha kuwa watatu, Mu’aawiyah, Yaziyd, Haaruwn, Ibn Ziyaad na mfano wa hao – na Maimamu wengine na watu wao ambao waliuliwa wote watarudishwa maishani baada ya kutokea Mahdi na wao (yaani Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ‘Aliy, na Hasan na Husayn) watamtia adabu kila mmoja ambaye aliwaadhibisha Maimamu wao na watalipiza kisasi kutokana nao, kabla ya kuwasili Dajjaal, kisha watakufa wakisubiri hukumu katika Siku ya Hukumu.’ Tunamuomba Allaah Awaangamize Maraafidhah.

 

9. Kutokana na misingi yao ya imani ni dai dhidi ya Maswahaba kwamba wameiharibu Qur-aan. Allah Amewazuia hao Maswahaba wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) – Mola Awe Radhi nao – kuharibu hata neno moja kutoka katika Kitabu cha Allaah. Isipokuwa, wale waliokiharibu kwa uhakika ni Rawaafidh. Ni mara ngapi wameharibu maandishi ya Qur-aan na maana zake? Uharibifu wao mwingi ni kuhusiana na Aaayah za ahadi za Allaah na tahadhari Zake na Aayah zinazohusiana na Ukafiri na Wanafiki, ambazo wanazitumia kwa Maswahaba wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) – hali ya kuwa ni Maraafidhah ambao ndio wanaostahikia kutumiliwa Aayah hizi kwao wao.

 

10. Katika misingi yao mikuu ni Taqiyyah (kusema uongo katika kulinda upotofu wao). Wanaitakidi kuwa ni tisa ya kumi ya dini yao na yeyote asiyekuwa na Taqiyyah hana dini. Wanalithibitisha suala hili kwa maneno ya Abu Ja’far ambaye amesema: ‘Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) ametusisitiza sisi kuwa na Taqiyyah.’ Pia wamesema kwamba: ‘Taqiyyah inatokana na dini yangu na dini ya mababa zangu na yeyote asiyekuwa na Taqiyyah hana imani.’  [Angalia al-Kaafi cha al-Kullayniy 2/217-218].

 

11. Katika dini yao ni kujengea juu ya makaburi, haswa kwa Maimamu wao, na kufanya Twawaaf juu yake na kuomba msaada maiti waliomo kaburini. Wanatoa pesa nyingi kwa ajili ya maiti zao na kulipa viapo na kafara katika milango ya majengo haya ya makaburi. Hizi ni aina kuu za shirki.

 

12. Katika masuala muhimu ya dini yao ni ndoa ya muda (Mut’ah) – ambayo Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameifanya kuwa na umuhimu mahsusi pale tu ilipokuwa na haja na dharura maalumu. Hata hivyo, suala hili baadaye lilifutwa na Allaah kwa ulimi wa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Miongoni mwa msimuliaji wa uharamu wa ndoa ya muda alikuwa ni ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu) mwenyewe.

 

Mashia wameifanya ndoa ya muda kuruhusika na kusimulia juu yake kwa ili inayoitwa ‘hadiyth’ inayoonesha sifa zake, kitu ambacho Shari’ah na watu wenye ‘ilmu wameikataa. Kwa mfano, wanasema: ‘Yeyote anayejitosheleza shahawa zake kwa mwanamke muumini [aliyemo ndani ya ndoa ya muda (mut’ah)] basi ni kama kwamba amezuru Ka’bah mara 70.’

 

Wanasema: ‘Wasimulizi waaminifu walioipokea ni as-Swaadiq ('Alayhis Salaam) anayesema: ‘Hakika ndoa ya muda (Mut’ah) inatokana na dini yangu na dini ya mababa zangu. Yeyote anayeifuata basi ameihuisha dini yetu, yeyote anayeikataa basi ameikataa dini yetu na ameamini vinginevyo visivyokuwa dini yetu.’

 

Ndoa ya muda kwa mfumo huu, kwa mujibu wa wao, ni kutokana na misingi mikuu hata kama iwapo mtu ataiacha, itatambuliwa kama ni Kufuru.

 

Kuna baadhi ya simulizi kutokana nao kuhusiana na hili, kwa mfano: ‘Yeyote anayeitekeleza ndoa ya muda mara moja, basi hadhi yake itakuwa kama hadhi ya al-Husayn ('Alayhis Salaam). Yeyote anayeitekeleza ndoa ya muda mara mbili, basi hadhi yake itakuwa kama ya al-Hasan ('Alayhis Salaam). Yeyote anayeitekeleza ndoa ya muda mara tatu, basi hadhi yake itakuwa kama hadhi ya ‘Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu). Yeyote anayetekeleza ndoa ya muda mara nne, basi hadhi yake itakuwa kama hadhi yangu.’

 

Tamko lao hili la kusema ('Alayhis Salaam) ni kutokana na matamshi yao wanayotumia wao, lakini ukweli matumizi ya kusema baada ya kuwataja Maswahaba ni kusema (Radhiya Allaahu ‘anhu) au (Rahimahu Allaah) kwa Taabi’iy (waliowafuata Maswahaba) na wale baada yao. Na si kusema (‘Alayhis Salaam).

 

Huu ni muhtasari mfupi ndani ya dini ya Maraafidhah ingawa ukafiri wao na upotofu wao unajaza idadi nyingi za vitabu.

 

 

Imeandikwa na:

 

Rabiy' bin Haadiy ‘Umayr al-Madkhaliy

 

21/Jumaadal-Akhirah/1432 H.

 

 

 

 

Share