03-Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd: Tawhiyd Ni Fitwrah (Maumbile Asili Ya Mwana Aadam)

 

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

03-Tawhiyd Ni Fitwrah (Maumbile Asili Ya Mwana Aadam)

 

 

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:

 

فَأَقِمْ وَجْهَكَ لِلدِّينِ حَنِيفًا ۚ فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا ۚ لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٣٠﴾

Basi elekeza uso wako kwenye Dini yenye kujiengua na upotofu inayoelemea haki. Umbile la asili la kumpwekesha Allaah Aliyowaumbia watu. Hakuna mabadiliko katika uumbaji wa Allaah. Hivyo ndio Dini iliyonyooka sawasawa, lakini watu wengi hawajui.  [Ar-Ruwm: 30]

 

Na Hadiyth ya Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ أَنَّهُ كَانَ يَقُولُ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((مَا مِنْ مَوْلُودٍ إِلَّا يُولَدُ عَلَى الْفِطْرَةِ  فَأَبَوَاهُ يُهَوِّدَانِهِ ، وَيُنَصِّرَانِهِ  وَيُمَجِّسَانِهِ  كَمَا تُنْتَجُ  الْبَهِيمَةُ بَهِيمَةً جَمْعَاءَ ، هَلْ تُحِسُّونَ فِيهَا مِنْ جَدْعَاءَ؟)) ثُمَّ يَقُولُ أَبُو هُرَيْرَةَ:  وَاقْرَءُوا إِنْ شِئْتُمْ: ((فِطْرَتَ اللَّـهِ الَّتِي فَطَرَ النَّاسَ عَلَيْهَا ۚ لَا تَبْدِيلَ لِخَلْقِ اللَّـهِ))  

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba alikuwa akisema: Rasuli  wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  amesema; ((Hakuna kizazi kinachozaliwa (mtoto mchanga) isipokuwa anazaliwa katika 'fitwrah' kisha wazazi wake (humbadilisha na) humuingiza katika dini ya Uyahudi, au Unaswaara au Umajusi, kama mfano mnyama mwenye pembe  anavyomzaa mnyama mwenye pembe kama yeye, je, mtahisi kuwa hana pembe?   Kisha Abuu Hurayrah akasema: Someni mkipenda: (kauli ya Allaah):  ((Umbile la asili la kumpwekesha Allaah Aliyowaumbia watu. Hakuna mabadiliko katika uumbaji wa Allaah))  [Al-Bukhaariy na Muslim]     

 

 

 

Share