09-Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd: Aina Zote Tatu za Tawhiyd Zinaafikiana, Haiwezekani Kukosekana mojawapo

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

09-Aina Zote Tatu za Tawhiyd Zinaafikiana, Haiwezwkani Kukosekana Mojawapo

 

 

 

Aina zote Tatu za Tawhiyd zinaafikiana. Kutokuamini mojawapo humtoa mtu nje ya Uislamu kwa sababu makafiri Quraysh waliamini Tawhiydur-Rubuwbiyyah wakakanusha ya Uluwhiyyah. Waliamini kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ndiye Muumba wao, na Ndiye Muumba wa mbingu na ardhi, Ndiye Anayendesha mambo yote, Ndiye Anayewaruzku, Na Ndiye Anayeteremsha mvua n.k. Dalili kadhaa katika Qur-aan:

 

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَهُمْ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ﴿٨٧﴾

Na ukiwauliza: Ni nani kawaumba? Bila shaka watasema: “Allaah.”  Basi vipi wanaghilibiwa?  [Az-Zukhruf: 87]

 

Na pia:

 

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۚ قُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿٢٥﴾

Na ukiwauliza: “Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi?” bila shaka watasema: “Allaah.” Sema: “AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah).” Bali wengi wao hawajui.   [Luqmaan: 25]

 

Na pia:

 

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۚ قُلْ أَفَرَأَيْتُم مَّا تَدْعُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ إِنْ أَرَادَنِيَ اللَّـهُ بِضُرٍّ هَلْ هُنَّ كَاشِفَاتُ ضُرِّهِ أَوْ أَرَادَنِي بِرَحْمَةٍ هَلْ هُنَّ مُمْسِكَاتُ رَحْمَتِهِ ۚ قُلْ حَسْبِيَ اللَّـهُ ۖ عَلَيْهِ يَتَوَكَّلُ الْمُتَوَكِّلُونَ﴿٣٨﴾

Na ukiwauliza: “Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi?” Bila shaka watasema: “Allaah.” Sema: “Je, mnaonaje wale mnaowaomba badala ya Allaah; ikiwa Allaah Atanikusudia dhara; je, wao wataweza kuondosha dhara Yake? Au Akinikusudia rahmah; je wao wataweza kuizuia rahmah Yake?” Sema: “Ananitosheleza Allaah”, Kwake watawakali wenye kutawakali. [Az-Zumar: 38]

 

Na pia:

 

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّنْ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۖ فَأَنَّىٰ يُؤْفَكُونَ ﴿٦١﴾

Na ukiwauliza: “Ni nani aliyeumba mbingu na ardhi, na akatiisha jua na mwezi?” Bila shaka watasema: “Allaah.” Basi vipi wanavyoghilibiwa?

 

اللَّـهُ يَبْسُطُ الرِّزْقَ لِمَن يَشَاءُ مِنْ عِبَادِهِ وَيَقْدِرُ لَهُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿٦٢﴾

Allaah Humkunjulia na Humdhikishia riziki Amtakaye katika waja Wake. Hakika Allaah kwa kila kitu ni Mjuzi.

 

 

وَلَئِن سَأَلْتَهُم مَّن نَّزَّلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَأَحْيَا بِهِ الْأَرْضَ مِن بَعْدِ مَوْتِهَا لَيَقُولُنَّ اللَّـهُ ۚ قُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ ۚ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يَعْقِلُونَ ﴿٦٣﴾

Na ukiwauliza: “Ni nani Ateremshaye maji kutoka mbinguni, Akahuisha kwayo ardhi baada ya kufa kwake?” Bila shaka watasema: “Allaah”.  Sema: “AlhamduliLLaah, Himidi Anastahiki Allaah.” Bali wengi wao hawatii akilini.   [Al-‘Ankabuwt: 61 -63]

 

Na pia:

 

قُلْ مَن يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ أَمَّن يَمْلِكُ السَّمْعَ وَالْأَبْصَارَ وَمَن يُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَيُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ وَمَن يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۚ فَسَيَقُولُونَ اللَّـهُ ۚ فَقُلْ أَفَلَا تَتَّقُونَ﴿٣١﴾

Sema: “Nani anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhini. Au nani anayemiliki kusikia na kuona; na nani anayemtoa aliye hai kutoka mfu, na anayemtoa mfu kutoka aliye uhai; na nani anayeendesha mambo (yote)?”  Watasema: “Ni Allaah”; basi sema: “Je basi hamuwi na taqwa?”   [Yuwnus: 31]

 

Lakini walimshirikisha katika ‘ibaadah zao wakidai kuwa walivyokuwa wakiviabudu vinawakaribisha kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَالَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءَ مَا نَعْبُدُهُمْ إِلَّا لِيُقَرِّبُونَا إِلَى اللَّـهِ زُلْفَىٰ إِنَّ اللَّـهَ يَحْكُمُ بَيْنَهُمْ فِي مَا هُمْ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ ۗ إِنَّ اللَّـهَ لَا يَهْدِي مَنْ هُوَ كَاذِبٌ كَفَّارٌ ﴿٣﴾

na wale waliojichukulia badala Yake walinzi (wakisema): “Hatuwaabudu isipokuwa ili wapate kutukurubisha kwa Allaah tumkaribie” Hakika Allaah Atahukumu baina yao katika yale waliyokhitilafiana nayo. Hakika Allaah Hamwongoi aliye muongo, kafiri.  [Az-Zumar: 3]

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Akathibitisha tena kwamba Yeye Ndiye wa kuabudiwa katika Rubuwbiyyah Yake (Uola, umiliki, uendeshaji wa ulimwengu, uumbaji, utoaji rizki, uhuishaji na ufishaji, n.k.)  na Uluwhiyyah Yake (‘ibaadah): 

 

اللَّـهُ الَّذِي جَعَلَ لَكُمُ الْأَرْضَ قَرَارًا وَالسَّمَاءَ بِنَاءً وَصَوَّرَكُمْ فَأَحْسَنَ صُوَرَكُمْ وَرَزَقَكُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ ۖ فَتَبَارَكَ اللَّـهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ﴿٦٤﴾

Allaah Ambaye Amekufanyieni ardhi kuwa mahali pa makazi, na mbingu kama ni paa na Akakutieni sura, Akazifanya nzuri zaidi sura zenu, na Akakuruzukuni katika vizuri. Huyo Ndiye Allaah Rabb wenu. Basi Tabaaraka-Allaah, Amebarikika Allaah Rabb wa walimwengu.

 

هُوَ الْحَيُّ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ فَادْعُوهُ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ ۗ الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴿٦٥﴾

Yeye Ndiye Aliye hai daima hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye; basi muombeni Yeye wenye kumtakasia Dini. AlhamduliLLaah, Himidi Anastahiki Allaah Rabb wa walimwengu.   [Ghaafir: 64- 65]

 

 Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۖ أَنَّىٰ يَكُونُ لَهُ وَلَدٌ وَلَمْ تَكُن لَّهُ صَاحِبَةٌ ۖ وَخَلَقَ كُلَّ شَيْءٍ ۖ وَهُوَ بِكُلِّ شَيْءٍ عَلِيمٌ ﴿١٠١﴾

Mwanzilishi wa mbingu na ardhi. Inamkinikaje kuwa Yeye Ana mwana na hali hana mke! Naye Ameumba kila kitu, Naye kwa kila kitu ni Mjuzi.

 

 

 

ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ فَاعْبُدُوهُ ۚ وَهُوَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ وَكِيلٌ ﴿١٠٢﴾

Huyo kwenu Ndiye Allaah, Rabb wenu. Hapana muabudiwa wa haki ila Yeye Muumbaji wa kila kitu, basi mwabuduni Yeye Pekee. Naye juu ya kila kitu ni Mdhamini Anayetegemewa kwa yote.  [Al-An’aam: 101-102]

 

Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ خَالِقُ كُلِّ شَيْءٍ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ﴿٦٢﴾

Huyo Ndiye Allaah Rabb wenu, Muumba wa kila kitu, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye; basi vipi mnaghilibiwa?  [Ghaafir: 62]

 

 Na pia:

 

خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ بِالْحَقِّ ۖ يُكَوِّرُ اللَّيْلَ عَلَى النَّهَارِ وَيُكَوِّرُ النَّهَارَ عَلَى اللَّيْلِ ۖ وَسَخَّرَ الشَّمْسَ وَالْقَمَرَ ۖ كُلٌّ يَجْرِي لِأَجَلٍ مُّسَمًّى ۗ أَلَا هُوَ الْعَزِيزُ الْغَفَّارُ ﴿٥﴾

Ameumba mbingu na ardhi kwa haki, Anaufunika usiku juu ya mchana, na Anafunika mchana juu ya usiku, na Anatiisha jua na mwezi; kila kimoja kinakwenda mpaka muda maalumu uliokadiriwa. Tanabahi! Yeye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwingi wa kughufuria.

 

 

خَلَقَكُم مِّن نَّفْسٍ وَاحِدَةٍ ثُمَّ جَعَلَ مِنْهَا زَوْجَهَا وَأَنزَلَ لَكُم مِّنَ الْأَنْعَامِ ثَمَانِيَةَ أَزْوَاجٍ ۚ يَخْلُقُكُمْ فِي بُطُونِ أُمَّهَاتِكُمْ خَلْقًا مِّن بَعْدِ خَلْقٍ فِي ظُلُمَاتٍ ثَلَاثٍ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ لَهُ الْمُلْكُ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُصْرَفُونَ ﴿٦﴾

Amekuumbeni kutokana na nafsi moja, kisha Akamfanya humo mkewe na Akakuteremshieni katika wanyama wa mifugo jozi nane. Anakuumbeni matumboni mwa mama zenu umbo baada ya umbo, katika viza vitatu. Huyo Ndiye Rabb wenu Ana ufalme, hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye, basi vipi mnageuzwa?   [Az-Zmuar 5 – 6]

 

Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

يَا أَيُّهَا النَّاسُ اذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ ۚ هَلْ مِنْ خَالِقٍ غَيْرُ اللَّـهِ يَرْزُقُكُم مِّنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ فَأَنَّىٰ تُؤْفَكُونَ ﴿٣﴾

Enyi watu! Kumbukeni neema za Allaah kwenu. Je, kuna muumbaji yeyote badala ya Allaah Anayekuruzukuni kutoka mbinguni na ardhi? Hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, basi wapi mnapogeuzwa? [Faatwir: 3]

 

Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

أَفَحَسِبْتُمْ أَنَّمَا خَلَقْنَاكُمْ عَبَثًا وَأَنَّكُمْ إِلَيْنَا لَا تُرْجَعُونَ ﴿١١٥﴾

 “Je, mlidhania kwamba Sisi Tulikuumbeni bila kusudio mcheze tu na kwamba nyinyi Kwetu hamtorejeshwa?”

 

 

فَتَعَالَى اللَّـهُ الْمَلِكُ الْحَقُّ ۖ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ رَبُّ الْعَرْشِ الْكَرِيمِ ﴿١١٦﴾

Basi Ametukuka Allaah Mfalme wa hak). Hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye. Rabb wa ‘Arsh tukufu.

 

وَمَن يَدْعُ مَعَ اللَّـهِ إِلَـٰهًا آخَرَ لَا بُرْهَانَ لَهُ بِهِ فَإِنَّمَا حِسَابُهُ عِندَ رَبِّهِ ۚ إِنَّهُ لَا يُفْلِحُ الْكَافِرُونَ ﴿١١٧﴾

Na yeyote yule anayeomba du’aa (au kuabudu) pamoja na Allaah muabudiwa mwengine hana ushahidi wa wazi wa hilo; basi hakika hesabu yake iko kwa Rabb wake. Hakika hawafaulu makafiri.   [Al-Muuminuwn: 115-117]

 

Na pia Anasema (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

رَبِّ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَمَا بَيْنَهُمَا ۖ إِن كُنتُم مُّوقِنِينَ﴿٧﴾

Rabb wa mbingu na ardhi na vilivyo baina yake, mkiwa ni wenye yakini.

 

لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۖ رَبُّكُمْ وَرَبُّ آبَائِكُمُ الْأَوَّلِينَ﴿٨﴾

Hapana muabudiwa wa haki ila Yeye, Anahuisha na Anafisha; Rabb wenu na Rabb wa baba zenu wa awali. [Ad-Dukhaan: 7- 8]

 

Na Anasema pia Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

إِنَّ رَبَّكُمُ اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۖ يُدَبِّرُ الْأَمْرَ ۖ مَا مِن شَفِيعٍ إِلَّا مِن بَعْدِ إِذْنِهِ ۚ ذَٰلِكُمُ اللَّـهُ رَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۚ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ﴿٣﴾

  Hakika Rabb wenu ni Allaah Ambaye Ameumba mbingu na ardhi katika siku sita, kisha Istawaa juu ya ‘Arsh. Anaendesha mambo yote. Hakuna mwombezi yeyote ila baada ya idhini Yake. Huyu Ndiye Allaah Rabb Wenu, basi mwabuduni. Je, hamkumbuki?   [Yuwnus: 3]

 

Anathibitisha pia kuhusu Tawhiyd Yake ya Asmaa na Swifaat kwamba inaafikiana na Tawhiyd ya Rubuwbiyyah na Uluwhiyyah:

 

 

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ ۖ لَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ﴿٨﴾

Allaah, hapana hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye. Anayo Majina Mazuri kabisa.  [Twaahaa: 8]

 

Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

وَإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَاحِدٌ ۖ لَّا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الرَّحْمَـٰنُ الرَّحِيمُ ﴿١٦٣﴾

Na Ilaah wenu (Allaah) ni Ilaah Mmoja, hapana Muabudiwa wa haki ila Yeye, Ar-Rahmaan, Mwenye kurehemu.  [Al-Baqarah: 163]

 

 

Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta’aalaa)

 

إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْقَصَصُ الْحَقُّ ۚ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا اللَّـهُ ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٦٢﴾

Hakika haya ni masimulizi ya haki. Na hapana Muabudiwa wa haki ila Allaah. Na hakika Allaah Yeye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Aal-‘Imraan: 62]

 

Kuwa na ujuzi wa Tawhiyd ya Asmaa wasw-Swifaat (Majina na Sifa za Allaah) utamtambua Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) vizuri kabisa na hutokuwa mwenye kukanusha, na itakuepusha na kupotoa maana ya Majina na Sifa Zake na kuzibadilisha maana au kumfananisha na viumbe vyenginevyo. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

 

قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ

  Sema; “Muiteni Allaah au muiteni Ar-Rahmaan, vyovyote mtakavyomwita basi Yeye Ana Majina Mazuri kabisa.    [Al-Israa: 110]

 

Na Anasema pia (Subhaanahu wa Ta’aalaa):

 

الَّذِي خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ وَمَا بَيْنَهُمَا فِي سِتَّةِ أَيَّامٍ ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ ۚ الرَّحْمَـٰنُ فَاسْأَلْ بِهِ خَبِيرًا ﴿٥٩﴾

Ambaye Ameumba mbingu na ardhi na vilivyo baina yake katika siku sita, kisha Istawaa juu ya ‘Arsh Ar-Rahmaan, basi ulizia kuhusu Yeye; kwani ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika.

 

وَإِذَا قِيلَ لَهُمُ اسْجُدُوا لِلرَّحْمَـٰنِ قَالُوا وَمَا الرَّحْمَـٰنُ أَنَسْجُدُ لِمَا تَأْمُرُنَا وَزَادَهُمْ نُفُورًا ۩﴿٦٠﴾

Na wanapoambiwa: “Msujudieni Ar-Rahmaan” husema: “Ni nani huyo Ar-Rahmaan? Tumsujudie unayetuamrisha, na inawazidishia kukengeuka kwa chuki.  [Al-Furqaan: 59 – 60]

 

Na pia:

 

كَذَٰلِكَ أَرْسَلْنَاكَ فِي أُمَّةٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهَا أُمَمٌ لِّتَتْلُوَ عَلَيْهِمُ الَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ وَهُمْ يَكْفُرُونَ بِالرَّحْمَـٰنِ ۚ قُلْ هُوَ رَبِّي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ مَتَابِ ﴿٣٠﴾

Hivyo ndivyo Tumekutuma katika Ummah uliokwishapita kabla yake umati nyingine ili uwasomee yale Tuliyokufunulia Wahy; nao wanamkufuru Ar-Rahmaan. Sema: “Yeye Ndiye Rabb wangu, hapana muabudiwa wa haki ila Yeye, Kwake natawakali na Kwake ni mahali pangu pa kurejea kutubu.”   [Ar-Ra’d: 30]

 

Share