22-Umuhimu Wa Tawhiyd Na Fadhila Zake: Tawhyd Ni Sharti Ya Kuingia Jannah

 

Umuhimu Na Fadhila Za Tawhiyd

 

22-Tawhyd Ni Sharti Ya Kuingia Jannah

 

 

 

Dalili zifuatazo zimetaja kuwa: Laa ilaaha illa Allaah ni sharti ya kuingia Jannah:

 

Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

((لاَيَدْخُلُ الْجَنَّةَ إِلا نَفْسٌ مُؤْمِنَةٌ))

((Hatoingia Jannah isipokuwa nafsi iliyoamini))

 

Na Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Anathibitisha kwamba kutenda mema pekee hamitoshi mtu kuingia Jannah, bali mpaka mtu awe mwenye kuamini. Na Tawhiyd ni msingi wa iymaan:

 

 وَمَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَأُولَـٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ يُرْزَقُونَ فِيهَا بِغَيْرِ حِسَابٍ﴿٤٠﴾

Na yeyote atakayetenda mema kati ya mwanamume au mwanamke, naye ni Muumini, basi hao wataingia Jannah wataruzukiwa humo bila ya hesabu. [Ghaafir: 40]

 

Pia Hadiyth ya ‘Ubaadah bin Asw-Swaamit (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

 

((مَنْ شَهِدَ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ وَأَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ وَأَنَّ عِيسَى عَبْدُ اللَّهِ وَرَسُولُهُ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَى مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِنْهُ وَالْجَنَّةُ حَقٌّ وَالنَّارُ حَقٌّ أَدْخَلَهُ اللَّهُ الْجَنَّةَ عَلَى مَا كَانَ مِنْ الْعَمَلِ))

((Atakayeshuhudia moyoni na kukiri kwamba: laa ilaaha illa Allaah  (hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah), na kwamba ‘Iysaa ni mja wa Allaah na Rasuli Wake, na neno Lake Alilompelekea Maryam na Ruwh kutoka Kwake, na kwamba Jannah ni haki, na Moto ni haki, Allaah Atamuingiza Jannah kwa ‘amali zozote alizonazo)). [Al-Bukhaariy (3/1267) (3252), Muslim (1/57) (28) Ahmad (5/313) (22727), Ibn Hibbaan (1/431) (202), An-Nasaaiy (6/331) (11132)]

 

Na Hadiyth ya Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) kwamba Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alisema:

 

((يَا أَبَا هُرَيْرَةَ (وَأَعْطَانِي نَعْلَيْهِ) قَالَ: اذْهَبْ بِنَعْلَيّ هَاتَينِ فَمَنْ لَقِيتَ مِنْ وَرَاء هَذَا الْحَائِطِ يَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاّ اللّهُ مُسْتَيْقِنا بِهَا قَلُبُهُ فَبَشّرْهُ بِالْجَنّةِ))

((Ee Abaa Hurayrah (akanipa viatu vyake) Nenda na viatu vyangu hivi, utakayemkuta nyuma ya ukuta huu akiwa anakiri moyoni na anashuhudia kwamba: laa ilaaha illa Allaah (hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah) akiwa amethibitika nayo moyoni, mbashirie Jannah)). [Muslim]

 

 

Na Hadiyth ya ‘Uthmaan bin ‘Affaan (Radhwiya Allaahu ‘anhu) Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:

 

((مَنْ مَاتَ وَهُوَ يَعْلَمُ أَنَّهُ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ دَخَلَ الْجَنَّة))

((Atakayefariki akiwa anajua kwamba: laa ilaaha illa Allaah (hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah) ataingia Jannah)). [Muslim]

 

 

Share