Imaam 'Abdul-Kariym Al-Jazariy - Mja Mwema Hafanyi Mijadala

Mja Mwema Hafanyi Mijadala

www.alhidaaya.com

 

Imaam 'Abdul-Kariym Al-Jazariy amesema:

 

"Mchaji Allaah hafanyi mijadala."

 

[Ash-Shu'ab, 8129]

 

Haytham bin Jamiyl aliulizwa: "Mtu ana ujuzi wa mas-alah ya Sunnah, je, anaweza kufanya mijadala au malumbano katika fani hiyo?" Akajibu: "Hapana, bali anapaswa kuwajulisha watu waijue Sunnah, na wakiipokea kutoka kwake ni vizuri, la wasipoipokea, basi anyamaze (asilumbane)."

 

[Jaami' Al-Bayaan Al-'Ilm Wa Fadhwlihi, 4/94]
 

 

Share