Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah - Usiwe Na Kasumba Na Imaam Au Shaykh Fulani

Usiwe Na Kasumba Na Imaam Fulani Au Shaykh Fulani
Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah
 
 
 
Shaykh Al-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
 
"Na mwenye Kuta'asswabu (kuwa na kasumba) na Mmoja kwa Dhati yake katika Ma-Imaam na akawaacha wengine,
basi mtu huyo atakuwa kwenye manzilah ya yule mwenye Kuta'asswabu na Mmoja katika Maswahaba bila wengine.
 
Mtu huyo atakuwa ni kama Raafidhwiy (Shia) ambae anata'asswab na 'Aliy bila (akawaacha) Makhalifa Watatu (wengine) na Jumhuur ya Maswahaba wengine.
 
Mtu huyo atakuwa ni kama Khaarijiy ambaye anamfanyia twa'ani (anamponda) 'Uthmaan na 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhumaa).
 
Basi hizi ni njia za watu wa bid'ah na matamanio ambao zimethibiti hoja za Kitabu na Sunnah na Ijmaa' kuwa wamekemewa,
wametoka nje ya shariy'ah na mfumo (Manhaj) ambayo ametumwa nayo Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wasallam).
 
Kwa hiyo, atakaye ta'aswab na yeyote katika Ma-Imaam kwa Dhati yake basi atakuwa amefanana na hao (waliotajwa).
 
Ni sawa sawa ata'aswabu kwa Maalik au kwa Ash-Shaafi'iy au kwa Abuw Haniyfah au kwa Ahmad au wengineo.
 
Kisha upeo wa mwenye kuta'asswabu kwa mmoja kati ya hao anakuwa ni mjinga wa kiwango chake cha  elimu na Dini, na kiwango cha wengineo pia, anakuwa ni mjinga na dhalimu, na Allaah Anaamrisha watu kushikamana na elimu na uadilifu, na Anakataza ujinga na dhulma.
 
 
[Majmuw' Al-Fataawaa, juz. 2, uk. 252]
 
Share