Skip navigation.
Home kabah

Du'aa Ya Kunywa Maziwa

SWALI:

Which dua was (the Prophet)  saying before drinking milk.  Only Milk not other drinks like water or juices.  Please advise.

''Swali hili limekuja kwa lugha ya Kingereza  nasi tunaliwacha hivyo lilivyo, lakini jibu litakuwa  kwa kiswahili Insha-Allaah'' 

 

 


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho


Mtume صلى الله عليه وآله وسلم  amefadhilisha kinywaji cha Maziwa na kasema mtu aombe dua ifuatayo baada ya kunywa maziwa:

 ((عن عبد الله بن عباس رضي الله عنهما: "من أطعمه الله طعامًا، فليقل: اللهم بارك لنا فيه، وأطعمنا خيرًا منه، ومن سقاه الله لبنًا فليقل: اللهم بارك لنا فيه، وزدنا منه، فإنه ليس شيء يجزئ من الطعام والشراب غير اللبن"))  رواه أحمد وأبو داودو قال الألبان حديث حسن

((Imetoka kwa Abdullahi Bin 'Abaas رضي الله عنهما:  "Atakayelishwa chakula kutoka kwa Allaah سبحانه وتعالى aseme "Ee Mola Mlezi Tubarikie nacho, na Utulishe (chakula) bora kuliko hiki";  Na atakayenyeshwa Maziwa  na Allaah سبحانه وتعالى   aseme, Ee Mola Mlezi Tubarikie nayo, na Tuzidishie"  kwani hakuna kitu kinachojazilia katika chakula na kinywaji isipokuwa Maziwa))  Ahmad, Abu Dawuud, na kasema Sheikh Albaani ni Hadithi Hassan.

Wa Allaahu A'alam