Kula Futari Kwa Kafiri
SWALI:
Hivi unaruhusiwa kula futari kwa kaafiri?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Sio futari peke yake bali vyakula vyote vilivyo halali kwetu tunaruhusiwa kula isipokuwa nyama ambazo zinachinjwa nao ikiwa si katika Ahlil Kitaab japokuwa washirikina na Ahlil Kitaab wote ni makafiri. Lakini ikiwa makafiri hao watakuwa wamenunua nyama iliyo halali kutoka kwa bucha inayojulikana kuwa ni halali unaweza kula bila ya tatizo lolote. Chakula cha futari na wakati mwengine kinakuwa sawasawa tu.
Na Allah Anajua Zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


