Shaykh Yahyaa Al-Hajuwriy - Hukmu Ya Kuwasomea Maiti Qur-aan

Hukmu Ya Kuwasomea Maiti Qur-aan

 

Shaykh Yahyaa Al-Hajuwriy (Hafidhwahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

Nini hukmu ya mwenye kusoma Al-Faatihah au chochote katika Qur-aan kuwasomea Maiti?

 

 

JIBU:

Hili ni jambo la kuzushwa. Hakulifanya Nabiy (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wasallam) wala Maswahaba zake (Ridhwaanu Allaahi ‘alayhim), hawakuwa wakiwasomea Maiti (Suwrat) Al-Faatihah, au Aayatul-Kursiy, au Al-Mu’awwidhatayn (Suwrat Al-Falaq na An-Naas), au Al-Ikhlaasw, au chochote katika Qur-aan.

 

Amesema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

“Mwenye kuzusha katika jambo letu (Dini yetu) hili ambalo halimo, basi hurudishwa (halipokelewi).”[Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Na amesema Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

“Hakika Allaah Kazuia tawbah ya mwenye kufanya bid’ah mpaka aache bid’ah yake.”

 

Inapasa (aache hilo na afanye) tawbah kwa kitendo hicho.

 

 

[As-ilah Min Ahlis-Sunnah Bil-Khushim, Bitaariykh: Laylat Ath-Thulathaa 21 Rabiy’ Al-Aakhir 1423 H]

 

 

 

Share