016-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Maamrisho Wa Kuzihifadhi Sunnah Na Adabu Zake

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب في الأمر بالمحافظة عَلَى السنة وآدابها

016 – Mlango Wa Maarisho Wa Kuzihifadhi Sunnah Na Adabu Zake

 

Alhidaaya.com

 

 

قَالَ الله تَعَالَى:

 

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ﴿٧﴾

Na lolote analokupeni Rasuli (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) basi lichukueni, na analokukatazeni, basi acheni. [Al-Hashr: 7]

 

 

وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ ﴿٣﴾

Na wala hatamki kwa hawaa.

إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ ﴿٤﴾

Hayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa. [An-Najm: 3-4]

 

 

 قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ﴿٣١﴾

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): “Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Atakupendeni Allaah na Atakughufurieni dhambi zenu. [Aal-‘Imraan: 31]

 

لَّقَدْ كَانَ لَكُمْ فِي رَسُولِ اللَّـهِ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ لِّمَن كَانَ يَرْجُو اللَّـهَ وَالْيَوْمَ الْآخِرَ وَذَكَرَ اللَّـهَ كَثِيرًا ﴿٢١﴾

Kwa yakini mna kigezo kizuri kwa Rasuli wa Allaah kwa mwenye kumtaraji Allaah na Siku ya Mwisho na akamdhukuru Allaah kwa wingi. [Al-Ahzaab: 21]

 

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا ﴿٦٥﴾

Basi Naapa kwa Rabb wako, hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni mwamuzi katika yale wanayozozana baina yao, kisha wasipate katika nyoyo zao karaha katika yale uliyohukumu na wajisalimishe, kwa kujisalimisha (kikamilifu). [An-Nisaa: 65]

 

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ ﴿٥٩﴾

Mkizozana katika jambo basi lirudisheni kwa Allaah na Rasuli. [An-Nisaa: 59]

 

مَّن يُطِعِ الرَّسُولَ فَقَدْ أَطَاعَ اللَّـهَ ﴿٨٠﴾

Atakayemtii Rasuli basi kwa yakini amemtii Allaah. [An-Nisaa: 80]

 

إِنَّكَ لَتَهْدِي إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿٥٢﴾

Na hakika wewe (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) bila shaka unaongoza kuelekea njia iliyonyooka.

صِرَاطِ اللَّـهِ ﴿٥٣﴾

Njia ya Allaah… [As-Shuwraa: 52-53]

 

فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٦٣﴾

Basi watahadhari wale wanaokhalifu amri yake, isije kuwasibu fitnah au ikawasibu adhabu iumizayo. [An-Nuwr: 63]

 

وَاذْكُرْنَ مَا يُتْلَىٰ فِي بُيُوتِكُنَّ مِنْ آيَاتِ اللَّـهِ وَالْحِكْمَةِ ﴿٣٤﴾

Na kumbukeni yale yanayosomwa majumbani mwenu katika Ayaat za Allaah na Hikmah (Sunnah). [Al-Ahzaab: 34]

 

 

Hadiyth – 1

 

عن أبي هريرةَ رضي الله عنه عن النَّبيّ صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((دَعُونِي مَا تَرَكْتُكُمْ، إِنَّمَا أَهْلَكَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ كَثْرَةُ سُؤالِهِمْ واخْتِلافُهُمْ عَلَى أنْبيَائِهِمْ، فَإِذَا نَهَيْتُكُمْ عَنْ شَيْء فَاجْتَنِبُوهُ، وَإِذَا أمَرْتُكُمْ بشيءٍ فَأْتُوا مِنْهُ مَا اسْتَطَعْتُمْ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amepokea kutoka kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Jiepusheni kwa mambo ambayo sijawatajia, kwani hakika waliangamia wale walio kabla yenu kwa sababu ya kuuliza kwao maswali mengi na kukhitalifiana na Rasuli wao. Basi ninapowakataza jambo liepukeni, na ninapowaamuru jambo, basi fanyeni kwa kadiri muwezavyo.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

 

عن أَبي نَجيحٍ العِرباضِ بنِ سَارية رضي الله عنه قَالَ: وَعَظَنَا رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم مَوعظةً بَليغَةً وَجِلَتْ مِنْهَا القُلُوبُ، وَذَرَفَتْ مِنْهَا العُيُونُ، فَقُلْنَا: يَا رسولَ اللهِ، كَأَنَّهَا مَوْعِظَةُ مُوَدِّعٍ فَأوْصِنَا، قَالَ: ((أُوصِيكُمْ بِتَقْوَى اللهِ، وَالسَّمْعِ وَالطَّاعَةِ وَإنْ تَأمَّر عَلَيْكُمْ عَبْدٌ حَبَشِيٌّ، وَإِنَّهُ مَنْ يَعِشْ مِنْكُمْ فَسَيَرَى اختِلافًا كَثيرًا، فَعَليْكُمْ بسُنَّتِي وسُنَّةِ الخُلَفاءِ الرَّاشِدِينَ المَهْدِيِيِّنَ عَضُّوا عَلَيْهَا بالنَّواجِذِ، وَإِيَّاكُمْ وَمُحْدَثَاتِ الأُمُورِ؛ فإنَّ كلَّ بدعة ضلالة)). رواه أَبُو داود والترمذي، وَقالَ: ((حديث حسن صحيح))

Abuu Najiyh Al-‘Irbaadhw bin Saariyah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitupa mawaidha mazito (yenye maana pana), nyonyo zikaingia khofu na macho  yakabubujikwa na machozi. Tukamwambia: Ee Rasuli wa Allaah, inaonekana kana kwamba haya mawaidha ni yakutuaga, basi tuusie. Akasema: “Nawausia taqwa ya Allaah, kusikiliza na kutii, hata kama mkiongozwa na mtumwa mhabeshi. Hakika atakayeishi umri mrefu miongoni mwenu ataona khitilafu nyingi. Kwa hivyo ninyi shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za  Khulafaa Ar-Rashidiyna (Makhalifah waongofu) wenye kuongoza. Ishikilieni (Sunnah) kwa magego. Na tahadharini mambo yenye kuzushwa, hakika kila bid’ah ni upotevu.” [Abuu Daawuud na At-Tirmidhy, na amesema: Hadiyth hii ni Hasan Swahiyh]

 

 

Hadiyth – 3

 

عَنْ أَبي هريرةَ رضي الله عنه: أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ: ((كُلُّ أُمَّتِي يَدخُلُونَ الجَنَّةَ إلا مَنْ أبَى)). قيلَ: وَمَنْ يَأبَى يَا رَسُول الله؟ قَالَ: ((مَنْ أَطَاعَنِي دَخَلَ الجَنَّةَ، وَمَنْ عَصَانِي فَقَدْ أبَى)). رواه البخاري

Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesimulia: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Ummah wangu wote wataingia Jannah isipokuwa atakayekataa.” Akaulizwa: “Ni yupi atakayekataa Ee Rasuli wa Allaah? Akajibu: “Atakayenitii mimi ataingia Jannah, na atakayeniasi basi amekataa.” [Al-Bukhaariy]

 

 

Hadiyth – 4

 

عن أَبي مسلم، وقيل: أَبي إياس سَلمة بنِ عمرو بنِ الأكوع رضي الله عنه أنَّ رَجُلًا أَكَلَ عِنْدَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم بِشِمَالِهِ، فَقَالَ: ((كُلْ بِيَمِينكَ)) قَالَ: لا أسْتَطيعُ. قَالَ: ((لاَ استَطَعْتَ)). مَا مَنَعَهُ إلا الكِبْرُ، فمَا رَفَعَهَا إِلَى فِيهِ. رواه مسلم

Abuu Muslim, pia anaitwa Abuu Iyaas, Salamah bin ‘Amruw bin Al-Akwa’ (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesimulia: Mtu mmoja alikula kwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mkono wake wa kushoto. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Kula kwa mkono wako wa kulia.” Yule mtu akasema siwezi. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia: “Hutaweza!” Hakuna kilichomzuia isipokwa ni kibri. Basi hakuweza tena kuinua mkono wake hadi kinywani mwake. [Muslim]

 

 

Hadiyth – 5

 

عن أَبي عبدِ الله النعمان بن بشير رَضيَ الله عنهما، قَالَ: سمعت رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يقول: ((لَتُسَوُّنَّ صُفُوفَكُمْ، أَوْ لَيُخَالِفَنَّ اللهُ بَيْنَ وُجُوهِكُمْ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

وفي رواية لمسلم: كَانَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم يُسَوِّي صُفُوفَنَا حتى كأنَّما يُسَوِّي بِهَا القِدَاحَ حَتَّى إِذَا رَأَى أَنَّا قَدْ عَقَلْنَا عَنْهُ. ثُمَّ خَرَجَ يَومًا فقامَ حَتَّى كَادَ أنْ يُكَبِّرَ فرأَى رَجلًا بَاديًا صَدْرُهُ، فَقَالَ: ((عِبَادَ الله، لَتُسَوُّنَّ صُفُوفَكُمْ أَوْ لَيُخَالِفَنَّ اللهُ بَيْنَ وُجُوهِكُمْ))

Abuu ‘Abdillaah, An-Nu’maan bin Bashiyr (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) amesema: Nilimsikia Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Wa-Allaahi mtazisawazisha safu zenu au Allaah Atazibadilisha nyuso zenu (ziwe kama wanyama au nyoyo zikhitilafiane).” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Riwaayah nyingine ya Muslim imesema:

Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akizisawazisha safu kana kwamba alikuwa anasawazisha kwazo mshale, mpaka atuone kuwa tumefahamu juu ya umuhimu huo. Kisha siku moja akatoka, akasimama hata alipokaribia kupiga Takbiyr, akamuona mtu kifua chake kimetokeza, akasema: “Enyi waja wa Allaah, mtasawazisha safu zenu au Allaah Atazibadilisha nyuso zenu (ziwe kama wanyama au nyoyo zikhitilafiane).”

 

 

Hadiyth – 6

 

عن أَبي موسى رضي الله عنه قَالَ: احْتَرقَ بَيْتٌ بالمَدِينَةِ عَلَى أهْلِهِ مِنَ اللَّيلِ، فَلَمَّا حُدِّثَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم بشَأنِهِمْ، قَالَ: ((إنَّ هذِهِ النَّارَ عَدُوٌّ لَكُمْ، فَإِذَا نِمْتُمْ، فَأطْفِئُوهَا عَنْكُمْ)). مُتَّفَقٌ عَلَيه

Abuu Muwsaa (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesimulia: Siku moja nyumba iliteketea Madiynah wakati wa usiku na wenyewe wamo ndani. Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alipohadithhiwa habari hiyo, alisema: “Hakika huo moto ni adui yenu, mnapolala uzimeni.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 7

 

عَنْهُ، قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((إنَّ مَثَلَ مَا بَعَثَنِي الله بِهِ مِنَ الهُدَى والعِلْم كَمَثَلِ غَيثٍ أَصَابَ أرْضًا فَكَانَتْ مِنْهَا طَائِفةٌ طَيِّبَةٌ، قَبِلَتِ المَاءَ فَأَنْبَتَتِ الكَلأَ والعُشْبَ الكَثِيرَ، وَكَانَ مِنْهَا أَجَادِبُ أمسَكَتِ المَاء فَنَفَعَ اللهُ بِهَا النَّاسَ فَشَربُوا مِنْهَا وَسَقُوا وَزَرَعُوا، وَأَصَابَ طَائفةً مِنْهَا أخْرَى إنَّمَا هِيَ قيعَانٌ لا تُمْسِكُ مَاءً وَلا تُنْبِتُ كَلأً، فَذَلِكَ مَثَلُ مَنْ فَقُهَ في دِينِ اللهِ وَنَفَعَهُ بمَا بَعَثَنِي الله بِهِ فَعَلِمَ وَعَلَّمَ، وَمَثَلُ مَنْ لَمْ يَرْفَعْ بِذَلِكَ رَأسًا وَلَمْ يَقْبَلْ هُدَى اللهِ الَّذِي أُرْسِلْتُ بِهِ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

Abuu Muwsaa (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mfano wa Aliyonituma kwayo Allaah katika uongofu na elimu, ni mfano wa mvua nyingi iliyonyesha katika nchi, ikawa ina rutuba, ikakubali maji, ikaotesha nyasi na maji mengi. Na sehemu nyingine ikawa ni kavu na ngumu inayozuia maji, Allaah Akawanufaisha watu kwa mvua hiyo. Wakanywa, wakanywesha mifugo na kulimia kwayo. Na ikanyesha sehemu nyingine ambayo ni kavu haizuii maji, wala haioteshi nyasi. Basi mifano hiyo ni mfano wa mtu aliyekuwa na ufahamu mzuri katika Dini ya Allaah, yakamnufaisha yale Aliyonituma kwayo Allaah, akajifunza na akafundisha. Na mfano wa mwisho ni mfano wa mtu ambaye, hakuinua kichwa kwa jambo hilo na wala hakuukubali uongofu wa Allaah niliyotumwa nao.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 8

 

عن جابر رضي الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم: ((مَثَلِي وَمَثَلُكُمْ كَمَثَلِ رَجُلٍ أوْقَدَ نَارًا فَجَعَلَ الجَنَادِبُ والفَرَاشُ يَقَعْنَ فِيهَا وَهُوَ يَذُبُّهُنَّ عَنْهَا، وَأَنَا آخذٌ بحُجَزكُمْ عَنِ النَّارِ، وَأنْتُمْ تَفَلَّتونَ مِنْ يَدَيَّ)). رواه مسلم

Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Mfano wangu na mfano wenu ni kama mtu aliyewasha moto, panzi na vipepeo wakawa wanaingia naye humo (mtu huyo) akawa anazuia wasiingie. Nami nimewashika viuno vyenu (sehemu ya kuifungia mkanda) kuwaokoa na moto, lakini mnaniponyoka mkononi mwangu (nashinda kuwazuia)!” [Muslim]

 

 

Hadiyth – 9

 

عَنْهُ أنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم أَمَرَ بِلَعْقِ الأَصَابِعِ وَالصَّحْفَةِ، وَقَالَ: ((إنَّكُمْ لا تَدْرونَ في أَيِّها البَرَكَةُ)). رواه مسلم.

وفي رواية لَهُ: ((إِذَا وَقَعَتْ لُقْمَةُ أَحَدِكُمْ فَلْيَأخُذْهَا، فَليُمِطْ مَا كَانَ بِهَا مِنْ أذىً، وَلْيَأكُلْهَا وَلا يَدَعْهَا لِلشَّيطَانِ، وَلا يَمْسَحْ يَدَهُ بالمنْدِيلِ حَتَّى يَلْعَقَ أصَابعَهُ فَإِنَّهُ لا يَدْرِي في أيِّ طَعَامِهِ البَرَكَةُ)).

وفي رواية لَهُ: ((إنَّ الشَّيطَانَ يَحْضُرُ أَحَدَكُمْ عِنْدَ كُلِّ شَيءٍ مِنْ شَأنِهِ، حَتَّى يَحْضُرَهُ عِنْدَ طَعَامِهِ، فَإذَ سَقَطَتْ مِنْ أَحَدِكُمْ اللُّقْمَةُ فَليُمِطْ مَا كَانَ بِهَا مِنْ أذَىً، فَلْيَأكُلْهَا وَلا يَدَعْهَا لِلشَّيطَانِ))

Jaabir (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesimulia: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ameamrisha kulamba vidole na sahani, akasema: “Ninyi hamjui ni wapi penye baraka.” [Muslim] 

Riwaayah nyingine ya Muslim imesema: 

 “Linapoanguka tonge la chakula la mmoja wenu, aliokote na aondoe taka iliyoingia na alile, wala asimuachie shaytwaan, wala asiupanguse mkono wake kwa kitambaa mpaka avilambe kidole vyake; kwani hajui ni katika chakula kipi kuna baraka.” 

Riwaayaha nyingine tena ya Muslim imesema:  

“Hakika shaytwaan anahudhuria katika kila jambo la mmoja wenu hata anahudhuria  kwenye chakula chake. Basi linapoanguka tonge la chakula la mmoja wenu, aondoe sehemu iliyoingia taka na alile, wala asimuachie shaytwaan.”

 

 

Hadiyth – 10

 

عن ابن عباس رضي الله عنهما، قَالَ: قَامَ فِينَا رَسُول الله صلى الله عليه وسلم بِمَوعِظَةٍ، فَقَالَ: "يَا أيُّهَا النَّاسُ، إنَّكُمْ مَحْشُورونَ إِلَى الله تَعَالَى حُفَاةً عُرَاةً غُرْلًا" كَمَا بَدَأْنَا أَوَّلَ خَلْقٍ نُعِيدُهُ وَعْدًا عَلَيْنَا إِنَّا كُنَّا فَاعِلِينَ  

ألا وَإنَّ أَوَّلَ الخَلائِقِ يُكْسى يَومَ القِيَامَةِ إبراهيمُ صلى الله عليه وسلم، ألا وَإِنَّهُ سَيُجَاءُ بِرجالٍ مِنْ أُمَّتي فَيُؤخَذُ بِهِمْ ذَاتَ الشَّمالِ، فَأَقُولُ: يَا رَبِّ أصْحَابِي. فَيُقَالُ: إنَّكَ لا تَدْرِي مَا أحْدَثُوا بَعْدَكَ. فَأقُولُ كَما قَالَ العَبدُ الصَّالِحُ: {وَكُنْتُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا مَا دُمْتُ فِيهِمْ} إِلَى قولِهِ: {العَزِيزُ الحَكِيمُ} [المائدة: 117- 118] فَيُقَالُ لِي: "إنَّهُمْ لَمْ يَزَالُوا مُرْتَدِّينَ عَلَى أعْقَابِهِمْ مُنْذُ فَارَقْتَهُمْ" مُتَّفَقٌ عَلَيه

‘Abdullaah bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما)   amesema: Siku moja Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  alisimama na kututolea mawaidha akasema: “Enyi watu, hakika mtafufuliwa na Allaah haliyakuwa hamna viatu, mpo uchi na bila kutahiriwa  (na magovi) Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

كَمَا بَدَأْنَا أَوَّلَ خَلْقٍ نُّعِيدُهُ

Kama Tulivyoanza umbo la awali Tutalirudisha tena [Al-Anbiyaa: 104]

 

Tanabahini! Hakika mtu wa kwanza atakayevishwa nguo ni Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام). Tanabahini! Wataletwa watu katika Ummah wangu na watapelekwa upande wa kushoto (motoni), nami nitasema: “Ee Rabb wangu, Swahaba wangu!” Nitaambiwa: “Wewe hujui watu hawa walichokizua baada yako.” Hapo nitasema kama alivyosema mja mwema (Nabiy ‘Iysaa):

 

وَكُنتُ عَلَيْهِمْ شَهِيدًا مَّا دُمْتُ فِيهِمْ ۖ فَلَمَّا تَوَفَّيْتَنِي كُنتَ أَنتَ الرَّقِيبَ عَلَيْهِمْ ۚ وَأَنتَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ شَهِيدٌ ﴿١١٧﴾

Na nilikuwa juu yao shahidi wakati nilipokuwa nao. Uliponikamilishia muda Ukanichukua juu, Ulikuwa Wewe Ndiye Mwangalizi juu yao. Na Wewe Ni Mwenye Kushuhudia kila kitu.

 

إِن تُعَذِّبْهُمْ فَإِنَّهُمْ عِبَادُكَ ۖ وَإِن تَغْفِرْ لَهُمْ فَإِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١١٨﴾

Ukiwaadhibu, basi bila shaka hao ni Waja Wako, na Ukiwaghufuria basi hakika Wewe Ndiye Mwenye Enzi na Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote. [Al-Maaidah (5:117-118]

 

Nitaambiwa: “Wao waliendelea kukengeuka na kugeuka nyuma kuondokelea mbali ulipowaacha.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 11

 

عن أَبي سعيد عبد الله بن مُغَفَّلٍ رضي الله عنه قَالَ: نَهَى رَسُول الله صلى الله عليه وسلم عَنِ الخَذْفِ، وقالَ: ((إنَّهُ لا يَقْتُلُ الصَّيْدَ، وَلا يَنْكَأُ العَدُوَّ، وإنَّهُ يَفْقَأُ العَيْنَ، وَيَكْسِرُ السِّنَّ)). مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

وفي رواية: أنَّ قَريبًا لابْنِ مُغَفَّل خَذَفَ فَنَهَاهُ، وَقالَ: إنَّ رَسُول الله صلى الله عليه وسلم نَهَى عَن الخَذْفِ، وَقَالَ: ((إنَّهَا لا تَصِيدُ صَيدًا)) ثُمَّ عادَ، فَقَالَ: أُحَدِّثُكَ أنَّ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم نَهَى عَنْهُ، ثُمَّ عُدْتَ تَخذفُ!؟ لا أُكَلِّمُكَ أَبَدًا.

Abuu Sa’yd, ‘Abdullaah bin Mughaffal (Radhwiya Allaahu ‘anhu) amesema: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza al-khadhaf’ (kurusha vijiwe kwa kutumia kidole gumba na cha shahaadah) akasema: “Kwani hakiuwi windo wala hakimuuwi adui, bali hutoboa jicho na kuvunja jino tu.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

Riwaayah nyingine ya Muslim imesema:

“Jamaa mmoja wa karibu kwa Ibn Mughaffal alifanya khadhaf. Akamkataza na akamwambia: Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza kitendo hiki (khadhaf), akasema: “Kwani hakiwindi windo” Kisha yule jamaa akarudia kitendo hicho. Akamwambia: Nimekuhadithia kuwa Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amekataza jambo hilo kisha umerudia kitendo hicho cha khadhaf? Sitazungumza nawe kamwe!

 

 

Hadiyth – 12

 

 وعَن عابس بن رَبيعة، قَالَ: رَأيْتُ عُمَرَ بن الخطاب رضي الله عنه يُقَبِّلُ الحَجَرَ- يَعْنِي: الأسْوَدَ- وَيَقُولُ: إني أَعْلَمُ أنَّكَ حَجَرٌ مَا تَنْفَعُ وَلا تَضُرُّ، وَلَولا أنِّي رَأيْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم يُقَبِّلُكَ مَا قَبَّلْتُكَ. مُتَّفَقٌ عَلَيهِ

‘Aabis bin Rabiy’h amesema: Nilimuona ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu ‘anhu) akilibusu Hajarul Aswad (jiwe jeusi) na akasema: Hakika najua wewe ni jiwe, hunufaishi wala hudhuru, lau kama nisingelimuona Rasuli (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akikubusu nisingelikubusu. [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Share