Shaykh Yahyaa Al-Hajuwriy- Hukmu Ya Anayemtuhumu Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah)

 

Hukmu Ya Anayemtuhumu Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah)

Kuwa Ni Miongoni Mwa Murji-ah

 

Utetezi Wa Al-‘Allaamah Al-Hajuwriy kwa Al-Imaam Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah).

 

Shaykh Yahyaa Al-Hajuwriy (Hafidhwahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com  

 

 

SWALI:

 

Je, Shaykh Al-Albaaniy ni katika Murji-ah Al-Fuqahaa?

 

 

JIBU:

 

Wale wanaosema kuwa Shaykh Al-Albaaniy ni Murji-iy ((Neno kubwa linatoka katika midomo yao. Hawasemi isipokuwa uongo tu)).

 

Shaykh Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) ni Mwanachuoni Salafi, na amewaraddi Murji-ah na Jahmiyyah na Qadariyyah na Jabriyyah na wengineo, kinyume na hao wanaomtuhumu kwa tuhuma hiyo, ambao hawajaweza kufanya aliyofanya yeye.

 

Lakini ni kama inavyosemwa, “شنشنة أعرفها من أخزم“ (Makusudio ni kisa cha Haatim Atw-Twaa-iy alivyofananishwa na babu yake Akhzam Atw-Twaa-iy kwa tabia. - Akikusudia Shaykh Yahyaa kuwa, maadui wa haki nao wanafanana tuhuma zao na dhulma zao kwa watu wa haki).

 

Huwezi kumkuta Salafi anapambana na baatwil na watu wa baatwil isipokuwa watamrushia makubwa (tuhuma kubwa kubwa).

 

Basi tambua hili.

 

[Nadhwaraat Min Awaail Duruws Fadhwiylat Ash-Shaykh Yahyaa bin ‘Aliy Al-Hajuwriy

 

 

 

Share