Skip navigation.
Home kabah

Hukmu Ya Mwanamke Kuadhini Na Kukimu

Hukmu Ya Mwanamke Kuadhini Na Kukimu

 

Imaam Muqbil Bin Haadiy Al-Waadi’iy (Rahimahu Allaah)

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Je, mwanamke anafaa kuadhini na kukimu?

 

 

JIBU:

 

Haijapokelewa kutoka kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) suala hili la (mwanamke) kuadhini na wala (haijapokelewa) kutoka kwa Maswahaba na Maswahaabiyaat katika zama za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Na Allaah (‘Azza wa Jalla) Anasema:

فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيَطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ  

"Basi msilegeze kauli asije akaingiwa tamaa ambaye moyoni mwake mna maradhi." [Al-Ahzaab 33; 32]

 

Basi inamtosheleza adhaan ya mwanamme. Na (ama) iqaamah hakuna neno akikimu In Shaa Allaah; na Allaah Ndiye Anayeombwa msaada.

 

Ash-Shawkaaniy na Muhammd Swiddiyq Hasan Khan wamesema: “Aadhini na akimu, kwa sababu asili yake ni shariy’ah ya ujumla.

Lakini haikupokelewa kwamba wanawake walikuwa wakiadhini zama za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).

 

[Kutoka kanda: As-ilah Shabaab Al-Hasiynah, http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=938]

 

 

Rudi Juu