33-Mukhtasari Aqiydah Ya Muislamu: Nini hukumu ya kufuata shariy’ah zisizo za Kiislam?

Mukhtasari Wa ‘Aqiydah Ya Muislamu

Maswali Na Majibu Pamoja Na Dalili Kutoka Qur-aan Na Sunnah.

Imetarjumiwa na: Alhidaaya.com

 

 

 

33-Nini hukumu ya kufuata shariy’ah zisizo za Kiislam?

 

Kuzifuata shariy’ah zisizo za Kiislamu na kuzifanyia kazi na kuziacha shariy’ah za Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) ni kufuru kubwa.

 

وَمَن لَّمْ يَحْكُم بِمَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ﴿٤٤﴾

Na yeyote asiyehukumu kwa yale Aliyoyateremsha Allaah, basi hao ndio makafiri. [Al-Maaidah 44]

 

((وَمَا لَمْ تَحْكُمْ أَئِمَّتُهُمْ بِكِتَابِ اللَّهِ وَيَتَخَيَّرُوا مِمَّا أَنْزَلَ اللَّهُ إِلَّا جَعَلَ اللَّهُ بَأْسَهُمْ بَيْنَهُمْ))  حسن رواه ابن ماجه

((Na wasipohukumu viongozi wao kwa Kitabu cha Allaah na wakawa wanachagua katika Aliyoyateremsha Allaah, basi Allaah Atawajaalia kutoelewana (migongano) baina yao [Hadiyth Hasan ameipokea Ibn Maajah]

 

 

 

Share