Nashiyd Qaswiyda Na Hukmu Zake
SWALI:
Swali langu ni haya mapiya:-
a) KASWIDA ni nini katika (dini)SUNNA
b) Msimamo wa SUNNA katika......NASHEET.
c) Jee NASHEET ni nyimbo(HARAM) AU ni kumsifu MTUME WETU MUHAMMAD (S. A. W)?
d) Jee ni KHERI kusikiza NASHEET, kulikoni basi RAP, au nyimbo aina nyingine,
e) Jee ushawahi KUZISIKIA hizo Nasheet, hata kwa MBALI, zilivyofana na nyimbo za sikuhizi mbaya
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Tunashukuru kupata swali kuhusu maudhui hiyo, jambo ambalo limedhihirika sana siku hizi miongoni mwetu Waislamu, hivyo ni vizuri kujua hukmu ya jambo hili.
a) KASWIDA ni nini katika (dini)SUNNA?
JIBU:
Nashiyd na Kaswida (Qaswiydah) zinajulikana na wengi ni
Nashiyd inatokana na Qaswiydah kwa sababu Qaswiydah ni mashairi, lakini kwa kuimbwa kwa sauti Fulani ya juu na yenye mahadhi ndipo ikajulikana
Na Nashiyd ni nyimbo ambazo zaidi zimehusishwa na Dini na haswa kumsifu Allah, au Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) au kitu chochote kile ambacho kinahusiana na Dini zaidi. Na kwa hivyo imetofautiana na kuitwa ni nyimbo kwa sababu ni nyimbo maalum.
Hukumu ya Qaswiydah au Nashiyd huwezi kusema ni Sunnah, lakini unaweza kusema ni jambo ambalo likifanywa kwa misingi mizuri itakuwa
b) Msimamo wa SUNNA katika......NASHEET
JIBU:
Imeruhusiwa kusoma au kusikiliza shairi kutokana na dalili katika Siyrah ya Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)
Kutoka kwa Anas (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba walipokuwa wakichimba al-khandaq (shimo katika vita vya al-Khandaq). Kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliwaona Maswahaba jinsi walivyochoka, na kubanwa na njaa, hivyo akasema (katika beti) ((Ewe Allah, hakuna maisha isipokuwa maisha ya Akhera, kwa hiyo wasamehe Maanswaari na Muhaajiriyn)) Nao (Maswahaba) wakajibu: "Sisi ndio tuliyoweka ahadi kwa Muhammad, kufanya jihaad maishani mwetu madamu tuko hai" [Al-Bukhaariy]
c) Jee NASHEET ni nyimbo (HARAM) AU ni kumsifu MTUME WETU MUHAMMAD (S. A. W)?
JIBU:
Nashiyd ni nyimbo, lakini zaidi zimejulikana kuwa ni nyimbo za dini. Kwa tafsiri haswa ya Nashiyd ni kipande cha shairi chenye kuimbwa kwa sauti ya aina moja.
Nashiyd kama tulivyosema sio haraam kuimba. Lakini isiwe kama nyimbo nyingine ziimbwazo ambazo zimekusanya kila aina ya maneno kama matusi, mambo ya kipuuzi n.k., au pia kama nyimbo ambazo zinaambatana na ala za muziki, hizo ni haraam zimekatazwa na dalili ipo kwenye Aayah ifuatayo:
((وَمِنَ النَّاسِ مَن يَشْتَرِي لَهْوَ الْحَدِيثِ لِيُضِلَّ عَن سَبِيلِ اللَّهِ بِغَيْرِ عِلْمٍ وَيَتَّخِذَهَا هُزُوًا أُولَئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ))
((Na miongoni mwa watu wapo wanaonunua maneno ya upuuzi, ili wawapoteze watu na njia ya Mwenyezi Mungu pasipo kujua, na wanaichukulia ni maskhara. Hao watapata adhabu ya kuwafedhehesha)) Luqmaan:6
Ibn Mas'uud ÑÖí Çááå Úäå amesema kuhusu aya hii "Naapa kwa Allaah hii inamaanisha ni nyimbo" [At-Twabariy 20:127]
Vile vile:
((وَاسْتَفْزِزْ مَنِ اسْتَطَعْتَ مِنْهُمْ بِصَوْتِكَ وَأَجْلِبْ عَلَيْهِم بِخَيْلِكَ وَرَجِلِكَ وَشَارِكْهُمْ فِي الأَمْوَالِ وَالأَوْلادِ وَعِدْهُمْ وَمَا يَعِدُهُمُ الشَّيْطَانُ إِلاَّ غُرُورًا))
((Na wachochee uwawezao katika wao kwa sauti yako, na wakusanyie jeshi lako la wapandao farasi na waendao kwa miguu. Na shirikiana nao katika mali na wana, na waahidi. Na Shetani hawapi ahadi ila ya udanganyifu)) [Al-Israa:64]
Mujaahid kasema hii ni vifirimbi.
Imesimuliwa kutoka katika Hadiyth sahihi kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuwa kasema: “Katika Ummah wangu watakuja watu ambao watahalalisha zinaa, hariri (kwa wanaume), pombe na ala za muziki (ma’aazif). Baadhi
Nashiyd za kumsifia Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) hazina neno kuimbwa lakini nazo zisiwe za kumsifu
Vile vile Nashiyd nyinginezo sio zote ambazo ni halaal kuziimba kwani kuna mambo mengi yanayozifanya zisiwe katika mipaka ya sheria nayo ni haya ya kuzingatia:
- Zisitumiwe vyombo vya muziki.
- Zisiwe na maneno ya kumtukuza mtu hadi ampandishe cheo cha utukufu wa Uungu.
- Zisiimbwe na wanawake hadharani au mbele ya wanaume au zisiwe na maneno ya pujufu, yasiyo na heshima au machafu.
- Zisiwe na sauti za uasharati na ufasiki na za mapenzi.
- Zisiwe na melodia za sauti ya juu hadi imfanye anayesikiliza au kuimba apatwe na shauku ya sauti zaidi hata aache kusikiliza maneno yenyewe yenye mafunzo ndani yake.
Wanawake wanaweza kuimba wakiwa wenyewe na haswa siku za sikukuu na siku za Harusi. Na wanaruhusiwa kupiga dufu wakiimba.
d) Jee ni KHERI kusikiza NASHEET, kulikoni basi RAP, au nyimbo aina nyingine,
JIBU:
Kusikiliza Nashiyd hakuna ubaya lakini kutegemea na Nashiyd zenyewe, na pia isiwe ndio shughuli ya kukuchukulia muda wako.
Bila ya shaka kusikiliza nyimbo kama hizo zinazoitwa RAP au nyimbo nyingine ni haraam kama tulivyotaja hapo kwa dalili zilizokuja katika Qur-aan. Hata kama zinamtaja Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam), lakini maadam zina ukosefu na ubaya tuliotaja hapo juu basi itakuwa ni haraam kuziimba.
Nashiyd zimfanye Muislamu apoteze wakati wake mwingi kuziimba au kuzisikiliza wakati angeliweza kufanya yaliyo na thawabu kama kusoma au kusikiliza Qur-aan, mawaidha na mengi mengineyo ambayo yatamuongezea elimu na thawabu. Tunaona kwamba siku hizi Nashiyd zimezidi kwa wingi na nyingi hazimo katika mipaka iliyoruhusiwa kisheria na wengi wanashughulika nazo na kuacha yale yaliyo muhimu kufanya katika dini yao kama kutafuta elimu, kusoma vitabu vya dini. Na kisingizio ni kwamba zinataja mambo yanayohusu dini.
Kwa hakika Nashiyd inaweza kuingia katika burudani zaidi kuliko mafundisho. Wengi wanaona ni bora kwa sababu inawafanya wasisikilize muziki kwa sababu ni haraam, hivyo lazima kupatikane badili. Na badili ya muziki ni Nashiyd kama wengi wanavyoona. Lakini ingekuwa bora zaidi kama badili hiyo ingekuwa Qur-aan au mawaidha kwa sababu ndani ya hivyo kuna elimu, mafundisho na ujira mkubwa.
Juu ya hivyo, Muislamu ameruhusiwa bali amesisitizwa kuisoma Qur-aan kwa kuipendezesha sauti yake.
عن البراء بن عازب رضي الله عنه أن النبي صلى الله عليه وسلم قال: (("زينوا القرآن بأصواتكم")). صححه الألباني في صحيح سنن أبي داود، ورواه الحاكم في المستدرك
Kutoka kwa Al-Baraa bin 'Aazib (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Pambeni Qur-aan kwa sauti zenu)) [Sunan Abu Daawuud, Al-Mustadrak Al-Haakim na ameipa daraja ya sahiyh Shaykh Al-Albaaniy]
عن سعد بن أبي وقاص رضي الله عنه قال: قال رسول اللَّه صلى الله عليه وسلم : ((ليس منا من لم يتغن بالقرآن)) روى أبو داود في سننه وصححه الألباني
Kutoka kwa Sa'ad bin Abi Waqaasw (Radhiya Allahu 'anhu) ambaye amesema: Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Sio miongoni mwetu yule asiyeiimba (asiyeipendezesha sauti yake) Qur-aan)) [Abu Daawuud na kaipa daraja ya sahiyh Shaykh Al-Albaaniy]
عن أبي هريرة رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال: ((ما أذن الله لشيءٍ أَذَنَهُ لنبي يتغنى بالقرآن)) البخاري
Kutoka kwa Abi Hurayrah (Radhiya Allahu 'anhu) kwamba Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Hakuna Anachopenda kusikiliza Allah
Wasomaji wangapi tunawasikia wakiisoma Qur-aan kwa sauti ya kupendeza na kuburudisha moyo? Kwa nini basi Muislamu asipendelee zaidi kupamba sauti yake katika kuisoma Qur-aan ili azidi kupata thawabu?
e) Jee ushawahi KUZISIKIA hizo Nasheet, hata kwa MBALI, zilivyofana na nyimbo za sikuhizi mbaya
JIBU:
Ndio kama tulivyosema kuwa Nashiyd za siku hzi nyingi kabisa zimevuka mipaka ya sheria hadi kufikia kama nyimbo za bendi za muziki. Nyingine nyingi zinaimbwa na kutiwa zana za muziki na nyingine zinaimbwa na wanawake au kuimbwa na mchanganyiko wa wanawake na wanaume jambo ambalo halifai kabisa katika dini yetu.
Na kumezidi siku hizi kama tunavyoona kwenye matelevisheni haswa kwenye idhaa za Kiislam kama vile 'Islam Channel' na zinginezo, hadi kumekuwa na makundi ya Nashiyd na makundi ya Rap wanazosema za Kiislam na wanatolea dalili za uhalali wake kwa kufananisha na wakati wa vita kuwa Maswahaba walikuwa wakihamasishana na wao nao wanafanya kama vile kwa njia hiyo ya Rap! Baya zaidi makundi mengi yamekuwa yakiiga mitindo, sauti, mahadhi ya bendi za makafiri na hata kuiga staili zao za uimbaji.
Na Allah Anajua zaidi
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


