020-Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake أسماء الله الحسنى وصفاته: AL-JABBAAR

 

أسماء الله الحسنى وصفاته

Majina Ya Allaah Mazuri Na Swifa Zake

 

Alhidaaya.com

 

 

الْجَبَّار

AL-JABBAAR

 

 

 

Al-Jabbaar:  Jabari, Asiyeshindwa kufanya Atakalo.

 

Jina hili tukufu la Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) limetajwa mara moja katika kauli Yake Ta’aalaa:    

هُوَ اللَّـهُ الَّذِي لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْمَلِكُ الْقُدُّوسُ السَّلَامُ الْمُؤْمِنُ الْمُهَيْمِنُ الْعَزِيزُ الْجَبَّارُ  

Yeye Ndiye Allaah Ambaye hakuna Muabudiwa wa haki ila Yeye, Mfalme, Mtakatifu Ametakasika na sifa zote hasi, Mwenye kusalimisha, Amesalimika na kasoro zote, Mwenye kusadikisha ahadi, Mwenye kuaminisha, Mwenye kudhibiti, kushuhudia, kuchunga na kuhifadhi, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Jabari, Asiyeshindwa kufanya Atakalo [Al-Hashr: 59:23]

 

Na sifa hii imetajwa mara tisa katika Qur-aan kuwahusisha wana Aadam mfano:

 

قَالُوا يَا مُوسَىٰ إِنَّ فِيهَا قَوْمًا جَبَّارِينَ وَإِنَّا لَن نَّدْخُلَهَا حَتَّىٰ يَخْرُجُوا مِنْهَا فَإِن يَخْرُجُوا مِنْهَا فَإِنَّا دَاخِلُونَ ﴿٢٢﴾

22. Wakasema: “Ee Muwsaa! Hakika humo kuna watu majabari; nasi hatutoingia humo mpaka watoke humo; watakapotoka humo; basi hakika sisi tutaingia.” [Al-Maaidah: 22]

 

Na katika kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

وَتِلْكَ عَادٌ ۖ جَحَدُوا بِآيَاتِ رَبِّهِمْ وَعَصَوْا رُسُلَهُ وَاتَّبَعُوا أَمْرَ كُلِّ جَبَّارٍ عَنِيدٍ﴿٥٩﴾

Na hao ni kina ‘Aad. Wamezikanusha kwa ushupavu Aayaat (ishara, hoja) za Rabb wao, na wakawaasi Rusuli Wake, na wakafuata amri ya kila jabari mkaidi. [Huwd 11: 59]

 

وَإِذَا بَطَشْتُم بَطَشْتُمْ جَبَّارِينَ ﴿١٣٠﴾

“Na mnapokamata kushambulia mnatumia nguvu kwa uadui na ujabari. [Ash-Shu’araa 26: 130]

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ndiye Al-Jabbaar Mwenye kuyaendesha mambo yote ya ardhini na mbinguni vile Atakavyo. Huamrisha, Hukataza kwa muktadha wa hekima Zake, na uadilifu na miongoni mwa hayo ni Dini Yake ambayo Amewaridhia nao waja wake.

 

Naye Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ndiye Mwenye kuunga: Mwenye kurekebisha mambo ya waja Wake, Anafanya yanayowafaa wao, Ambaye huunga ufukara wao, na Akawatosha na sababu za maisha na riziki zao.

 

Al-Jabbaar Ambaye Hashindwi; Ambaye Huunga unyonge wa wanyonge katika waja Wake. Anaunga kilichovunjika. Anamtajirisha fakiri.

 

Humwepesishia mwenye uzito, uzito wake. Huunga kiungo maalumu; nyoyo za waliovunjika kwa ajili Yake, wenye kunyenyekea kwa utukufu na ukubwa Wake.

 

Huziunga nyoyo za waliokandamizwa kutokana na ambao waliojifanya majabari, kama Alivyounga moyo wa mama yake Nabiy Muwsaa ('Alayhis Salaam) baada ya kumtupa mwanawe katika mto wa Nile, akiwa kwenye sanduku, kisha mwanawe huyo akafika katika mikono ya Fir‘awn ambaye katika kipindi hicho alikuwa akiua kila mtoto aliyezaliwa.

Moyo wa mama yake Nabiy Muwsaa ('Alayhis Salaam) ukwa umejaa khofu na wahka lakini Allaah; Al-Jabbaar Aliuthibitisha akaweza kuvumilia. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

وَقَالَتِ امْرَأَتُ فِرْعَوْنَ قُرَّتُ عَيْنٍ لِّي وَلَكَ ۖ لَا تَقْتُلُوهُ عَسَىٰ أَن يَنفَعَنَا أَوْ نَتَّخِذَهُ وَلَدًا وَهُمْ لَا يَشْعُرُونَ ﴿٩﴾

9. Na mke wa Fir’awn akasema: “Kiburudisho cha macho kwangu na kwako; usimuue, asaa akatufaa, au tumfanye mwana.” Nao hawatambui.

 

وَأَصْبَحَ فُؤَادُ أُمِّ مُوسَىٰ فَارِغًا ۖ إِن كَادَتْ لَتُبْدِي بِهِ لَوْلَا أَن رَّبَطْنَا عَلَىٰ قَلْبِهَا لِتَكُونَ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٠﴾

10. Na ukawa moyo uliojaa hisia wa mama yake Muwsaa mtupu! Alikaribia kumdhihirisha (kuwa ni mwanawe) lau kama Tusingeutia nguvu moyo wake ili awe miongoni mwa Waumini.  [Al-Qaswasw: 9-10]

 

Huunga nyoyo za wapendanao kwa kuwamwagia anuai za ukarimu Wake, na aina mbali mbali za elimu, na hali mbali mbali za iymaan na uongofu na tawfiyq.

 

Humuunga mgonjwa, aliyepatwa na mitihani, aliyedhoofu kiwiliwili na hivyo hurahisisha sababu zote za ponyo kwake.  

 

Humuunga aliyepatwa na matatizo kwa tawfiyq Yake kwa subira na utulivu, na humpa badala ya malipo makubwa, pindi atakaposimamia majukumu yake.

 

Humuunga mja wake Muumini, kwa kustawisha hali zake, na malengo yake, pindi anapoomba muombaji kwa kusema: “Allahumma-Jburniy” kwani hapa anahitaji kuungwa ambayo hakika yake ni kumstawisha na kuondosha yote yenye kuchukiza. [Tafsiyr Al-Qurtwubiy (9/301)

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ndiye Al-Jabbaar; Ni kizuizi kisichofikiwa, hafikiwi wala hawezi kuingiwa na chukizo juu Yake, Haiwapati waja Wake dhara na yeye akadhurika na wala haiwapati manufaa wakanufaika.

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ndiye Al-Jabbaar: Anapotaka kitu huwa kama Anavyotaka, wala hazuiwi na yeyote, wala hakiendi kinyume chake na hivyo basi matendo yake huwa kama kulazimisha.

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ndiye Al-Jabbaar: Ni Mkubwa Mwenye kutakabari: Ambaye hakuna mwenye kujiona ana haki zaidi yake.

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ndiye Al-Jabbaar: Mwenye kutenza nguvu kila kitu, Ambaye kila kitu kinamkurubia, na kila kitu kinanyenyekea Kwake, Ulimwengu wa juu na wa chini, pamoja ya yaliyomo miongoni mwa waja Wake watukufu, kila kimoja kimenyenyekea katika harakati zake, na utulivu wake na yanayokuja na yanayobaki kwa mmiliki wake na mpangaji wake, hana lolote katika amri yake wala katika hukumu zake chochote bali mambo yote ni kutoka kwa Allaah.

 

Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Ndiye Al-Jabbaar Ambaye moto wa Jahannam unarejea Kwake kwa upungufu wake, kwa muradi wake wa kutoshelezwa.  Na pia Atauamrisha uwaingize wanaotakabari na wanaojifanya majabari. Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Anasema:  

 

يَوْمَ نَقُولُ لِجَهَنَّمَ هَلِ امْتَلَأْتِ وَتَقُولُ هَلْ مِن مَّزِيدٍ ﴿٣٠﴾

30. “Siku Tutakapoiambia Jahannam: “Je, umeshajaa?” Nayo itasema: “Je, kuna ziada yoyote?”  [Qaaf 50:30]  

 

Na katika Hadiyth ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) 

 

 عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، رضى الله عنه قَالَ قَالَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم: ((تَحَاجَّتِ الْجَنَّةُ وَالنَّارُ فَقَالَتِ النَّارُ أُوثِرْتُ بِالْمُتَكَبِّرِينَ وَالْمُتَجَبِّرِينَ‏.‏ وَقَالَتِ الْجَنَّةُ مَا لِي لاَ يَدْخُلُنِي إِلاَّ ضُعَفَاءُ النَّاسِ وَسَقَطُهُمْ‏.‏ قَالَ اللَّهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى لِلْجَنَّةِ:  أَنْتِ رَحْمَتِي أَرْحَمُ بِكِ مَنْ أَشَاءُ مِنْ عِبَادِي ‏.‏ وَقَالَ لِلنَّارِ إِنَّمَا أَنْتِ عَذَابٌ أُعَذِّبُ بِكِ مَنْ أَشَاءُ مِنْ عِبَادِي‏.‏ وَلِكُلِّ وَاحِدَةٍ مِنْهُمَا مِلْؤُهَا، فَأَمَّا النَّارُ فَلاَ تَمْتَلِئُ حَتَّى يَضَعَ رِجْلَهُ فَتَقُولُ قَطٍ قَطٍ قَطٍ‏.‏ فَهُنَالِكَ تَمْتَلِئُ وَيُزْوَى بَعْضُهَا إِلَى بَعْضٍ، وَلاَ يَظْلِمُ اللَّهُ ـ عَزَّ وَجَلَّ ـ مِنْ خَلْقِهِ أَحَدًا، وَأَمَّا الْجَنَّةُ فَإِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ يُنْشِئُ لَهَا خَلْقًا))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Jannah na moto ulibishana; moto ukasema: “Nimefadhilishwa kupokea wenye kutakabari na majabari.” Jannah ikasema: “Nina nini! Mbona hakuna anayeingia kwangu isipokuwa watu dhaifu na dhalili?” Allaah (Tabaaraka wa Ta’aalaa) Akasema kuiambia Jannah: “Wewe ni rahmah Yangu, ambayo Namrehemu kwako nimtakaye katika waja wangu.” Na Akauambia moto: “Hakika wewe ni adhabu Ninayomuadhibu kwako nitamtakaye katika waja Wangu.” Na kila mmoja miongoni mwao watajaa. Ama moto, hautojaa mpaka Allaah Aweke Mguu Wake kisha utasema: “Qatw! Qatw! Qatw!” Hapo ndio utajaa, na sehemu zake mbalimbali zitakaribiana na Allaah (‘Azza wa Jalla) Hatodhulumu yeyote katika viumbe Vyake. Ama Jannah basi Allaah (‘Azza wa Jalla) Ataumba umbile jipya kuijazia)) [Al-Bukhaariy Kitaab At-Tafsiyr]

 

Katika riwaayah nyingine:

حتى يَضَع الجبَّار فيها قَدمَه

((Hadi Al-Jabbaar Atakapoweka mguu wake humo)) [Imepokewa na Ad-Daaraqutwniy katika Swifaat 15]

 

 

Faida, Mafunzo Tuyapatayo Na Jinsi Ya Kufanyia Kazi Jina Hili La Allaah, Al-Jabbaar:

 

1. Usijfanye jabari kwa wenzako, bali kumbuka kwamba wewe ni mja wa Al-Jabbaar Ambaye Anakutosheleza kuuvunja ujabari wako. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

 

كَذَٰلِكَ يَطْبَعُ اللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ قَلْبِ مُتَكَبِّرٍ جَبَّارٍ ﴿٣٥﴾

Hivyo ndivyo Allaah Anavyopiga chapa juu ya kila moyo wa mwenye kutakabari, jabari. [Ghaafir 40: 35]

 

2. Tafakari jinsi Al-Jabbaar Anavyokulazimishia mambo katika uhai wako; kuanzia mwili wako na jinsi viungo ndani yake kama moyo, maini, matumbo, damu inavyotembea, chakula kusagika, bongo kufanya kazi, usingizi wako na kuamka kwako na kadhaalika jinsi Anavyoviendesha bila ya uwezo wako. Kutafakari kwako haya yatakuzishia iymaan kumjua Al-Jabbaar na kuzidi kumtukuza.

 

3. Unga nyoyo za nduguzo kwa kuwasamehe makosa yao kwako, na kuwasaidia kwa uwezo wa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) wenye kuhitaji msaada wako, ili Al-Jabbaar Akuunge nawe pindi utakapopatwa na shida.

 

4. Muombe Al-Jabbaar  kwa du’aa za Sunnah  kama ifuatavyo:

 

Unaporukuu na kusujudu kusema:

 

سُبْـحانَ ذي الْجَبَـروت، والمَلَـكوت، وَالكِبْـرِياء، وَالْعَظَـمَه

Subhaana dhil-Jabaruwti wal-malakuwti, wal-kibriyaai, wal-‘adhwamah

Ametakasika Mwenye Ujabari (Utawala, Utukufu), na Ufalme, na Ukubwa, na Uadhama. [Hadiyth ya ‘Awf bin Maalik Al-Ashja’iyy (Radhwiya Allaahu 'anhu) - [Abuu Daawuwd (1/230), Ahmad (6/24), An-Nasaaiy (2/191) na ameipa daraja ya Swahiyh Al-Albaaniy katika Swahiyh Abiy Daawuwd (1/166)]

 

Na baina ya sijda mbili:

 

 اللّهُـمَّ اغْفِـرْ لي، وَارْحَمْـني، وَاهْدِنـي، وَاجْبُرْنـي، وَعافِنـي وَارْزُقْنـي وَارْفَعْـني

Allaahummaghfir-liy, warhamniy, wahdiniy, wajburniy, wa ’aafiniy, warzuqniy, warfa’-niy

Ee Allaah nighufurie, na unirehemu, na uniongoze, na uniungie, na unipe afya, na uniruzuku na uniinue. [Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) - Aswhaab As-Sunan isipokuwa An-Nasaaiy; Abuu Daawuwd (850), At-Tirmdihiy (284), Ibn Maajah (898),  na angalia: Swahiyh At-Tirmidhiy (1/90) na Swahiyh Ibn Maajah (1/148)]

 

 

 

Share