Al-Lajnah Ad-Daa'imah-Hukmu Ya Kusherehekea Sikukuu Ya Mama

Hukmu Ya Kusherehekea Sikukuu Ya Mama

 

Al-Lajnah Ad-Daaimah

 

www.alhidaaya.com

 

 

SWALI:

 

Swali la tano kuhusu kusherehekea Siku ya Mama 

 

 

JIBU:

 

Haijuzu kusherehekea inayoitwa Sikukuu ya Mama  wala aina ya ‘Iyd kama hizo za bid’ah kutokana na kauli ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):

مَنْ عَمِلَ عَمَلاً ليسَ عليه أمرُنا هذا فهو رَدٌّ

((Atakayetenda kitendo kisichokuwa katika jambo letu hili (Dini yetu) basi kitarudishwa.)) [Al-Bukhaariy] 

 

Na kusherehekea sikukuu ya mama si katika matendo aliyoyafanya Nabiy wala si katika waliyotenda Maswahaba wake (Radhwiya Allaahu ‘anhum) wala si katika ‘amali za Salaf wa Ummah, bali hivyo ni bid’ah na kuiga makafiri.

 

Wa biLLaahi At-Tawfiyq.

Swalaah na salaam kwa Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na ahli zake na Maswahaba zake.

 

 

[Al-Lajnah Ad-Daaimah Lil-Buhuwth Al-‘Ilimiyyah, Swali Namba (7912)]

 

 

Share