09-Kitaab At-Tawhiyd: Kutabaruku Kwa Mti Au Jiwe Na Vitu Kama Hivyo

Mlango Wa 9

بَابُ مَنْ تَبَرَّكَ بِشَجَرٍ أَوْ حَجَرٍ وَنَحْوِهِمَا

Kutabaruku Kwa Mti Au Jiwe Na Vitu Kama Hivyo

 


 

وَقَوْلِ اَللَّهِ تَعَالَى:

Na kauli ya Allaah Ta’aalaa:

أَفَرَأَيْتُمُ اللَّاتَ وَالْعُزَّىٰ ﴿١٩﴾

((Je, mmeona Laata na ‘Uzzaa?))

 

وَمَنَاةَ الثَّالِثَةَ الْأُخْرَىٰ ﴿٢٠﴾

((Na Manaata mwengine wa tatu?))

 

أَلَكُمُ الذَّكَرُ وَلَهُ الْأُنثَىٰ ﴿٢١﴾

((Je, nyinyi mna wana wa kiume Naye Ana wana wa kike?))

 

تِلْكَ إِذًا قِسْمَةٌ ضِيزَىٰ ﴿٢٢﴾

((Hiyo basi hapo ni mgawanyo wa dhulma kubwa!))

 

إِنْ هِيَ إِلَّا أَسْمَاءٌ سَمَّيْتُمُوهَا أَنتُمْ وَآبَاؤُكُم مَّا أَنزَلَ اللَّـهُ بِهَا مِن سُلْطَانٍ ۚ إِن يَتَّبِعُونَ إِلَّا الظَّنَّ وَمَا تَهْوَى الْأَنفُسُ ۖ وَلَقَدْ جَاءَهُم مِّن رَّبِّهِمُ الْهُدَىٰ ﴿٢٣﴾

((Hayo si chochote isipokuwa ni majina mmeyaita nyinyi na baba zenu, wala Allaah Hakuyateremshia dalili yoyote. Hawafuati isipokuwa dhana na yale yanayotamani nafsi (zao), na hali imekwishawajia kutoka kwa Rabb wao mwongozo)) [An-Najm (53: 19-23)]

 

عن أَبِي وَاقٍد اللَّيْثِيِّ (رضي الله عنه) قَالَ: خَرَجْنَا مَعَ النَّبِيِّ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وآله وَسَلَّمَ) إِلَى حُنَيْنٍ وَنَحْنُ حُدَثَاءُ عَهْدٍ بِكُفْرٍ، وَلِلِمُشْرِكِينَ سِدْرَةٌ، يَعْكُفُونَ عِنْدَهَا وَيُنَوِّطُونَ بِهَا أَسْلِحَتَهُمْ، يُقَالَ لَهَا ذَاتُ أَنْوَاطٍ، فَمَرَرْنَا بِسِدْرَةٍ فَقُلْنَا: يَا رَسُولَ اللهِ اجْعَلْ لَنَا ذَاتَ أَنْوَاطٍ كَمَا لَهُمْ ذَاتُ أَنْوَاط. فَقَالَ النَّبِيُّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم): ((الله أكبر! هَذَا كَمَا قَالَ قَوْمُ مُوسَى "اجْعَلْ لَنَا إِلَهًا كَمَا لَهُمْ آلِهَةٌ" وَالَّذِي نَفْسِي بِيَدِهِ لَتَرْكَبُنَّ سُنَّةَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Waaqid Al-Laythiyy(رضي الله عنه)  amesema: “Tulitoka pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwenda [vitani] Hunayn nasi ndio kwanza tumetoka katika ukafiri, na washirikina walikuwa na mkunazi wanaufanyia ‘ibaadah na walikuwa wakitundika silaha zao [kupata Baraka]. Wakiuita ‘Dhaatu Anwaatw’. Tukapita mbele ya mkunazi tukasema: “Ee Rasuli wa Allaah, tufanyie nasi dhaata-anwaatw kama walivyokuwa nao [makafiri] dhaatu-anwaatw” Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: ((Allaahu Akbar!  Hivi ni kama walivyosema watu wa Muwsaa “Tufanyie nasi muabudiwa kama walivyokuwa nao waabudiwa” Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, mtafuata nyendo za walio kabla yenu [za ujahili na kufru])) [At-Tirmidhiy na ameikiri ni Swahiyh]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah An-Najm (53:19, 20).

 

2-Kujua kiini cha jambo walilolitaka Maswahaba (kuhusu kuweka mti kama wa dhaat anwaatw).

 

3-Maswahaba hawakutekeleza walichoomba.

 

4-Niyyah yao ilikuwa kujikuruibisha kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa kuomba huko, wakidhani kuwa Atalipenda hilo.

 

5-Ikiwa (Maswahaba رضي الله عنهم) hawakujua kosa hilo, wengineo ni wepesi zaidi kutokulijua kosa hilo (na kuingia katika shirki).

 

6- (Maswahaba رضي الله عنهم) wana malipo mema na walikuwa na ahadi ya kughufuriwa jambo ambalo wengineo hawana.

 

7- Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuwapa udhuru kwa hili, bali aliwakanushia kwa kusema, ((Allaahu Akbar!  Hivi ni kama… na mtafuata nyendo za walio kabla yenu…)) Hivyo alidhihirisha uzito wake kwa mambo hayo matatu.

 

8-Lililo muhimu katika jambo hili ni fundisho lililokusudiwa kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alifananisha ombii lao na ombi la wana wa Israaiyl pindi walipomuomba Muwsaa, “Tufanyie muabudiwa.”

 

9-Kukanushwa ombi hilo ni maana ya laa ilaaha illaa Allaah, ambayo juu ya kuwa ni adhimu, iliwifachikia na hawakuhisi. 

 

10-Kuapa kwa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alipotowa hukmu, na haapi isipokuwa kwa manufaa.

 

11-Shirki inaweza kuwa ndogo au kubwa, kwa sababu Maswahaba hawakuritadi kwa ombi lao.

 

12-Kauli yao, “ndio kwanza tumetoka katika ukafiri” inatujulisha kwamba Maswahaba wengineo hawakuwa wajinga wa hilo.

 

13-Kutamka Takbiyr inaweza kuwa ni kuashiria jambo la kustaajabu, kinyume na wanavyodhania wengine (kuwa ni makruuh). 

 

14-Kufunga njia zote zinazopeleka kwenye shirki.

 

15-Kukatazwa kuwaiga watu wa Jaahiliyyah.

 

16-Mwalimu anaweza kuwa na hasira anapofundisha wanafunzi wake (kwa ajili ya kukosoa jambo ovu).

 

17-Kanuni ya jumla katika maendeleo ya mwana Aadam na kufanana kwa mawazo, imedhihirishwa katika kauli yake, ((Hizi ni njia [Sunan])).

 

18-Ni alama ya Unabiy, kwa sababu imetokea sawa na alivyojulisha.

 

19-Kile walichokemewa Mayahudi na Wakristo katika Qur-aan kimekemewa kwetu pia.

 

20-Maswahaba رضي الله عنهم walitambua kwamba matendo ya ‘ibaadah yamejengwa kwa msingi wa wazi kabisa; (‘fanya!’, ‘acha!’) Ndipo kukawa na ukumbusho kuhusu anapoulizwa kaburini; “Ni nani Rabb wako?” Hilo liko wazi. Na kuhusu “Nani Nabiy wako?” Hilo linatokana na Wahyi wa khabari za mambo ya ghaibu. Lakini kuhusu “Ni ipi Dini yako?” basi hilo linahusu ombi lao (Mayahudi kwa Muwsaa), “Tufanyie muabudiwa…” mpaka mwisho.

 

21-Desturi za Ahlul-Kitaab zinakanushwa sawa na za washirikina.

 

22-Aliyetoka katika upotofu baada ya kwishauzoea, (akaingia Uislamu) hajasalimika kabisa na itikadi hizo. Hii ni kutokana na kauli yao, “Nasi ndio kwanza tumetoka katika ukafiri.”

 

 

 

 

Share