13-Kitaab At-Tawhiyd: Kuomba Kinga Kwa Asiyekuwa Allaah Ni Shirki

Mlango Wa 13

بَابٌ مِنَ الشِّرْكِ الِاسْتِعَاذَةُ بِغَيْرِ اللهِ

Kuomba Kinga Kwa Asiyekuwa Allaah Ni Shirki


 

وَقَوْلُ اَللَّهِ تَعَالَى:

Na kauli ya Allaah Ta’aalaa:

 

وَأَنَّهُ كَانَ رِجَالٌ مِّنَ الْإِنسِ يَعُوذُونَ بِرِجَالٍ مِّنَ الْجِنِّ فَزَادُوهُمْ رَهَقًا ﴿٦﴾

((“Na kwamba walikuwa wanaume miongoni mwa wana Aadam wanajikinga na wanaume miongoni mwa majini, basi wakawazidishia madhambi, uvukaji mipaka ya kuasi na khofu”)) [Al-Jinn (72: 6)]

 

عن خَوْلَةَ بِنْتَ حَكِيمٍ (رضي الله عنها) قالت: سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ:  ((مَنْ نَزَلَ مَنْزلاَ ثُمَّ قَالَ: "أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللَّهِ التَّامَّاتِ مِنْ شَرِّ مَا خَلَقَ" لَمْ يَضُرَّهُ شَيْءٌ حَتَّى يَرْتَحِلَ مِنْ مَنْزِلِهِ ذَلِكَ)) رواه مسلم

Imepokelewa kutoka kwa Khawlah bint Hakiym(رضي الله عنها)  kwamba kamsikia Nabiy (صلى الله عليه وسلم) akisema: ((Atakayefikia mahali kisha akasema: A’uwdhu bikalimati-LLaahit-taammati min sharri maa Khalaq' - Najilinda kwa maneno ya Allaah yaliyotimia na shari ya Alichokiumba-  hakuna kitakachomdhuru hadi atakapoondoka mahali pake hapo)) [Muslim]

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Melezo ya Aayah katika Suwratul-Jinn.

 

2-Kuomba ulinzi kwa asiyekuwa Allaah (سبحانه وتعالى) ni shirki.

 

3-Hii imeungwa mkono na Hadiyth kwa vile Wanachuoni huitumia kuthibitisha kuwa maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى) (yaani Qur’aan) hayakuumbwa kwani yangelikuwa yameumbwa, tusingelitakiwa kujikinga kwa maneno ya Allaah (سبحانه وتعالى), wakasema kuwa kujikinga kwa viumbe ni shirki.

 

4-Fadhila ya du’aa hii japokuwa ni fupi.

 

5-Licha ya ukweli kuwa jambo linaweza kuongoza kwenye manufaa ya kiduna kama kuzuia madhara au kupata manufaa, lakini hilo halithibitishi kuwa silo la shirki.

 

 

 

Share