28-Kitaab At-Tawhiyd: Itikadi Ya Tatwayyur (Kutabiri Nuksi, Mikosi Na Kadhaalika)

Mlango Wa 28

بَابُ مَا جَاءَ فِي التَّطَيُّرِ

Itikadi Ya Tatwayyur  (Kutabiri Nuksi, Mikosi Na Kadhaalika)


 

 

وَقَوْلِ اَللَّهِ تَعَالَى:

Na kauli ya Allaah Ta’aalaa:

 

  أَلَا إِنَّمَا طَائِرُهُمْ عِندَ اللَّـهِ وَلَـٰكِنَّ أَكْثَرَهُمْ لَا يَعْلَمُونَ ﴿١٣١﴾

((Tanabahi! Hakika nuksi yao iko kwa Allaah lakini wengi wao hawajui)) [Al-A’raaf (7: 131)]

 

At-Tatwayyur:  Itikadi za ushirikina kutabiri na kuamini mkosi, nuksi, dhana mbaya n.k.  

وَقَوْلِهِ:

Na kauli Yake:

قَالُوا طَائِرُكُم مَّعَكُمْ ۚ أَئِن ذُكِّرْتُم ۚ بَلْ أَنتُمْ قَوْمٌ مُّسْرِفُونَ ﴿١٩﴾

((Rusuli) Wakasema: “Nuksi yenu mnayo wenyewe. Je, kwa vile mnakumbushwa? Bali nyinyi ni watu wapindukao mipaka”)) [Yaasiyn (36: 19)]

 

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((لاَ عَدْوَى وَلاَ طِيَرَةَ وَلَا هَامَةَ وَلاَ صَفَرَ)) أَخْرَجَاهُ  زَادَ مُسْلِمٌ: ((وَلا نَوْءَ وَلا غُولَ))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hakuna ‘adwaa wala twiyarah wala hakuna haamah wala hakuna swafar))  [Al-Bukhaariy na Muslim] Na Muslim amezidisha: ((Wala hakuna naw-a wala hakuna ghuwl))

 

‘Adwaa:     Uambukizaji wa magonjwa bila idhini ya Allaah.

 

Haamah:    Ukorofi, mkosi unaotokana na bundi - ndege wa usiku.

 

Swafar:      Ukorofi, mkosi unaodaiwa unatoka katika mwezi wa Swafar.

 

An-Naw-a: Kilima – ugawanyaji wa wakati kwa mujibu wa kujitokeza nyota au

                     sayari fulani.

 

Ghuwl:     Mizimu. 

 

وَلَهُمَا عَنْ أَنَسٍ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((لَا عَدْوَى وَلَا طِيَرَةَ وَيُعْجِبُنِي الْفَأْلُ))  قَالُوا:  وَمَا الْفَأْلُ؟ قَالَ: ((الْكَلِمَةُ الطَّيِّبَةُ))

Na wawili hao [Al-Bukhaariy na Muslim] wamesimulia kutoka kwa Anas(رضي الله عنه)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hakuna ‘adwaa wala hakuna twiyarah [itikadi ya kutabiri mkosi, nuksi] na inanipendekeza Al-Fa-l)) Wakauliza: Nini Al-Fa-lu? Akajibu: ((Neno zuri)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

وَلأَبِي دَاوُدَ بِسَنَدٍ صَحِيحٍ: عَنْ عُقْبَةَ بْنِ عَامِرٍ قَالَ: ذُكِرَتِ الطِّيَرَةُ عِنْدَ رَسُولِ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) فَقَالَ: ((أَحْسَنُهَا الْفَأْلُ، وَلاَ تَرُدُّ مُسْلِمًا. فَإِذَا رَأَى أَحَدُكُمْ مَا يَكْرَهُ فَلْيَقُلْ: اللَّهُمَّ لاَ يَأْتِي بِالْحَسَنَاتِ إِلاَّ أَنْتَ وَلاّ يَدْفَعُ السَّيِّئَاتِ إِلاَّ أَنْتَ، وَلاَ حَوْلَ وَلاَ قُوَّةَ إِلاَّ بِكَ))

Na kwa Abuu Daawuwd, kwa isnaad Swahiyh: Imepokelewa kutoka kwa ‘Uqbah bin ‘Aamir (رضي الله عنه) amesema: Kuliwahi kutajwa mbele ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) Atw-Twiyarah (itikadi ya kutabiri na kuamini kitu fulani kuwa kinaleta mkosi, nuksi), akasema: ((Lililo bora katika hayo ni Al-Fa-lu. Vinginevyo hayo yote hayamuzuilii Muislamu kutafuta malengo yake. [kutokutenda aliloazimia]. Mmmoja wenu atakapoona analochukia aseme: “Allaahumma laa ya-tiy bil-hasanaati illaa Anta, walaa yad-fa’us-sayyiaat illa Anta, walaa hawla walaa quwwata illaa Bika - Ee Allaah, hakuna anayeweza kuleta mambo mema isipokuwa ni Wewe, wala hakuna anayeweza kukinga mabaya isipokuwa ni Wewe. Na Hakuna uwezo wala nguvu ila kutokana Nawe)) [Hadiyth Swahiyh ameipokea Abuu Daawuwd kwa isnaad Swahiyh]

 

Al-Fa-lu: Matumaini na itikadi kuwa jambo hutokea kwa idhini ya Allaah (سبحانه وتعالى).

 

وعن ابْنِ مَسْعُودٍ مَرْفُوعًا: ((الطِّيَرَةُ شِرْكٌ، الطِّيَرَةُ شِرْكٌ، وَمَا مِنَّا إِلاَّ وَلَكِنَّ اللَّهَ يُذْهِبُهُ بِالتَّوَكُّلِ)) رَوَاهُ أَبُو دَاوُدَ وَالتِّرْمِذِيُّ وَصَحَّحَهُ. وَجَعَلَ آخِرَهُ مِنْ قَوْلِ ابْنِ مَسْعُودٍ

Na kutoka kwa Ibn Mas’uwd ni Hadiyth Marfuw’: ((Atw-Twiyarah ni shirki, Atw-Twiyarah ni shirki. Na hakuna yeyote miongoni mwetu asiyehisi jambo moyoni [Kuhusu Atw-Twiyarah] lakini Allaah Huiondoa kwa kutawakali Kwake)) [Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth hii Hasan Swahiyh] Na imetajwa kwamba kauli ya mwisho ni ya Ibn Mas’uwd.

 

وَلأَحْمَدَ مِنْ حَدِيثِ ابْنِ عَمْرِو: ((مَنْ رَدَّتْهُ الطِّيَرَةُ عَنْ حَاجَتِهِ، فَقَدْ أَشْرَكَ)) قَالُوا: فَمَا كَفَّارَةُ ذَلِكَ؟ قَالَ: ((أَنْ يَقُولَ اللَّهُمَّ لاَ خَيْرَ إِلاَّ خَيْرُكَ، وَلاَ طَيْرَ إِلاَّ طَيْرُكَ، وَلاَ إِلَهَ غَيْرُكَ))

Na Imaam Ahmad amesimuila Hadiyth ya Ibn ‘Amr: ((Atakayerudi nyuma pasina na kuitekeleza haja yake kwa sababu ya Atw-Twiyarah [itikadi ya kutabiri mkosi, nuksi] amefanya shirki)) Wakuliza: Basi nini kafara yake? Akajibu: ((Aseme: Allaahumma laa khayra illa khayruka, wa laa Twayra illa twayruka, wa laa ilaaha ghayruka – Ee Allaah, hakuna khayr ila Uiletayo Wewe, wala hakuna ubaya ila Ulioukadiria Wewe, na hapana muabudiwa wa haki zaidi Yako)) [Ahmad]

 

وَلَهُ مِنْ حَدِيثِ الْفَضْلِ بْنِ عَبَّاسٍ: ((إِنَّمَا الطِّيَرَةُ مَا أَمْضَاكَ أَوْ رَدَّكَ))

Naye [Imaam Ahmad] pia amesimulia Hadiyth: ((Hakika mtu huhukumiwa kwa dhambi za Atw-Twiyarah inapompelekea kufanya au kujizuia na jambo [aliloazimia kulitenda])) [Ahmad]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Kukumbusha maana ya Aayah:

 

أَلَا إِنَّمَا طَائِرُهُمْ عِندَ اللَّـهِ

((Tanabahi!  Hakika nuksi yao iko kwa Allaah))

            na:

طَائِرُكُم مَّعَكُمْ ۚ

((Nuksi yenu mnayo wenyewe))

 

2-Kukanusha kwamba maradhi yaweza kumsibu mtu bila ya idhini ya Allaah.

 

3-Kukanusha (At-Twiyarah) – Itikadi kuwa mtu aweza kudhuriwa na mkosi, nuksi isiyokuwa katika Qadhwaa na Qadar ya Allaah.  

 

4-Kukanusha kwa haamah (nuksi inayotokana na bundi)

 

5-Kukanusha kuwa mwezi wa Swafar ni mwezi wa nuksi.

 

6-Al-Fa-al haijakatazwa, bali ni mustahabb - inapendekezwa.

 

7-Ufafanuzi wa Al-Fa-al kwa kirefu.

 

8-Hakuna ubaya ikiwa mashaka hayo yataingia katika nyoyo ilhali mtu anachukia. Bali Allaah (سبحانه وتعالى) Atamhifadhi mtu huyo kwa sababu ya kutawakali Kwake kwa dhati kabisa.

 

9-Du’aa ya kusoma ikiwa mtu atapata hisia za namna hiyo.

 

10-Kutajwa kwamba Atw-Twiyarah ni shirki.

 

11-Ufafanuzi wa Atw-Twiyarah iliyoharamishwa.

 

 

Share