30-Kitaab At-Tawhiyd: Kutafuta Mvua Kwa Manazili Ya Mwezi Na Nyota

Mlango Wa 30

بَابُ مَا جَاءَ فِي الِاسْتِسقَاءِ بِالْأَنْوَاءِ

Kutafuta Mvua Kwa Manazili Ya Mwezi Na Nyota


 

 

وَقَوْلِ اَللَّهِ تَعَالَى: 

Na kauli ya Allaah Ta’aalaa: 

وَتَجْعَلُونَ رِزْقَكُمْ أَنَّكُمْ تُكَذِّبُونَ ﴿٨٢﴾

((Na mnafanya badala (shukurani za) riziki zenu kuwa nyinyi mnakadhibisha)) [Al-Waaqi’ah (56: 82)]

 

وَعَنْ أَبِي مَالِكٍ الأَشْعَرِيِّ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((أَرْبَعٌ فِي أُمَّتِي مِنْ أَمْرِ الْجَاهِلِيَّةِ لاَ يَتْرُكُونَهُنَّ: الْفَخْرُ بِالأَحْسَابِ وَالطَّعْنُ فِي الأَنْسَابِ وَالاسْتِسْقَاءُ بِالنُّجُومِ وَالنِّيَاحَةُ))

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Maalik Al-Ash’ariyyi (رضي الله عنه)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Mambo manne katika Ummah wangu ni miongoni mwa mambo ya kijaahiliyyah na hawayaachi; kujifakharisha kwa unasaba na mafaniko yao, kutukanana kwa nasabu, kutafuta mvua kwa nyota kuomboleza)) [Muslim]

 

وَقَال: ((النَّائِحَةُ إِذَا لَمْ تَتُبْ قَبْلَ مَوْتِهَا تُقَامُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَعَلَيْهَا سِرْبَالٌ مِنْ قَطِرَانٍ وَدِرْعٌ مِنْ جَرَبٍ)) رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Na akasema (صلى الله عليه وآله وسلم): ((Mwombolezi asipotubia kabla ya kufa kwake, Siku ya Qiyaamah atavalishwa kanzu ya shaba iliyoyeyuka na joho la upele [wa ukoma])) [Muslim]

 

وَلَهُمَا عَنْ زَيْدِ بْنِ خَالِدٍ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) قَالَ: صَلَّى لَنَا رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) صَلاةَ الصُّبْحِ بِالْحُدَيْبِيَةِ عَلَى إِثْرِ سَمَاءٍ كَانَتْ مِنَ اللَّيْلِ،  فَلَمَّا انْصَرَفَ أَقَبْلَ عَلَى النَّاسِ فَقَالَ: ((هَلْ تَدْرُونَ مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ؟)) قَالُوا: اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمَ. قَالَ: ((قَالَ أَصْبَحَ مِنْ عِبَادِي مُؤْمِنٌ بِي وَكَافِرٌ، فَأَمَّا مَنْ قَالَ مُطِرْنَا بِفَضْلِ اللَّهِ وَرَحْمَتِهِ، فَذَلِكَ مُؤْمِنٌ بِي كَافِرٌ بِالْكَوْكَبِ، وَأَمَّا مَنْ قَالَ مُطِرْنَا بِنَوْءِ كَذَا وَكَذَا، فَذَلِكَ كَافِرٌ بِي مُؤْمِنٌ بِالْكَوْكَبِ))

Imepokelewa kutoka kwa Zayd bin Khaalid (رضي الله عنه)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alituswalisha Swalaah ya asubuhi Hudaybiyah baada ya usiku wa mvua. Alipomaliza akawakabili watu akasema: ((Je, mnajua Rabb wenu Amesema nini?)) Wakajibu: “Allaah na Rasuli Wake ndio wajuao.” Akasema: ((Allaah Amesema: Baadhi ya waja Wangu wameamka leo wakiwa wenye kuniamini, na wengine wamekufuru. Aliyesema kuwa mvua ni kutokana na fadhila na rahmah za Allaah, basi huyo ni mwenye kuniamini wala haamini nyota. Ama aliyesema: Tumenyeshewa mvua kutokana na nyota fulani, yeye ni mwenye kunikufuru na mwenye kuamini nyota)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

وَلَهُمَا مِنْ حَدِيثِ ابْنِ عَبَّاسٍ مَعْنَاهُ وَفِيهِ: قَالَ بَعْضُهُمْ لَقَدْ صَدَقَ نَوْءَ كَذَا وَكَذَا فَأَنْزَلَ اللَّهُ هَذِهِ الآيَاتِ:

Nao wawili (Al-Bukhaariy na Muslim) wamerekodi Hadiyth ya Ibn ‘Abbaas(رضي الله عنهما)  kama hiyo na nyongeza kwamba: “Wakasema baadhi yao kwamba imenyesha mvua kwa sababu ya nyota kadhaa wa kadhaa”, kisha Allaah Akateremsha Aayah zifuatazo:

 

فَلَا أُقْسِمُ بِمَوَاقِعِ النُّجُومِ ﴿٧٥﴾

((Basi Naapa kwa maangukio ya nyota))

 

وَإِنَّهُ لَقَسَمٌ لَّوْ تَعْلَمُونَ عَظِيمٌ ﴿٧٦﴾

((Na hakika hicho ni kiapo adhimu lau mngelijua))

 

إِنَّهُ لَقُرْآنٌ كَرِيمٌ ﴿٧٧﴾

((Hakika hii bila shaka ni Qur-aan kariym, tukufu))

 

فِي كِتَابٍ مَّكْنُونٍ ﴿٧٨﴾

((Katika Kitabu kilichohifadhiwa))

 

لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ ﴿٧٩﴾

((Haigusi isipokuwa waliotakaswa kabisa)

 

تَنزِيلٌ مِّن رَّبِّ الْعَالَمِينَ ﴿٨٠﴾

((Ni uteremsho kutoka kwa Rabb wa walimwengu))

 

أَفَبِهَـٰذَا الْحَدِيثِ أَنتُم مُّدْهِنُونَ ﴿٨١﴾

Je, kwa maneno haya nyinyi ni wenye kuikanusha na kuibeza?

 

وَتَجْعَلُونَ رِزْقَكُمْ أَنَّكُمْ تُكَذِّبُونَ ﴿٨٢﴾

((Na mnafanya badala (shukurani za) riziki zenu kuwa nyinyi mnakadhibisha)) [Al-Waaqi’ah (56:75-82)]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah Al-Waaqi’ah (56: 75-82).

 

2-Desturi nne mbaya za kipindi cha jaahiliyyah (kabla ya Uislamu).

 

3-Kufr zilizomo katika baadhi ya desturi hizo.

 

4-Baadhi ya matendo ya kufru hayamtoi mtu katika Uislamu.

 

5-Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

((أَصْبَحَ مِنْ عِبَادِي مُؤْمِنٌ بِي وَكَافِرٌ))

((Baadhi ya waja Wangu wameamka leo wakiwa wenye kuniamini, na wengine wamekufuru)).

 

kwa sababu ya neema, rahmah (ya mvua) waliyoteremshiwa.

 

6-Umuhimu wa iymaan katika mazingira hayo.

 

7-Kudhihiri kufru katika hali kama hizo.

 

8-Ukumbusho kuhusu usemi wao: “Tumepata mvua kwa sababu ya nyota kadhaa”

 

9-Njia ya kuwafundisha wanafunzi kwa maswali katika kueleza jambo kama Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alivyosema: ((Je, mnajua Rabb wenu Amesema nini?)).

 

10-Adhabu waliyoandaliwa wenye kuomboleza kwa sauti msibani.

 

 

 

 

Share