31-Kitaab At-Tawhiyd: Kumpenda Allaah Na Rasuli Wake Kuliko Nafsi Yako Au Yeyote Yule

Mlango Wa 31

باب: وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ

Kumpenda Allaah Na Rasuli Wake Kuliko Nafsi Yako Au Yeyote Yule


 

 

قَوْلِ اللَّهِ تَعَالَى:

Na kauli Yake Ta’aalaa:

((وَمِنَ النَّاسِ مَن يَتَّخِذُ مِن دُونِ اللَّـهِ أَندَادًا يُحِبُّونَهُمْ كَحُبِّ اللَّـهِ ۖ وَالَّذِينَ آمَنُوا أَشَدُّ حُبًّا لِّلَّـهِ ۗ ))

((Na miongoni mwa watu wako wenye kuchukua asiyekuwa Allaah na kuwafanya kuwa ni wanaolingana (na Allaah) wanawapenda kama kumpenda Allaah. Na wale walioamini wana mapenzi zaidi kwa Allaah)) [Al-Baqarah (2: 165)]  

وَقَوْلِهِ:

Na kauli Yake:

 

قُلْ إِن كَانَ آبَاؤُكُمْ وَأَبْنَاؤُكُمْ وَإِخْوَانُكُمْ وَأَزْوَاجُكُمْ وَعَشِيرَتُكُمْ وَأَمْوَالٌ اقْتَرَفْتُمُوهَا وَتِجَارَةٌ تَخْشَوْنَ كَسَادَهَا وَمَسَاكِنُ تَرْضَوْنَهَا أَحَبَّ إِلَيْكُم مِّنَ اللَّـهِ وَرَسُولِهِ وَجِهَادٍ فِي سَبِيلِهِ فَتَرَبَّصُوا حَتَّىٰ يَأْتِيَ اللَّـهُ بِأَمْرِهِ ۗ  

((Sema: “Ikiwa baba zenu na watoto wenu na ndugu zenu na wake (au waume) zenu na jamaa zenu na mali mliyoichuma na biashara mnayoikhofia kuharibika kwake, na majumba mnayoridhika nayo, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Allaah na Rasuli Wake na kufanya jihaad katika njia Yake; basi ngojeeni mpaka Allaah Alete Amri Yake (ya adhabu)) [At-Tawbah (9: 24)]

 

عَنْ أَنَسٍ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((لاَ يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى أَكُونَ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ وَلَدِهِ وَوَالِدِهِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ)) أَخْرَجَاهُ

Imepokelewa kutoka kwa Anas (رضي الله عنه) kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Haamini mmoja wenu mpaka anipende mimi kuliko watoto wake na baba yake na watu wote)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

وَلَهُمَا عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ): ((ثَلاثٌ مَنْ كُنَّ فِيهِ وَجَدَ بِهِنَّ حَلاوَةَ الإِيمَانِ: أَنْ يَكُونَ اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَحَبَّ إِلَيْهِ مِمَّا سِوَاهُمَا، وَأَنْ يُحِبَّ الْمَرْءَ لاَ يُحِبُّهُ إِلاَّ لِلَّهِ، وَأَنْ يَكْرَهَ أَنْ يَعُودَ فِي الْكُفْرِ بَعْدَ إِذْ أَنْقَذَهُ اللَّهُ مِنْهُ  كَمَا يَكْرَهُ أَن ْيُقْذَفَ فِي النَّار))

Nao Al-Bukhaariy na Muslim wamerekodi Hadiyth kutoka kwake Anas(رضي الله عنه)  amesema: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Mambo matatu atakayekuwa nayo, atapata utamu wa Iymaan: Allaah na Rasuli Wake wawe vipenzi zaidi kwake kuliko wengineo, ampende mtu na wala asimpende isipokuwa kwa ajili ya Allaah, na achukie kurudi katika ukafiri baada ya Allaah kumwokoa kutoka huko kama anavyochukia kuingizwa motoni)) [Al-Bukhaariy na Muslim]  

وَفِي رِوَايَة:َ ((لاَ يَجِدُ أَحَدٌ حَلاوَةَ الإِيمَانِ حَتَّى...)) إِلَى آخِرِهِ

Katika riwaayah: ((Hatopata mtu utamu wa iymaan mpaka …)) mpaka mwisho wa Hadiyth

 

وَعَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ قَالَ: مَنْ أَحَبَّ فِي اللَّهِ وَأَبْغَضَ فِي اللَّهِ، وَوَالَى فِي اللَّهِ، وَعَادَى فِي اللَّهِ، فَإِنَّمَا تُنَالُ وِلايَةُ اللَّهِ بِذَلِكَ، وَلَنْ يَجِدَ عَبْدٌ طَعْمَ الإِيمَانِ وَإِنْ كَثُرَتْ صَلاتُهُ وَصَوْمُهُ  حَتَّى يَكُونَ كَذَلِكَ، وَقَدْ صَارَتْ عَامَّةُ مُؤَاخَاةِ النَّاسِ عَلَى أَمْرِ الدُّنْيَا، وَذَلِكَ لاَ يُجْدِي عَلَى أَهْلِهِ شَيْئًا  - رَوَاهُ ابْنُ جَرِيرٍ

Na Imepokelewa kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amesema: Anayependa kwa ajili ya Allaah, na akachukia kwa ajili ya Allaah, na akafanya urafiki kwa ajili ya Allaah, akafanya uadui kwa ajili ya Allaah, kwa sifa hizo, ndipo hupatikana urafiki wa Allaah. Na wala mja hatoonja utamu wa iymaan hata kama zikikithiri Swalaah zake, na Swawm zake, ila awe katika sifa hizo. Aghlabu ya urafiki wa watu ni sababu ya maslahi ya kidunia. Lakini hilo halitowafaidisha kitu (Aakhirah). [Ibnu Jariyr]

 

وَقَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ فِي قَوْلِهِ تَعَالَى: ((وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ الْأَسْبَابُ)) قَالَ: الْمَوَدَّةُ

Na akasema Ibn ‘Abbaas kuhusu kauli Yake Ta’aalaa: ((na yatawakatikia mafungamano yao)) [Al-Baqarah (2:166)]. Amesema mafungamano hapa yamaanisha upendo.

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah Al-Baqarah (2: 165).

 

2- Tafsiri ya Aayah katika Suwrah At-Tawbah (9: 24).

 

3-Lazima tumpende Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kuliko nafsi zetu, familia zetu na mali zetu.

 

4-Kutokuwa na Iymaan (katika Hadiyth: “Haamini mmoja wenu mpaka …” hakumaanishi ni kutoka nje ya Uislamu.

 

5-Iymaan ina ladha, yaani wakati mwengine Muumini hupata ladha yake na wakati mwengine hapati ladha.

 

6-Hakuna anayeweza kupata urafiki wa Allaah (سبحانه وتعالى) na ladha ya iymaan isipokuwa tu anapokuwa na ‘amali nne moyoni: (1) Kupenda kwake kwa ajili ya Allaah; (2) Kuchukia kwake kwa ajili ya Allaah; (3) Urafiki wake kwa ajili ya Allaah; (4) Uadui wake kwa ajili ya Allaah.

 

7-Ufahamu wa Maswahaba kwamba ghalibu ya mafungamano ya watu na usuhuba ni kwa ajili ya maslahi ya kidunia.

 

8-Tafsiri ya Aayah:

وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ الْأَسْبَابُ

((na yatawakatikia mafungamano yao)).

 

9-Hata baadhi ya washirikina humpenda sana Allaah (سبحانه وتعالى).

 

10-Tishio la adhabu kwa mtu anayependa "mambo manane" zaidi kuliko Dini yake. “Mambo manane” ni:  (1) wazee wake (2) kizazi chake (3) ndugu zake (4) mume au mke wake (5) ukoo wake (6) mali yake (7) biashara yake (8) maskani yake. 

 

11-Yeyote anayemfanyia Allaah (سبحانه وتعالى) washirika na kumpenda huyo mshirika kama pendo lake kwa Allaah (سبحانه وتعالى), basi hivyo ni shirki kuu.

 

Share