34-Kitaab At-Tawhiyd: Kuhisi Amani Dhidi Ya Mipango Ya Allaah Ni Kinyume Na Tawhiyd

Mlango Wa 34

باب:  أَفَأَمِنُوا مَكْرَ اللَّـهِ ۚ فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْخَاسِرُونَ

Kuhisi Amani Dhidi Ya Mipango Ya Allaah (Ya Adhabu Zake) Ni Kinyume Na Tawhiyd


قَوْلِ اَللَّهِ تَعَالَى:

Kauli Yake Ta’aalaa:

 

 أَفَأَمِنُوا مَكْرَ اللَّـهِ ۚ فَلَا يَأْمَنُ مَكْرَ اللَّـهِ إِلَّا الْقَوْمُ الْخَاسِرُونَ ﴿٩٩﴾

((Je, wameaminisha mipango ya Allaah? Basi hawaaminishi mipango ya Allaah isipokuwa watu wenye kukhasirika)) [Al-A’raaf (7: 99)]

وَقَوْلِهِ

Na kauli Yake:

  وَمَن يَقْنَطُ مِن رَّحْمَةِ رَبِّهِ إِلَّا الضَّالُّونَ ﴿٥٦﴾

 

((Na nani anayekata tamaa na rahmah ya Rabb wake isipokuwa wapotofu)) [Al-Hijr (15: 56)]

 

وَعَنِ اِبْنِ عَبَّاسٍ أَنَّ رَسُولَ اَللَّهِ (صَلَّى اَللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) سُئِلَ عَنِ الْكَبَائِرِ؟ فَقَالَ: ((اَلشِّرْكُ بِاَللَّهِ، وَالْيَأْسُ مِنْ رَوْحِ اَللَّهِ، وَالأَمْنُ مِنْ مَكْرِ اَللَّهُ))

Na kutoka kwa Ibn ‘Abbaas(رضي الله عنهما)  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliulizwa kuhusu madhambi makubwa. Akasema: ((Kumshirikisha Allaah, na kukata tamaa na faraja ya Allaah, na kuaminisha mpango wa Allaah [ya adhabu])) [Al-Bayhaqiy katika Majma’ Az-Zawaaid, Al-Bazaar, Atw-Twabaraaniy]

 

وَعَنِ اِبْنِ مَسْعُودٍ قَالَ: ((أَكْبَرُ الْكَبَائِرِ الإِشْرَاكُ بِاَللَّهِ، وَالأَمْنُ مِنْ مَكْرِ اَللَّهِ، وَالْقُنُوطُ مِنْ رَحْمَةِ اَللَّهِ، وَالْيَأْسُ مِنْ رَوْحِ اَللَّهِ)) رَوَاهُ عَبْدُ اَلرَّزَّاقِ

Na kutoka kwa Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه)  amesema: ((Madhambi makubwa zaidi ni kumshirikisha Allaah, na kuaminisha mipango ya Allaah [ya adhabu Zake], na kukata tamaa Rahmah ya Allaah, na kuvunjika tamaa na faraja ya Allaah)) [‘Abdur-Razaaq]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah Al-A’raaf (7: 99).

 

2-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah Al-Hijr (15: 56).

 

3-Ukali wa adhabu iliyoahidiwa kwa anayedhani kuwa amesalimika na adhabu za Allaah (سبحانه وتعالى).

 

4-Adhabu kali iliyoahidiwa kwa anayekata tamaa na rahmah za Allaah (سبحانه وتعالى).

 

 

 

 

Share