35-Kitaab At-Tawhiyd: Kuvumilia Maqadario Ya Allaah Ni Miongoni Mwa Iymaan

 

Mlango Wa 35

بَابٌ مِنَ الْإِيمَانِ بِاللَّهِ الصَّبْرُ عَلَى أَقْدَارِ اللَّهِ

Kuvumilia Maqadario Ya Allaah Ni Miongoni Mwa Iymaan

 


 

 

وَقَوْلُ اَللَّهِ تَعَالَى:

Na kauli ya Allaah Ta’aalaa:

وَمَن يُؤْمِن بِاللَّـهِ يَهْدِ قَلْبَهُ

((Na yeyote   anayemuamini Allaah, (Allaah) Huuongoza moyo wake)) [At-Taghaabun (64: 11)]

 

قَالَ عَلْقَمَةُ: هُوَ الرَّجُلُ تُصِيبُهُ الْمُصِيبَةُ فَيَعْلَمُ أَنَّهَا مِنْ عِنْدِ اللَّهِ فَيَرْضَى وَيُسَلِّمُ

‘Alqamah amesema: “Huyo ni yule ambaye anapopatwa na msiba hutambua kwamba umetoka kwa Allaah kisha akaridhika na akasalimu amri.”

 

وَفِي صَحِيحِ مُسْلِمٍ عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ)  قَالَ: ((اِثْنَتَانِ فِي النَّاسِ هُمَا بِهِمْ كُفْرٌ، الطَّعْنُ فِي النَّسَبِ، وَالنِّيَاحَةُ عَلَى الْمَيِّتِ))

Na katika Swahiyh Muslim kutoka kwa Abuu Hurayrah (رضي الله عنه  kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Mambo mawili hupelekea kufru miongoni mwa watu; kukashifu nasaba yake na kumlilia maiti – kuomboleza)) [Muslim]

 

وَلَهُمَا عَنِ اِبْنِ مَسْعُودٍ (رضي الله عنه) مَرْفُوعًا: ((لَيْسَ مِنَّا مَنْ ضَرَبَ الْخُدُودَ وَشَقَّ الْجُيُوبَ وَدَعَا بِدَعْوَى الْجَاهِلِيَّةِ)) متفق عليه

Imepokelewa kutoka kwa Ibn Mas’uwd (رضي الله عنه) Hadiyth Marfuw’: ((Si miongoni mwetu anayejipiga mashavu, akapasua mifuko na akaomba maombi ya kijaahiliyyah)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

وَ عَنْ أَنَسٍ (رضي الله عنه)  أنَّ رَسُولُ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم) قَال: َ((إِذَا أَرَادَ اللَّهُ بِعَبْدِهِ الْخَيْرَ عَجَّلَ لَهُ الْعُقُوبَةَ فِي الدُّنْيَا، وَإِذَا أَرَادَ اللَّهُ بِعَبْدِهِ الشَّرَّ أَمْسَكَ عَنْهُ بِذَنْبِهِ حَتَّى يُوَافِيَ بِهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ))

Kutoka kwa Anas kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Allaah Anapompendelea mja Wake khayr, Humharakishia adhabu yake duniani. Na Allaah Anapomtakia mja Wake shari Humzuilia dhambi zake Amlipe Siku ya Qiyaamah [Amuadhibu huko])) [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah] 

 

 وَ قال النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((إِنَّ عِظَمَ الْجَزَاءِ مَعَ عِظَمِ الْبَلاءِ وَإِنَّ اللَّهَ إِذَا أَحَبَّ قَوْمًا ابْتَلاهُمْ فَمَنْ رَضِيَ فَلَهُ الرِّضَا وَمَنْ سَخِطَ فَلَهُ السَّخَطُ)) رواه الترمذي وقال حديث حسن

((Hakika jazaa kubwa ipo ni kwa balaa kubwa na hakika Allaah Akiwapenda watu Huwajaribu kwa mtihani. Basi atakayeridhika Allaah Atamridhia na atakayechukia atapata ghadhabu Zake)) [At-Tirmidhiy na amesema Hadiyth Hasan]

 

 

Masuala Muhimu Yaliyomo:

 

1-Tafsiri ya Aayah katika Suwrah At-Taghaabun (64:11).

 

2-Hili (Kukubali Qadhwaa na Qadar ya Allaah سبحانه وتعالى) ni sehemu ya iymaan halisi kwa Allaah (سبحانه وتعالى).

 

3-Mtu kukashifu nasaba yake.

 

4-Adhabu kali iliyoahidiwa kwa wanaojipiga mashavu, kuchana nguo na akalia kwa maombolezi ya kijaahiliyyah.

 

5-Dalili kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Anamtakia khayr mja Wake.

 

6-Dalili kuwa Allaah (سبحانه وتعالى) Anamtakia shari mja Wake.

 

7-Dalili ya mapenzi ya Allaah (سبحانه وتعالى) kwa anayemuabudu.

 

8-Ubaya wa kutokuridhika na Qadhwaa na Qadar ya Allaah (سبحانه وتعالى).

 

9-Fadhila na thawabu za kukubali mitihani ya Allaah (سبحانه وتعالى).

Share